'Mwanajeshi' aliyepiga picha na Lema afungwa jela miaka minne

Mkuu huyo siyo mwanajeshi ni muhuni tu wa Chadema ambaye alivalishwa na Lema sare za Jeshi nakupiga naye picha kulichafua jeshi letu kujiingiza kwenye siasa.

Sidhani kama hilo la Lema kumvisha magwanda linawezekana ila ni uzembe wa Jeshi lenyewe kwani vijana wa JKT huwa wanavaa hayo magwanda na kulindia usiku kwenye ulinzi shirikishi mbona.
 
Tena Kosa la ziada la Yule Askari likikuwa kushiriki siasa ,kugombea uchaguzi,na kutumia jina la mtu au kufoji( kihiyo) Huko akijuwa yote hayo ni uvunjaji wa Sheria ,na pia uvunjaji wa taratibu za ajira za jeshi na utumishi wa umma.
 
Ritz; Nakuona kama unacheka vile............. zomba; Rejao; thatha; hebu chekeni kwa pamoja tuwaone............!


Ritz; Umesema CDM imemsababishia kijana wa watu kifungo??????
Kwa kweli unanichekesha tumia akili wewe mtumwa feki,,,,haya mambo ya familia na watoto kwenda shule ni mambo ya kawaida na utaona mwenyewe na utashaangaa na magamba wako.

Wakuu wangu Mingoi, chama, binafsi yangu sijamuelewa huyu kamanda labda mje mumjibu nyie.
 
Last edited by a moderator:
Cheap popularity ndo athari zake.Kwani angevaa kawaida asingeshabikia Chadema mpaka akavae nguo za watu wakati sio zake
 
Mambo ya ajabu kabisa sasa wanamkomoa nani.......

Hakomolewi mtu bali wanajenga nidhamu katika jeshi na kuonyesha katika jamii ni jinsi gani ilivyo vigumu kuyavaa hayo magwanda kwa sababu kufanya hivyo lazima uwe umepitia ukuruta (kukimbia bila kutembea from A-B) na umepigishwa kwata la nguvu.
 
Sidhani kama hilo la Lema kumvisha magwanda linawezekana ila ni uzembe wa Jeshi lenyewe kwani vijana wa JKT huwa wanavaa hayo magwanda na kulindia usiku kwenye ulinzi shirikishi mbona.

Mkuu huyo muhuni kavaa sare za jeshi letu wamepanga na Lema pamoja na Nassari wamepiga picha pamoja halafu unasema ni uzembe wa jeshi lenyewe.
 
Miaka minne mbona kidogo sana alitakiwa afungwe miaka 10 ili liwe fundisho kwa watu wenye akili kama za kwake unapiga picha genge la maandamano unatemea nini tena ukiwa na sale za jeshi letu tukufu!
 
Mimi naomba kuuliza hii kesi ilisikilizwa kwenye mahakama gani na je ilisikilzwa na kutolewa hukumu siku hiyo hiyo.Je kesi zote mwaka huu zitasikilizwa na kutolewa hukumu mara moja kama hii.
 
Sidhani kama hilo la Lema
kumvisha magwanda linawezekana ila ni uzembe wa Jeshi lenyewe kwani
vijana wa JKT huwa wanavaa hayo magwanda na kulindia usiku kwenye ulinzi
shirikishi mbona.
JKT tangu lini wakavaa magwanda ya mawingu? huwa naona wanavaa full green
 
Vipi na wale waliomuua mwangosi?shimbo nae vipi?Wacha aende jela lakini 2015 atakuwa shujaa na wapo wengi wanajeshi wanaoona haya mateso,ipo siku watasema inatosha.Poor CCM
 
Mkuu huyo muhuni kavaa sare za jeshi letu wamepanga na Lema pamoja na Nassari wamepiiga picha pamoja halafu unasema ni uzembe wa serikali.

Their PR stunts backfire na sasa wao wameisha ingia mitini wakati yeye ananyea ndoo. Huu ndiyo utamu wa siasa za matukio. Hit and Run.
 
Kwa hiyo utaki kukubali kuwa mwanajeshi wa Chadema kaenda jela miaka minne.

kwenu ccm kila kitu kinawezekana, mradi mna interest nacho. nyie wafungeni, waueni, wateseni watu mnavyopenda, ila jueni kuwa iko siku mtajibu hayo yote. msije tu mkasahau mliyoyafanya. hata kama huyo mwanajeshi katuhumiwa, ni kwa haki au ni kwa sababu amepiga picha na lema? mjue vilio vyovyote vinavyotolewa na raia kwa ajili yenu, hayo machozi na masononeko ya watu msifikiri yatapita bure.
 
wanajeshi wangapi wanapiga picha na wabunge wa ccm hawafungwi kama sio uonevu nin?i

tatizo ni kwamba huyu wa kwenu hakuwai hata kupitia mafunzo ya mgambo.mlimvalisha tu magwanda ya jeshi letu for political reasons,ndio kinachomcost,alidanganywa na wanasiasa uchwara afanye siasa uchwara in the name of jwtz ili ionekane eti kuna kauasi flani jeshini
 
Mkuu huyo siyo mwanajeshi ni muhuni tu wa Chadema ambaye alivalishwa na Lema sare za Jeshi nakupiga naye picha kulichafua jeshi letu kujiingiza kwenye siasa.

Labda sijaelewa sawasawa, kumbe alikuwa mhuni tu na si mwanajeshi?...
 
Mimi naomba kuuliza hii kesi ilisikilizwa kwenye mahakama gani na je ilisikilzwa na kutolewa hukumu siku hiyo hiyo.Je kesi zote mwaka huu zitasikilizwa na kutolewa hukumu mara moja kama hii.

Mkuu
katika kesi, ukisomewa mashitaka na ukayakubali. Kinachofuatia ni hukumu tu.

Nafikili hicho kimetokea kwa huyo jamaa. I'm sorry for him. Aliingizwa mkenge na wajanja.
 
Ramadhani ighodu wa usalama wa Taifa amehukumiwa miaka mingapi? Msitufanye wajinga subirini tu kiama chenu kinakuja! Nosense
 
Mkuu kulichafua Jeshi letu ni ujinga?

Mkuu Ritz za asubuhi na tumai umeamka salama
Mkuu tunaomba pia kesi za kina Dk Ulimboka na Mwangosi mzishuurikie haraka kama hii mlivyofanya na pia familia ya mwangosi muipe huduma inazostahili
 
Last edited by a moderator:
Mnaosema jeshi lenu ninyi ni kina nani? Nani halipi kodi kwa ajili ya JWTZ? Acheni upuuzi wa kuchekelea uonevu na udhalimu.Kupiga picha na kiongozi wa upinzani ni miaka minne then mnatumia siasa kuona hilo ni sahihi kweli? Wanajeshi wangapi wamepiga picha na viongozi wa CCM? Hakika mnaochekelea upumbavu huu iko siku mtawajibika kwani sidhani hata kama angekuwa amekiuka kanuni then,adhabu ya miaka 4 inaendana na uzito wa kosa.
 
Back
Top Bottom