Mwanaharakati na aliyekuwa mke wa hayati Nelson Mandela, Winnie Mandela afariki dunia

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,001
112,646
Mwanaharakati na mke wa zamani wa Rais wa kwanza mwafrika wa Afrika Kusini(hayati Nelson Mandela), Bi. Winnie Mandela amefariki leo Jumatatu mchana akiwa na umri wa miaka 81 jijini Johannesburg.

Mpinga Ubaguzi wa Rangi Winnie Madikizela-Mandela (81) alizaliwa tarehe 26, Septemba mwaka 1936.

Msaidizi wake, Zodwa Zwane amethibitisha taarifa hizo.

winnie.jpg


winnie na mandela.jpg

Mwanaharakati wa kupigania haki za watu weusi na mke wa zamani wa aliyekuwa rais wa Afrika Kusini, Winnie Madikizela-Mandela amefariki dunia nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa ya familia iliyochapishwa na Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini, SABC, Bi Madikizela-Mandela amefariki kutokana na matatizo ya kiafya ya muda mrefu.

Bi Winnie Madikizela-Mandela aliyeendelea kuwa mwanachama wa chama tawala cha ANC hadi mauti yanamfika alifanikiwa kuhudhuria ibada ya sikukuu ya Pasaka siku ya Ijumaa kabla ya hali ya afya yake kubadilika na kukimbizwa hospitali ya Netcare Milpark kwa matibabu ambapo mchana wa Jumatatu alitangazwa kufariki dunia.

Hali ya kiafya ya Bi Madikizela-Mandela inatajwa kuzorota kwenye miaka ya hivi karibuni huku akilazimika kufanyiwa upasuaji mara kadhaa kutokana na maradhi ya kisukari.

Wakati wa uhai wake, Bi Madikizela-Mandela licha ya kuwa mke wa zamani wa rais wa kwanza wa Afrika Kusini aliyechaguliwa baada ya kukomeshwa kwa ubaguzi wa rangi, Nelson Mandela, pia aliwahi kushika nyadhifa kadhaa serikalini na aliwahi kuwa kiongozi wa Umoja wa Wanawake wa chama cha ANC.

Bi Madikizela-Mandela atakumbukwa kwa kuwa mmoja wa wanawake waliokuwa mstari wa mbele kwenye mapambano ya ukombozi wa Afrika Kusini hususani vita dhidi ya ubaguzi wa rangi ambayo mara kadhaa ilimpelekea kusweka ndani.

Bi Madikizela-Mandela alikuwa akiitwa kwa jina la heshima la ‘Mama wa Taifa’ kutokana na mchango wake kwa ukombozi wa nchi hiyo.

Bi Madikizela-Mandela na Mzee Nelson Mandela walitengana mwaka 1992 na mwaka 1994 wawili hao waliachana huku talaka yao ikikamilika mwaka 1996.
 
Kumbe miaka inakimbia asee..
Huyu juzi juzi tu hapa alikuwa mwanadada matata sana leo hii ana miaka 81......!!?

Rip
 
Kumbe miaka inakimbia asee..
Huyu juzi juzi tu hapa alikuwa mwanadada matata sana leo hii ana miaka 81......!!?

Rip
 
Kumbe miaka inakimbia asee..
Huyu juzi juzi tu hapa alikuwa mwanadada matata sana leo hii ana miaka 81......!!?

Rip
 
Winnie Madikizela-Mandela (amezaliwa tar. 26-09-1936 na jina la Nomzamo Winifred Zanyiwe Madikizela ) ni mwanasiasa wa Afrika Kusini, ambaye ameshikilia nafasi kadhaa serikalini na alikuwa mkuu wa ligi ya wanawake ANC.
Wakati huu yeye ni mwanachama wa kamati ya kimataifa ya ANC.

Ingawa bado alikuwa mke wa Nelson Mandela wakati Mandela alipewa urais wa Afrika ya Kusini mnamo Mei 1994, kamwe hakuwa first lady wa Afrika ya Kusini, kwani wanandoa hawa walikuwa wametengana miaka miwili iliyopita.

Hii ilikuwa baada ya Winnie kugunduliwa kuwa na uhusiano wa kimapemzi na watu wengine baada ya kuachiliwa kwa Nelson kutoka gerezani mnamo Februari 1990.

Talaka ya mwisho ilipitishwa mnamo tarehe 19 Machi 1996.

Kama mwanaharakati mwenye utata, yeye ni maarufu miongoni mwa wafuasi wake ambao humwita 'Mama wa Taifa'.
Lakini si wote wanaompenda kwani wengine humtusi, hasa kutokana na madai kadhaa ya uhusika wake katika ukiukaji wa haki za binadamu, iliyohusisha mateso na mauaji ya mtoto wa umri wa miaka 14 aliyekuwa anaitwa Stompie Moeketsi mwaka wa 1989.

Alazwe anapostahili.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom