Mwanajeshi wa Korea Kaskazini ahamia K. Kusini kwa kuogelea

nankumene

JF-Expert Member
Nov 12, 2015
5,916
2,000
Mwanajeshi wa Korea Kaskazini ahamia K. Kusini kwa kuogelea
upload_2017-6-19_0-24-38.jpeg

Image caption Ramani ya Korea kaskazini
Mwanajeshi mmoja wa Korea Kaskazini ametorokea Korea Kusini kupitia kuvuka mto Han kwa kuogelea ,ikiwa ni mara ya pili kwa raia wa taifa hilo kuhamia kwa majirani zao.

Mkuu wa Jeshi nchini Korea Kusini amesema kuwa mwanajeshi huyo aliogelea na kupitia eneo moja jembamba sana la maji ya mto huo yalio na kasi kubwa baada ya kuvalia boya lilolomsaidia kuelea.

Wiki iliopita mwanajeshi mwengine wa Korea Kaskazini alipitia mpaka unaolindwa sana unaogawanya mataifa hayo mawili.

Wanajeshi walikuwa wakihamia Korea Kusini katika kiwango cha mmoja kwa mwaka.

Mwanajeshi huyo aliyedaiwa kuwa na miaka ya ishirini alipatikana katika eneo la Gimpo, Magharibi mwa mji mkuu wa Korea Kusini Seoul, kulingana na chombo cha habari cha Yonhap.

Alipiga kelele akisema ''musiniue'', niko hapa kuhama ,kwa mwanajeshi wa Korea Kusini ambaye alikuwa amemuona, kilisema chombo cha habari cha Yonhap.

Mwanajeshi huyo sasa atahojiwa na maafisa wa kijeshi.

Korea Kaskazini na Kusini ziko katika vita baradi tangu mzozo kati yao umalizike 1953 kupitia makubaliano.

Seoul inasema kuwa zaidi ya raia 30,000 wa Korea Kaskazini wamehamia kusini tangu kumalizika kwa vita vya Korea, wengi wao kupitia China ambayo ina mpaka mrefu na Korea Kaskazini.
Mwanajeshi wa Korea Kaskazini ahamia K. Kusini kwa kuogelea - BBC Swahili
 
MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
18,848
2,000
Bora wasimtaje majina maana ndugu na jamaa zake aliowaacha watapokea kibano ili iwe funzo kwa yeyote mwenye mawazo kama hayo.
Lakini pia wawe makini naye asiwe ametumwa kuwazuga tu ili asaidie katika maandalizi ya vita.

Inafaa ifahamike nchi hizi mbili bado zipo kwenye vita, hawakutia saini makubaliano ya amani ila walisitisha vita. Hivyo ina maana kwa lugha za kijeshi, wapo bado kwenye vita 'technically at war'.
Walisaini kitu kinaitwa 'Armistice Agreement' ambayo huruhusu mataifa kusitisha vita ili wazungumze, hivyo bado hawajatia saini 'Peace treaty'. Ina maana mnyukano unaweza kuibuka muda wowote hadi pale wataheshimiana na kuingia kwenye makubaliano ya amani.

Korea Kaskazini amewekeza sana kwenye kuelekeza mizinga na vifaa vyake vyote kutua mji mkuu wa Kusini, yaani kwamba vikibonyezwa, hata kama Marekani atafaulu kupangua kadhaa, lakini kuna mizinga mingi tu itatua Seoul na kusababisha vifo kwa mamilioni. Huwa sielewi kwanini Korea Kusini walijenga mji mkuu karibia na mpaka.

Siku zote mji mkuu unafaa kuwa katikati mwa nchi, ni kama tu hapo Bongo mumegoma kwenda Dodoma halafu mnategemea Dar ambayo ipo kwenye fukwe, siku mtaleta za kuleta kwa wazungu hapo nyambizi moja imetosha kuwatesa.
 
sansam100

JF-Expert Member
Oct 24, 2015
287
250
Adhabu yake huwa ni Kifo kwa wanafamilia ili wengine wajifunze na kutoa taarifa endapo wataona mwenendo Kama huyo kwa ndugu zao ili kujiokoa wasiuliwe iwapoa atatoroka
 
sansam100

JF-Expert Member
Oct 24, 2015
287
250
uongo mtupu. Hizo ni propaganda tu za nchi za magharibi
Dunia sikuhizi haendi kwa story Kama zako, google kuhusu North Korea defectors, utajua kuna mwingine miaka ya nyuma alitorokea japana na ndege ya Kivita, Mig ya mrusi ambazo zilikua advanced walizopewa na mrusi, Mi nadhani wewe sio mfutiliaji wa mambo au labda unaweza kuwa na language barrier Utashindwa kupata taarifa za ukweli mpaka uhadisiwe na mtu, Hali ya kiuchumi ya North Korea ni mbaya, pesa yote inaishia kwenye jeshi watu wanataabika wana TV station moja ya serikali hawana internet raia wa Kawaida, wanazuia uwezekano wowote watu wasiwe na taarifa ili wawe wamebaki wajinga. Ukiona marekani hamshambulii ulidhani kuwa anaogopa ili hofu ni kwa washirika wake ambao ni South Korea na Japan, kwa vile wako kwenye strike range ya north kwa hivyo kutakua na uhalibifu wa mali na maafa. Usipende stori za kwenye vijiwe sio vizuri kabisa kujazwa mawazo kutoka Kwenye midomo ya watu uwe unatafuta taarifa Mwenyewe
 
Dragoon

JF-Expert Member
Nov 24, 2013
7,037

wewe ndio unafuata story za kwenye vijiwe. yaani unasema google ndio chanzo cha habari? pole sana. Eti marekani haogopi kushambulia sababu ya washirika wake! tokea lini mmarikani akashindwa kupigana vita kisa kahofia taifa flani litadhulika? tokea lini mmarekani kapigana vita kashinda?
Nyie ndio aina ya watu dhaifu kabisa kwenye kufikiria. Mnalishwa mambo tu mnayameza kama yalivyo ndio maana unaamini hadi upuuzi.
hebu fuatilia news kupitia media za Urusi, Korea kaskazini na China ndio utajua dunia inavyokwenda. Sio kukaa tu unaangalia CNN na magazeti ya udaku.
 
amygdala

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
1,080

kusoma media za urusi na china peke yake ni kupotoka coz na wao wanaandika habari zenye interest na mataifa yao.....yaani ww uende kusoma sputnik ama interfax na russian insider habari ya marekan au ujeruman hutokuta positive hata moja hata usome miaka kumi...hizo russian today na zinginezo zilianzishwa mahususi kueneza ushwaish wa russia dubian kama zilivyo kina BBC so kama ww unasoma hizo basi utakua na mawazo ya upande mmoja kijana, soma za east na za west af bongo yako itachanganua
 
Kwa hiyo unataka niamini unachokiamini wewe? mimi nafuatilia media za aina mbalimbali, nachagua za kuziamini na zingine napuuzia na kuweka kapuni
 
Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
8,123
2,000
Mmh! Sio spy huyo. Ukute uduku kashatuma spy akawachunguze south korea
Kim mjanja sana, yaani hata ukijaribu kufikilia tukio hili limekaa kisanii kidogo, yaani muda huu Korea kasikasini na Kusini wako kwenye tension kubwa, Korea kasikazini kwa hivi sasa mipaka imewekewa ulinzi mkali si kwa kutumia Askali tu bali na DRONES ambazo wanazo nyingi tu na Patrol inafanywa 24X7, sasa huyu dogo ma miaka 20 anawezaje kuvaa boya ambalo kwa kawaida upakwa rangi maalum ili zionekane kirahisi hata ukiwa kwenye ndege unangalia chini mtu aliye vaa boya anaonekana ili kurahisisha uhokoaji kama inatokea ajali ya majini, unless kama dogo alitumia inner tube ya tairi ya gari - I might be wrong lakini mimi hayo ndiyo maoni yangu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom