MwanaJF jiulize umepata nini kipya kila utumiapo mtandao wa kijamii

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
44,565
188,766
Habari za mihangaiko.

Mazingira yoyote yale unapokuwepo binadamu unaweza kupata kitu chochote chanya (Faida) au hasi (Hasara).

Hapa twende moja kwa moja mfano, hapa JamiiForums kuna watu wa tofauti tofauti sana na wana mitazamo mbalimbali.

Wewe unapoingia humu kuwa na lengo hata moja tu la kupata kitu kipya chenye mantiki. Unakuta mtu anasema "walahi Jf sihami" ukifuatilia nini kinamfanya aseme hivi? Unakuta kuona kumbe ni umbea /member aliyejitoa ufahamu kuandika upumbafu/ nk.

Ila kwa makini angetulia na kutafakari kuna majukwaa mangapi humu Jf angeweza kupata tip hata moja mpya mfano kama ni mfanyabiashara angepata mawazo mengine mengi mapya toka humu.

Kuna vijana kabla ya kuingia Jf labda alikuwa vizuri kwenye programming ila kaingia huku kasombwa na upepo wa MMU anasahau kujifunza kitu kipya wakati kuna mambo mazuri sana Jukwaa la Science & Tech.

Mara nyingi ukitumia muda mwingi kwenye mambo yasiyo ya msingi akili yako itawaza hayo hayo.

Mtu anabaki kushangaa kwanini huyu member yupo vizuri kwenye haya masuala? Jibu wakati alipokuwa kama wewe alijifunza. Wewe wakati huu unafanya nini?

Kuna majukwaa mengi sana jaribu kutumia hata dakika 15 kila siku kupata kitu kipya then endelea na huko unaposema una-refresh.

Humu ndani wakati huu unaweza kujifunza bure kabisa ila baadae maarifa hayo watu watakuja nunua kutoka kwako.

Nawasilisha.

Siku njema!

Cc. Kichwa kichafu
 
Mkuu Kujisomea mambo ya kuongeza maarifa sio kawaida yetu vijana wa 90's n 20's..Angalia views na Reply za threads zenye kuelimisha utajione. Sie vijana tushachagua zetu ujinga tunapenda kwenda location kupiga picha. Alpha generation inaweza kua ndio kizazi cha hovyo kuwahi kutokea hapa duniani
 
mimi jukwaa la mapenzi ndo kipaumbele..vijana wa kubet....biashara napita bila ku comment.uko kwingine nawaachia wengine
Tafuta hata dakika 5 kujifunza kitu kipya.
Si kila siku unasema lazima u-invest pesa ili ufanike.

Bali unahitajika ku-invest muda ili upate hayo hayo mafanikio.

Ila si jambo baya kupita huko ulipoweka kambi.
 
Tunakuja kukumbuka muda tayari umetutupa mkono.
Mkuu Kujisomea mambo ya kuongeza maarifa sio kawaida yetu vijana wa 90's n 20's..Angalia views na Reply za threads zenye kuelimisha utajione. Sie vijana tushachagua zetu ujinga tunapenda kwenda location kupiga picha. Alpha generation inaweza kua ndio kizazi cha hovyo kuwahi kutokea hapa duniani
 
Back
Top Bottom