Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,546
- 851
fitna iko hapa:
issamichuzi.blogspot.com/
issamichuzi.blogspot.com/
michuzi Blog said:salamu toka bongocelebrity.com
wadau kunradhi,
leo nimepokea ujumbe maridhawa toka bongocelebrity.com ambao mhusika alisita kuutundika na badala yake kaamua kunitumia kwanza kuulizia kama autundike ama la. mie sio tu nimemruhusu autundike kama ulivyo bali pia nimeuweka hapa pia ili aliyeandika apate kuridhika na roho yake. Ila tatizo kaandika kama ni kwa niaba ya wadau wote na si yeye binafsi. Je ni kweli anawasemea enyi wadau wote wa globu hii ya jamii?
Hii ni hoja ambayo kama anavyosema mwandishi itabidi ijibiwe kwa hoja, hasa ukizingatia kwamba mtu kama yeye hata kama kaandika kwa nia ya kujeruhi watu anataka lazima hoja yake iwekwe hewani huku hashangai kuona wenzie ambao ni wastaarabu hawawekewi ribiti. Na je, kuna ubaya gani kuwa tarishi wa mdau kama mwanakijiji ambaye, kama wanvyofanya wadau wengine, hupenda kutumia globu hii kupitishia ujumbe wao kama mdau yeyote yule?
Namsihi mwandishi huyo kwamba endapom kama ana matatizo na wadau wa globu hii ya jamii asinishirikishe kwenye ugomvi wake kwa njia yoyote ile, maana ukisoma katikati ya mistari utaona dhahiri hana nia njema na mwanakijiji ambaye si mdau pekee anayepitishia ujumbe wake humu mara kwa mara. kwa kifupi wadau, nikiwa mtumishi wenu ama tarishi ambaye hauwawigi, mna maoni gani juu ya maoni ya huyu mdau ambaye hata jina kalificha wakati yeye mwenyewe ni hodari kutaja ya wenzie?
kwa upande wangu hii ni moja ya changamoto nyingi nilizokumbana nazo muda wote toka niende hewani na kwa taarifa yako mwandishi hivi ndivyo vitu vinavyonitia moyo na si kunivunja, kwani naelewa fika kwamba 'kizuri kwa bata mzinga, ni kibaya kwa kuku' na sio rahisi kumridhisha kila mtu hata uweje!
ujumbe wa huyo mdau ni kama ufuatavyo:
MICHUZI USITUMINYIE 2008 VINGINEVYO TUTAHAMA !
Kama kawa Issa Michuzi amechemsha huko kwenye blogu yake mpaka akatupiwa taulo eti alidhani Boxing Day inahusiana na masumbwi akakurupuka na kuandika habari za Japhet ambaye ubingwa wake wa Dunia haupo popote katika rekodi za dunia.
Tunamuelewa sana Michuzi anapotumia tungo kama mai hasband wako na majina kama ukerewe, A-town, n.k Lakini kwa hili si utani wala hasijifanye kuwa alikuwa anachekesha maana huwezi kuweka post nzima na picha ya watu kwa utani.
Michuzi Jr mtupie taulo huko ndugu yetu kwenye hii link:http://issamichuzi.blogspot.com/2007/12/boxing-dei.html#comments
La pili ni kuwa Michuzi (senior) ambaye ndiye huwa anamtumia taarifa zote Mzee Mwanakijiji wa USA (Mpelelezi) ana utofauti mkubwa sana na Michuzi (Junior) ndio maana wengine tumeamua kuhamia huku kuliko kwenye blogu yake ambayo ana amua bila sababu kuzuia comments za watu na wakati hujaandika matuzsi yeyote kama nilivyoandika sasa.
Michuzi (senior) inabidi ukue kiuandishi, hoja zijibiwe kwa hoja na siyo kumminyia mtu comments zake. Hapa sina haja ya kuomba eti haya niliyoyaandika yawekwe ni dhahiri yanawekwa maana ni kwa ajili ya kuboresha namna ya kuhabarisha watu na pia sijaandika tusi lolote.
Kama nimeongea vibaya naomba msamaha na nisahihishwe hapa hapa.N.B nendeni jambo forums muone jinsi ambavyo huyo mzee Mwanakijiji pamoja na mazuri yake mengi amejikweza kiasi mpaka anaonekana kuwa yeye ndiye chanzo cha habari zoooote na kwamba yeye hasahihishwi na pia kuwa anajua kila kitu cha fani zote ulimwenguni kuanzia uvuvi wa dagaa mwanza hadi ubunge hadi thesis defence hadi mapenzi ya mfano hadi hard science fiction! Hadi Leo yeye anajiita mpinzani wa kweli lakini utambulisho wake haujulikani na kuna mtu aliandika hapa mambo yake lakini yeye akatetewa kuwa hana haja ya kujibu wakati motto yake at KLH News ni kuwa kila kitu kinazungumzika na hoja hujibiwa kwa hoja. Mimi napenda kusoma na kujifunza mambo ambayo wengine huandika lakini sipendi mtu anapojinyanyua mpaka karibu kujivika uungu mdogo katika fani ya uandishi.
Samahani kwa kuwapotezea muda wakati wa siku ya kupeana zawadi.