Mwanakijiji na Uislamu wa TAA/TANU mpaka CCM

Kwanini awatoe hao kwenye nyekundu tu na asiwataje wengine waliobakia ilhali tunawajua wa majina na idadi yao? hebu jiulize halafu utajua alichokikusudia ili makala yake inoge!

Hata kama angewataja wote kama unavyotaka wewe iwe bado, haiondoi ukweli kwamba waislamu wengi walishiriki kuianzisha TAA/TANU/CCM lakini hawakuanza harakati zao kwa malengo ya kidini bali kwa ajili ya ukombozi wa Tanganyika, na hawakuwabagua watu wasio wa dini yao, hadi wakakubali kumpisha kijana mkristu Nyerere kuchukua uenyekiti wa TANU. Enzi hizo hakukuwa na ubaguzi kama leo mnavyowaita wenzenu kafiri, kwakuwa waislamu wa enzi zile walikuwa watu safi hawakuwa wanafiki.

Ili makala inoge ni katika kuweka ulinganifu (differences and similarities) wa pande mbili, au tatizo lako hukutaka hoja inoge?? Kama hoja ya mwanakijiji isingenoga bilashaka usingepata elimu kama ulivyoipata.
 
Siwezi kumwelewa kwa kuwa alichokiandika kwangu mimi hakipo kwenye historia ya kweli ya TAA mpaka CCM amesema TAA mpaka CCM ilijaa waislam watupu hapo ndio kweli sijamwelewa kwani kulikuwa na wakristo kama kina Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr Joseph Mutahangarwa, Dr Wlibard Mwanjisi, Dr Michael Lugazia na Dr Luciano Tsere, patrick kunambi, gerimano pacha, japhet kirilo na l.m. Makaranga.bila kuwashau joseph kimalando na john rupia.

Kwa kifupi amepika history!

Ndugu Mohammed Shossi,

Kwani chadema imejaa wachaga watupu na wakristo watupu? mbona kinaitwa chama cha kichaga na kikiristo tena wanakuwa specific wakatoliki! sasa hata hivyo mwanakijiji ameliongelea kinaga ubaga, au mzee kila neno uislamu likitajwa unafikiri upo kwenye mihadhara kuwa lazima utetee tuu hata kama huna la kutetea, kama kwenye thread ya MM nanukuu Kama ifuatavyo:

Mapinduzi kilipoasisiwa (wakati huo kikiitwa TANU na ASP) viongozi wake wengi
walikuwa ni Waislamu. Hili siyo siri. Kwa upande wa TANU viongozi waanzilishi
wake kabla hata Mwalimu Nyerere hajahamia Jijini Dar na kuanza shughuli za
kisiasa rasmi walikuwa ni Waislamu maarufu wa Jiji la Dar ambao majina yao
yalikuwa yakijulikana wakati huo.
Miongoni mwao tunaowakumbuka leo hii ni
familia ya Sykes (maarufu kati yao akiwa ni Abdulwahid Sykes na kaka zake Ali na
Abbas), masheikh maarufu wa Jiji la Dar es Salaam kama kina Sheikh Hassan bin
Amir, Sheikh Chaurembo na mzungumzaji maarufu, Sheikh Suleiman Takadir.
Kwa
madhumuni ya hoja yangu siwahesabu Wakristu kama John Rupia, Vedasto Kyaruzi au
Stephen Mhando ambao nao ni waasisi wa TANU kama vile ambavyo sitawahesabu watu
wengine ambao hawakuwa Wachagga lakini walishiriki katika uasisi wa CHADEMA kama
kina mzee Brown Ngwilulupi, Jacob Nkomola na Bob Makani. Tukiwaingiza hao
wengine hoja yetu haitanoga.
Ni Waislamu hata hivyo waliokuwa na nguvu zaidi
ndani ya TANU kutokana na nafasi zao na uwezo wao wa kifedha katika Jiji la Dar.
Walitumia mali na nafasi zao kuweza kukijenga chama na wengine walitoa hata
nyumba zao kwa ajili ya matumizi ya TANU.
Kitabu cha Mohammed Said cha Maisha
na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968): Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati
Za Waislam Dhidi Ya Ukoloni Wa Waingereza Katika Tanganyika kinaelezea kwa kina
jinsi Waislamu walivyokuwa na nafasi ya pekee katika kuanzishwa kwa TANU kiasi
kwamba sehemu mojawapo Said anatangaza pasipo shaka wala kujiuma meno kuwa
"Kimsingi Chama cha TANU kilikuwa ni chama cha Waislamu".
Lakini siyo
kutokana na uasisi wake tu ndio maana TANU ilikuwa ni chama cha Waislamu bali
pia eneo lake ambapo kilikuwa na nguvu sana. Kama CHADEMA kuwa na nguvu kwa muda
mrefu mikoa ya Kaskazini kutokana na kukubalika zaidi maeneo hayo TANU nayo
ilikuwa na nguvu sana katika maeneo ya Pwani na maeneo ambayo yalikuwa na
Waislamu wengi kama Tabora, Tanga na Dar yenyewe.
Hivyo, kilikuwa ni chama
cha Waislamu siyo kutokana na uasisi wake tu bali pia kutokana na maeneo yake
ambayo kilikuwa kimekubalika zaidi kwani hata katika maeneo hayo mengine ni
viongozi wengi wa Kiislamu waliokuwa wakijitokeza kukiunga mkono.
Vile vile
CCM baada ya kuundwa kufuatia kuunganishwa kwa ASP na TANU kilijikuta kimepokea
viongozi wengi ambao ni Waislamu kutoka Zanzibar na matokeo yake hadi leo hii ni
rahisi kuona kuwa Kamati Kuu inachukua wajumbe wengi kutoka Zanzibar kwa mujibu
wa Katiba ya CCM kitu ambacho kinasababisha chama hicho kuwa na Waislamu wengi
kwenye Kamati Kuu kutoka na wingi wa Waislamu wanaotoka Zanzibar.


Mwanakijiji Msamehe bure huyu ndugu yetu amezoea kubisha tu bila mantiki nadhani ndo amefundishwa hivyo madrasa kuwa uislamu unapotajwa wewe bisha tu hata bila mantiki. soma hapo kwenye bold majibu yako yapo hapo na jalibu kutafakari na kupata maana ya mantiki ya mwanakijiji.

CCM wanapowashutumu chadema ni chama cha wachaga huwa wanawaficha am kuwapuuza kuwa hawapo wanachama na viongozi wengine wa chadema ambao sio wachaga, na ccm wanapotoa propaganda kuwa chadema ni cha wakatoliki wanawaficha ama wanawapuuza wanachama wengine ambao sio wakatoliki wala wakristo, hivyo kwa dhana hiyo hiyo na mtazamo huo huo wa ki propaganda za ccm mwanakijiji aliwaficha wakristo wachache ambao ni miongoni mwa waasisi wa TAA/TANU/CCM ili kujenga dhana ile ile inayotumiwa na ccm kuwashutumu chadema. na mwanakijiji katanabaisha hapo juu. sasa ubishi wa kwenye mihadhara unatoka wapi ndugu?
 
Ok mkuu, labda kwa maswali tutaelewana:

  1. Kati ya wakristo na waislamu,ni wepi hasa walikua vinara waanzilishi wa TAA hadi TANU hadi CCM? Kama ni waislamu,basi umwelewe sasa MKJJ. Kama ni idadi sawa,basi nithibitishie. Na Kama ni wakristo,je nikisema kuwa ndio maana "waliwaweka pembeni waislamu baada ya uhuru" kama wanazuoni wengi wa kiislamu wanavyosema,nitakua nasema urongo?
  2. Kama MKJJ akiwarudisha wakristo "wazalendo" wote kwenye orodha yake,halafu akawarudisha na waasisi wote wa CDM wasio wakristo na wasio wachaga,je utaamini kwamba CDM si cha kikristo na si cha kichaga kama ilivyo CCM?
Pamoja mkuu!

mshindo hapa umemkamata pabaya na najua hatajibu hya maswali ataleta maneno na siasa
 
Kwanini awatoe hao kwenye nyekundu tu na asiwataje wengine waliobakia ilhali tunawajua wa majina na idadi yao? hebu jiulize halafu utajua alichokikusudia ili makala yake inoge!

Soma Upya article mama ya Mwanakijiji utajiona ulivyo Ngumbaru! Unashindwa elewa vitu vyepesi vigumu je?
 
Mimi sipo upande wa kutetea chama wala mtu natetea historia ya kweli napinga wakristo wazalendo waliopigania uhuru kusilimishwa na watu kama kina Mwanakijiji!

Sasa kama unataka kuonyesha kuwa Chadema ni chama cha wachaga na Kikristo, je na wewe huoni kuwa ndani ya Chadema kuna watu wa kabila na dini nyingine?
Mwanakijiji ametengeza logic kuwa kama ukiangalia Chadema kama chama cha wachaga na Kikristo, Kama viongozi wa CCM wanavyosema, Basi ni sawa pia kukiangalia CCM kama ni Chama cha Kiislam, kwa mantiki ya kuwa waanzilishi na viongozi mashuhuri walikuwa wengi waislam.
Hakutoa conclusion na ndio mana kwenye kichwa cha habari aliweka alama ya kuuliza (?).
Hivyo usitake kupotosha maana, ni vyema ungeuliza uweze kueleweshwa kuliko kuja kwa KUFOKA na kulaumu JF ati inatumiwa na Chama.

After all hata kama JF inatumiwa na Chama fulani ni haki wao mana huu ukumbi sio wa serekali, ni watu walikaa na kufikiria na kuanzisha mambo yao, so ukiona wanaegemea upande ambao huupendi anzisha forum yako.... mbona zipo nyingi?
 
Mimi nilimuelewa vizuri MMK alichomaanisha.Ukirudia kumsoma utatambua alitumia mfano huo ili watu wasipotoshwe
 
........nadhani ungejikita zaidi katika kupambanua vipengele vya comparison (differences & similarities)


Uko Juu Mkuu!,
 
Siwezi kumwelewa kwa kuwa alichokiandika kwangu mimi hakipo kwenye historia ya kweli ya TAA mpaka CCM amesema TAA mpaka CCM ilijaa waislam watupu hapo ndio kweli sijamwelewa kwani kulikuwa na wakristo kama kina Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr Joseph Mutahangarwa, Dr Wlibard Mwanjisi, Dr Michael Lugazia na Dr Luciano Tsere, patrick kunambi, gerimano pacha, japhet kirilo na l.m. Makaranga.bila kuwashau joseph kimalando na john rupia.

Kwa kifupi amepika history!

Shossi kwa vile umechagua kutokuelewa nilichoandika itabidi nikusaidie tu kwa moyo mkunjufu :


  1. Nukuu kwenye andiko langu la awali ni wapi nimesema kuwa "TAA mpaka CCM iilijaa Waislamu watupu"?Mohammed Said katika kitabu chake cha Abdulwahid Sykes anasema "TANU kuanzia mwanzo kilikuwa ni chama cha Waislamu" unakubaliana naye? - si maneno yangu hayo.
  2. Kwa vile umeweza kuonesha kuwa walikuwepo Wakristu katika TANU kitu ambacho mwanahistoria yeyote wa Tanzania anajua vizuri sana na kutokana na uwepo wake ina maana Mohammed Said amepotosha kwenye kitabu chache. Kama hili ni kweli TANU ilianzishwa kwa ushirikiano sawa wa Wakristu na Waislamu na dini zao hazikuwa sababu ya kujiona kuwa wanamiliki chama kwanini kitabu cha Mohammed Said kinaaminiwa na wapo wanaoamini kuwa ni "Waislamu ndio walioanzisha TANU" wakati kulikuwepo na Wakristu ambao tunawajua "majina na hata idadi yao"?
  3. Kama kuwepo kwa Wakristu ndani ya TANU kunafuta dhana ya TANU kama chama cha Waislamu kitu ambacho nakubaliana nacho (ndio maana nilisema hoja ya kuwa TANU ni chama cha Waislamu haina nguvu pale utakapoingiza Wakristu wake ndani yake) inakuwaje kuwepo kwa Watu wasio Wachagga ndani ya Chadema isivunje hoja ya Chadema kuwa ni chama cha Wachagga?
  4. Sote tunajua vizuri tu kuwa hakuna chama nchini ambacho kimeundwa kikiwa na watu wa dini moja, sehemu moja au kabila moja tu. HAKUNA. Lakini wapo watu walioafanikiwa kuwashawishi watu kwamba kati ya vyama vyote nchini ni Chadema ndicho ni cha "Wachagga, Wakristu na watu wa Kaskazini". Hata hivyo tunajua wapo Waislamu, Wasukumua na Wakerewe, Wahehe na Wangoni n.k na wapo watu wa Kusini (hadi MBozi na Katavi) n.k lakini pamoja na yote hayo kujulikana lakini bado watu wanaamini kuwa Chadema ni chama cha kidini, kikabila na kikanda?
  5. Umehamaki kuona kuwa nimewashambulia Waislamu; hivi unafikiria Wachagga wanajisikiaje wanaponyoshewa kidole na viongozi na wananchi wenzao ? Au mnafikiri Wachagga nao hawana hisia? Mnataka Wachagga wasijiunge na Chadema kwa sababu wakifanya hivyo watakuwa wanaonesha kuwa ni chama chao? Mnataka Wachagga, Wakristu na watu wa Kaskazini wanaotaka kujiunga na Chadema wakataliwe, waliopo wahesabiwe, na wenye nafasi mbalimbali waziachie kama mtu mmoja alivyowahi kupendekeza humu ili kufanya chama kisionekane cha "kikabila, Kikristu na Kikanda?
 
Mimi sipo upande wa kutetea chama wala mtu natetea historia ya kweli napinga wakristo wazalendo waliopigania uhuru kusilimishwa na watu kama kina Mwanakijiji!

Guys, tusipoteze bidhaa adimu kama nguvu zetu kupigania mambo yasiyo na tija. Udini ni silaha ya watu wababaishaji nashangaa kwanini tunaupenda na kuushupalia kama kuna lolote la maana tunalopata mwisho wa siku.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hapo kwenye red mkuu sikubaliani na wewe mwenye kujua na aliesoma kama wewe hawezi kusema eti TAA/TANU mpaka CCM ni chama cha waislamu ikiwa kulikuwa na wakristo kindakindaki kama madaktari watano – Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr Joseph Mutahangarwa, Dr Wlibard Mwanjisi, Dr Michael Lugazia na Dr Luciano Tsere, patrick kunambi, gerimano pacha, japhet kirilo na l.m. Makaranga.bila kuwashau joseph kimalando na john rupia.

Kwahiyo kimantiki Mwanakijiji analo alilokusudia na si jingine ila kuipembejea CDM na kuutukanisha Uislam! Kama alikuwa na haja na hoja ya kuisafisha TAA/TANU na CCM na waenyeji wa Dar es Salaam ambao ni Wazaramo ila aliona kuwa kina Sykes hawakuwa Wazaramo ametumia ufundi kuisuka hoja yake ili afanikishe malengo yake! Narudia hakututendea haki Waislam mimi nikiwa mmoja wao kwa kuufananisha Uislam na Uchagga ambao ndani ya huo Uchagga kuna waislam pia!

Shukran sana kwakuwa wewe mwenzetu umeenda sana shule na uimekusaidia sana nadhani utakuwa unaelewa mantiki ya mada yangu.

Ulimsoma ukamwelewa ama ulivyoona jina lake tu na mada aliyoweka uka draw conclusion? Maana unaweza ukawa uli pick neno Mwanakijiji and Waislamu ukaanza ku draw conclusion bila kuangalia kuwa Mwanakijiji alishatuambia aliamua kuwaondoa akina Bob Makani ambao si wachagga na ni waanzilishi CHADEMA na kubakiza wale watuhumiwa tuu kama ilivyo kwa wakristo wa CCM nakuwabakiza watuhumiwa Waislamu waanzilishi...Ebu karudie hii para alafu angalia conclusion yako kisha uje utu convince kuwa Mwanakijiji kasema waanzilishi wa CCM ambao umewatetea na kuicha CHADEMA bila utetezi implying unakubaliana na kuwa CHADEMA ni ya wachagga!

wengine tunaona umei personalize sana hili kwa UISLAMU na Mwanakijiji labda utusaidie kama huna own reservation kwenye hizo concept mbili (Mwanakiji=Personality; Uislamu=faith) ulizotumia kufikia conclusion yako
 
Hii ndio JF kaka wengine wanasema tawi la chama ila mie sijaamini bado.

- Mkuu heshima yako sana, haya maneno hata CCM sasa imeshathibitsha kwamba hayana ukweli wowote isipokuwa yalisemwa na wavivu wa kufikiri na kutafiti, ambao Mwenyekiti Mao aliwahi kuwasema kwamba " No research no right to speak", sasa kuendelea kuyaimba imba kila wakati ni kuimba wimbo wa hao wazembe wa kufikiri, imesemwa mara moja kwa makosa imerekebishwa, now we move foward!

- Ukiweka thread mpya ikipotea watafute Mods wakusaidie sababu, lakini sweeping statements bila facts sio dalili za busara kama unavyojaribu kuonekana kwenye post zako, wanapokusachi Airport kabla ya kuingia kwenye ndege haina maana kwamba wewe ni Osama au wewe ni mwizi, hapana ni utaratibu tu, kama huridhiki nao unaenda kunakopaswa kwa wahusika na unasema tatizo lako, lakini hupigi kelele publicly kwamba hawa wanaonisachi wanafikiri mimi mwizi!

- I mean vipi mkuu mbona post zako zinaonekana kuwa makini isipokuwa tu hizi sweeping statements!

Field Marshall Es!
 
Penye red, kwanza mimi sikujua kama Mohammed Shossi ni Muislam, pili nazidi kuamini kwamba Waislam wanatumia mda mwingi kupigania uislam

Ni haki yao (Waislamu) kuipigania imani yao maana ndiyo inayounda personality zao ila tatizo ni kuwa je wanapoipigania wako within a scope ya mambo ya imani ama wanaenda out of range? Leo mimi nikienda msikitini nakuanza kuwaambia waendeshe msikiti kufuata siasa ya chama fulani ama any other rules and regulation nje ya islamu waislamu wasipoipigania imani yao hapo hata mm nitawashangaa lakini inakuaje wachache wao wanaipigania mpaka kwenye institutions ambazo hazihusiani na religiousity kama vyama vya siasa? Hapo ni haki yangu kama raia wa Tanzania kuipigania nchi yangu isipelekwe kwenye mrengo wowote ule nje ya jinsi tulivyokubaliana kikatiba. Kama tutakubaliana tena vinginevyo that is subject to discussion lakini si sasa ambapo bado hatuja kubaliana na bado tuko bound na makubaliano ya kikatiba tuliyo i legitimize.
 
Siwezi kumwelewa kwa kuwa alichokiandika kwangu mimi hakipo kwenye historia ya kweli ya TAA mpaka CCM amesema TAA mpaka CCM ilijaa waislam watupu hapo ndio kweli sijamwelewa kwani kulikuwa na wakristo kama kina Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr Joseph Mutahangarwa, Dr Wlibard Mwanjisi, Dr Michael Lugazia na Dr Luciano Tsere, patrick kunambi, gerimano pacha, japhet kirilo na l.m. Makaranga.bila kuwashau joseph kimalando na john rupia.

Kwa kifupi amepika history!

Asante kwa kuleta tena hii historia, ila uchambuzi wako haujakamilika.
Kulingana na historia uliyoileta, kuanzia 1929 mpaka 1951 (miaka 22) TAA ilikuwa na wakristo viongozi wangapi?
na CDM ina umri wa miaka mingapi, na katika umri huo imekuwa na viongozi wote kabila au dini moja?

Kila chama kilichpo kimetimiza mashariti yaliyowekwa na katiba. ikiwa ni pamoja na kuwa vyama visivyo vya kikabila na kidini.
Hata mwanakijiji amsema hayo. kama hujaelewa rudia tena kumsoma vizuri mwanakijiji.
 

Ndugu yangu kwa Mwanakijiji.

Kwa watu makini makala yako ni moja ya utumiaji kalamu kupotosha jamii makala yako imebaka historia ya kweli ya TAA/TANU na sasa CCM kama nilivyoeleza mwanzo pengine mapenzi ya chama kimoja wapo ndio mapenzi hayo yamekusukuma kuinanga historia ya kweli.


Mohammed Shossi.


na kwa watu makini thread yako imejaa utetezi (mapenzi) wa kidini bila kuangalia mwanakijiji alitaka kuonyesha nini kwa jamii.

tumekuwa tukiimbiwa kila siku chadema ni ya wachaga kisa tu ni waanzilishi wake wengi kuwa wachaga na nikisoma thread yako bado naona waanzilishi wengi wa TANU/TAA and CCM ni waislamu sasa je hiyo inaifanya ccm kuwa ya waislamu?

ukipata jibu la swali hapo juu pia angalia mtazamo huo huo kwa chadema kwa ile hoja ya uchaga na chadema. mwanakijiji alitaka jamii ijue kuwa hizi propaganda hazina tija bali tu zipo kupotosha umma na kuendelea kututawala kwa "divide and rule strategy".
 
Nilikuwa namheshimu sana huyo Mwanakijiji lakini kwa makala yake hiyo amepoteza kabisa heshima yake kwangu.
Kumbe yeye ni tool ileile inayoutumiwa na kundi moja la watanzania kuwakandamiza wengine!.
Tangu lini CCM ikafungamana na Waislamu? Waislamu wamenyanyaswa sana na kukandamizwa na hicho cha wakishirikiana na kanisa.
Kumbuka MOU nyingi zilisainiwa na makubaliano mengi yakunufaisha kanisa yalifikiwa na chama hicho kwa manufaa ya wakristo wa watanzania.
Kuwafungamanisha waislamu na CCM ni sawa na kuwatukana waziwazi!

Nakubali kwa siku za karibuni waislamu wameonyesha kama kuunga mkono serikali ya Kikwete. Ieleweke vema hapa waislamu hawaungi mkono CCM bali wanamtetea Rais ambaye anasakamwa kwa sababu ya dini yake.
Kwakuwa wakristo waliamua kumsakama Kikwete kwa kutumia Chadema, by default Waislamu watakuwa upande wa pili!.
N.B Kwanini Mwanakiji hakulaumu swala la UKRISTO ndani ya Chadema badala yake kakimbilia uchaga! Pia udini haupimwi kwa majina ya viongozi! bali ni dhamira za Chama!
Chadema ni tool ya kanisa hilo halina ubishi hata muandike makala ndefu kiasi gani!
Siyo kweli kuwa JK amenyanyaswa kwa kigezo cha udini, bali kwa kigezo cha kufumbua macho baadhi ya mambo ambayo hayakustaili. Pia hali ya maisha imekuwa ngumu na serikali ya JK imeshindwa kutoa majibu yenye kuingia akilini. Hivyo CDM kama chama cha siasa kililiona hilo na kulichukua kama mtaji wa siasa. Baada ya Jk kuona hana pa kushika akaamua kutumia hoja hiyo kama advantage kwake lakini udini haupo CCM wala CDM lakini upo kwa kujengwa na wanasiasa.
 
kinachonishangaza pia ni kuwa watu wameshindwa kusoma hiyo alama ya 'kuuliza' ambayo ilikuwepo kwenye makala tangu mwanzo na hawajajiuliza kwanini sikuiweka kama statement of fact. Mada nzima ni swali wala haitoji jibu lakini kwa anayelisoma hilo swali anapata jibu ndani yake. Lakini watu wamekuja juu na kufikiria nimesema CCM ni chama cha Waislamu na Chadema chama cha Wachagga. Wanasahau hata ufunguzi wa hoja yangu umewekwa kwenye misingi ipi: NImeanza hoja kwa kusema hivi:


CHADEMA ni chama cha Wachagga na CCM ni chama cha Waislamu. Huwezi kukubali moja ya hilo na ukakataa jingine. Vigezo vinavyotumiwa na baadhi ya watu kuitaja CHADEMA kuwa ni chama cha Wachagga tukivikubali bila kutumia uwezo tuliojaliwa na Mwenyezi Mungu kuvihoji basi vinatusukuma kama mkokoteni ulioachiliwa kwenye mteremko na shehena ya madafu kufikia hitimisho kuwa CCM nayo yaweza kabisa kutajwa kuwa ni chama cha Waislamu.

Hivi ni gumu sana kujua maana ya kujenga hoja ya kimantiki na kuonesha ukweli kwa kutumia kuizungusha lugha?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
simple question kwa mwanakijiji. kwanini usiseme ccm na waislam. cdm na wakiristo: umerukia jamii ndogo ya wachaga?

Soma vizuri makala ya mwanakijiji hilo la kusema chadema ni chama cha wakristo ameliongelea pia

kama hujasoma kwa makini makala ya mwanakijiji usikurupuke kutoa shutuma, mimi nimeisoma mara tatu kujaribu kuilewa vizuri,

nakuomba uisome tena ndugu, ulilouliza limo pia.
 
Back
Top Bottom