Mwanajeshi mstaafu wa Marekani aliyeishi na VVU kwa miaka 20 bila kufahamu

Faith Luvanga

Member
Aug 21, 2018
14
15
Mwanajeshi wa majini wa Jeshi la Marekani amekuwa akiishi na Virusi vya Ukimwi kwa zaidi miongo miwili bila kujijua kutokana na kile anachodai kuwa wafanyakazi afya wa serikali hawakumpa majibu baada ya kumfanyia vipimo mnamo katikati ya mwaka 1995 ambapo wanajeshi wote wa jeshi la majini walipimwa virusi vya UKIMWI huko Colombia Kusini mwa Carolina.

Mwanajeshi huyo alifungua kesi mahakamani na kujitambulisha katika kesi hiyo kwa jina la John Doe ambalo si jina lake halisi ili kulinda faragha, amesema kuwa mnamo mwaka 1976 aliwahi kuumia wakati akihudumu majini ambapo anataja kuwa huenda ni moja ya sababu ya yeye kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Daktari wa kituo cha Afya cha Columbia aliamuru upimaji wa vipimo maabara uliojumuisha kipimo cha UKIMWI na kuwataka madaktari waliohusika kufanya vipimo hivyo kumpa majibu kila mwanajeshi aliempima, lakini John hakupewa majibu yake.

Mwanajeshi huyo amesema kuwa anajiona mwenye hatia kwa wanawake aliowahi kuwa nao kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa zaidi ya miaka 25 kwasababu alikua hafahamu kama anaishi na VVU.

Chad McGowan ambaye ni mwanasheria wake amesema kuwa kwa sasa anapatiwa huduma nzuri ingawa kwa miaka 25 alikua akipata matatizo ya kiafya mara kwa mara kutokana na kukosa huduma. Ameongeza kuwa baadhi ya athari alizopata ni pamoja na kuathirika kwa ubongo wake.

Takwimu zinaonesha kuwa maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kwa wanajeshi nchini Marekani mwaka 2008 yaliongezeka ndani ya miaka kumi iliyopita kufikia maambukizi 36 kwa kila kundi la wanajeshi 10,000 waliopimwa.

Jeshi la Marekani limesema kuwa linakadiria kutumia kiasi cha dola za kimarekani 14,000 hadi 37,000 kwa mwaka kwa ajili ya kuwahudumia wanajeshi walioathirika na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI, ambapo kwa mwaka 2008 walitumia dola milioni 7.8 hadi 20.7 kuhudumia wanajeshi 560 walioathirika.
 
25 yrs bila mbaazi
Kweli ukimwi hauwi bali kinachoua ni Presha na Arv
Wewe sema hivyo mkuu,kufa mapema baada ya kupata virusi itadepend na vitu vingi ikiwemo lishe,kinga yako ya mwili,lifestyle yako na matibabu yako unayopata kupambana na magonjwa nyemelezi.

Ukute jamaa alikuwa mtu wa mazoezi sana,ana lishe nzuri na kinga imara.
 
Back
Top Bottom