Ndugu wana jambo Forum kwa kutambua mchango wa Jambo forum napenda kuomba msaada katika tatizo langu hili kwani ninaaminia Wanajambo forums.
MImi ni mtanzania niishie Uchinani kama mwanafunzi sasa kuna mwanajeshi mmoja ambaye mimi simfahamu ila ni mtu wa karibu wa familia ya rafiki yangu.Huyu jamaa alimuambia rafiki yangu kuwa sasa yeye kaamishiwa makao makuu ya jeshi kama muhasibu na kwa kuanzia, jeshi wameanza kutoa tenda kwa wafanyakazi wa jeshi ya kupeleka baadhi ya vifaa hapo vya electronics hapo jeshini(Makao Makuu) ili kuinua vipato vya wanajeshi.Mimi kwa Elimu yangu kidogo ya bishara ilinitinga kidogo lakini niliamini kwani Rafiki yangu alinithibitishia mno.
Sasa akamuambia yule rafiki yangu amsaidie kumuunganisha na mtu yeyote aliye Uchinani na yeye akafanya hivyo,kwakuwa rafiki yangu alimuamini mno huyu jamaa na pia alimuona mtu ambaye yupo stable basi akaniambia nimpelekee bidhaa bila ya malipo ya awali mpaka hapo atapopokea mali na kulipwa toka jeshini ndio atanipatia pesa ikiwa pamoja na faida ujumla ilikuwa ni Milioni nne ya kitanzania kwani nilimpelekea USB 80 tena zile first quality kwani kwa sisi tulio huku ndio tunajua kipi ni feki na kipi ni mali kwani USB zinazopelekwa USA si sawa na zile zinazopelekwa Tanzania ila mimi niliamua kununu kiwango cha juu kwakuwa zinaenda kutumika sehemu nyeti mno na kwakuwa hii ndio fani yangu so ninajua kwa undani kwenye hayo masuala.
Mimi nimtumia kama kawaida tena nilitumia njia ghali mno kutuma kwakuwa jamaa alikuwa anasema zinahitajika kwa haraka mno, kwakuwa nilimuamini rafiki yangu mno ambaye tulikuwa wote shule ya msingi na kuendelea kuonana hadi siku za usoni kabla ya kuja China. HUyu jamaa baada ya kupokea hii mizigo akaanza longolongo kila siku nikiulizia naambiwa mara cheki bado mara mkuu wa majeshi kabadilishwa na kila siku safari haziishi.
NIkawasiliana na Mama yangu ili anisaidie kufuatilia kwani nilihisi huyu rafiki yangu ananichezea,mama akafanikiwa kuonana na huyu rafiki yangu na kumuihoji na kumpa mikakati yake na ndio huyu jamaa akatoa pesa kama shilingi laki nane na nusu..Na akaahidi kuendelea punde.Kwa bahati mbaya kipindi kufuatilio kunaendelea mama yangu akafariki dunia so kuniacha nikihang kwani Naweza kusema ingawa nina Baba lakini ni Jina tu tangu miaka hiyo ya 86. Huyu jamaa kwa sasa imefikia kipindi hataki hata kukutana na yule rafiki yangu akienda nyumbani kwake anaongopewa hayupo na kazini ni kama munavyofahamu mambo ya wanajeshi..
Sasa siku hizi haongei kitu na simu amebadilisha..na mimi kusema kweli kwa maisha ya Uchinani kama mwanafunzi pesa ni ngumu mno kama mujuavyo kwani hawa jamaa kila kitu kinamilikiwa na sirikali yao so kunanifanya niishi maisha magumu mno.
Tatizo ambalo naona nililifanya ni kuwa hakukuwa na written document kati yangu na huyu jamaa kwani mimi nilikuwa naongea na rafiki yangu sasa hii inanipa utata ni nini cha kufanya so ninaomba msaada wenu.kufuatilia yafuatayo
1.Je huyu jamaa ni kweli yupo huko makao makuu kwani nimepata fununu kuwa bado yupo Kisarawe Coast Region kama accountants.jina lake kamili ni
Osward Peter kazi ni Accountant kikosi ambacho nimesikia yupo ni T 191 kj.
2.Je ni nini natakiwa kufanya katika mlengo wa sheria..
Natumaini nitapata ufumbuzi wa tatizo.
Tafuta wakili aku represent. Ninachofanya mimi nakubaliana nae kiasi gani. Nampa kazi alafu nasahau. Kesi ikiisha unamalizia kiasi kilichobaki. Wakili anaweza kukugharimu kama $600 hivi tu. Na atafanya kila kitu kuanzia kwenda kufungua kesi polisi bongo, kumfuatilia mtuhumiwa na kuhakikisha kuwa ni kweli na kusimama nae mahakamani siku ya kesi. Kwa ujuzi wangu mimi jamaa atakubali kulipa kidogo kidogo. Wakili ataakikisha mahakama ni shahidi na hela zinakusanywa kwa amri ya mahakama.