Mwanajeshi Arusha matatani kwa mauji ya Mkewe ,adaiwa kunyonga na kwenda kunywa bia

Mwanamke aitwaye ,Surajeni Tairo(30)ambaye ni mke wa mwanajeshi ,Alfred Maganga mkazi wa Muriet ,jijini Arusha,anadaiwa kufa katika ugomvi na mumewe na mwili wake kukutwa na majeraha kadhaa shingoni na kichwani huku mumewe akidai amejinyonga.


Utata huo umekuja pale ndugu wa marehemu walipouona mwili wa marehemu ukiwa majeraha hayo na kutilia shaka tukio hilo ambapo walidai kwamba ndugu yao hakujinyonga bali ameuliwa kikatili na Mwanajeshi hiyo


Akizungumzia tukio hilo kaka wa marehemu aitwaye Benedict Tairo mkazi wa Sanawari jijini hapa amedai kuwa siku ya tukio septemba 1,mwaka huu majira saa 11 jioni na alipigiwa simu na mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa ni mwanajeshi kuwa mdogo wake amejinyonga.

Baadhi ya majirani na marehemu jina( limehifadhiwa)wamedai kuwa siku ya tukio walisikia ugomvi kati ya marehemu na mwanajeshi huyo na kwenda kuamua na baadae waliondoka na kuwaacha wakiwa ndani wamejifungia.


Jirani huyo alisema kuwa baadae walimwona mwanajeshi huyo akitoka nje kuelekea dukani na wakati akirejea alikuwa ameshikilia chupa ya bia mkononi.


"Tukiwa nyumbani mwanajeshi huyo alikuja na kutuambia kuwa mke wake alikuwa amejinyonga na kama atakuwa amekufa nipatieni kisu na mimi nijiue"amesema jirahi huyo.


Kaka wa marehemu amesema kuwa Septemba 3,mwaka huu siku ya jumanne mwili huo wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi na daktari wa hospital ya mt.meru aitwaye Alex Mtei kwa kushirikiana na askari polisi na ndugu wa familia ,hata hivyo matokeo ya uchunguzi huo hayakufahamika.


Mapema leo katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mount Meru daktari bingwa aliyebobea katika masuala ya uchunguzi wa vifo vyenye utata ,dkt Alex Mremi kutoka hosptali ya rufaa ya kcmc alifika ili kuufanyia uchunguzi mwili huo lakini wanajeshi waliokuwa wamefurika katika chumba cha maiti walimjia juu na kulazimika kuondoka bila kuufanyia uchunguzi mwili huo





View attachment 1199113
Most of African solders are barbaric.
Au sijui kwa sababu ya levels zao za elimu huko
 
Lakini lazima tushauriane tu kiuanaume. Jamani ukiona mambo magumu muache tu asepe kwao ama sepa wewe. Kuna wanaume wanapiga wake zao utafikiri hao wanawake wameshuka toka angani. Sio vizuri kabisa. Vile mlivyokubaliana kukaa pamoja na vivyohivyo kubalianeni tu kutengana kwa muda.
 
Back
Top Bottom