waziri2020
Senior Member
- May 31, 2019
- 190
- 451
Mwanaharakati na mtetezi wa haki za wanawake nchini Joyce Kiria "the Super woman" amtembelea mwalimu aliyekatwa mkono na mume wake kwa madai ya wivu wa mapenzi .
Akiongea katika hospitali ya Selian iliyopo Ngaramtoni wilayani Arumeru, mwanaharakati huyo amesema kuwa amesikitishwa na tukio la mwanamke huyo kukatwa mkono kinyama kikatili na mume wake wa ndoa akidai mke wake sio mwaminifu katika ndoa.
Kiria akiwa katika wodi aliyolazwa mwalimu Veronica Daudi amewaasa wanawake kuacha kuvumilia vitendo vya unyanyasaji ambavyo wamekuwa wakifanyiwa na waume zao na badala yake kutoka taarifa kwa vyombo vya dola.
Amesema wanawake wengi wamekua wakikosa haki kwa kuvumilia vipigo na manyanyaso ndani ya ndoa wakiofia kutengana na familia zao jambo linalo leta madhara makubwa kwa kuchukuliana sheria mkononi.
Joyce ni miongoni mwa wanawake wanaharakati waliojitolea kusaidia wanawake kupata haki hasa kupitia kipindi cha wanawake live kinacho zungumzia manyanyaso na ukatili dhidi ya wanawake katika jamii.
Akizungumza mwalimu Veronica Daudi ameshukuru Joyce Kiria kufika wodini hapo alipo lazwa kumpa faraja na kumsaidia mchango wa kuanza kupata mkono wa bandia na baadae kurejea kazini kwakwe kufundisha wanafunzi kama mwanzo
Amesema kilicho pelekea yeye kukatwa mkono wake na mumewe ni wivu wa mapenzi, baada ya mume wake kumlalamikia Mara kwa Mara juu ya kuwa na mausiano na wanaume wengine jambo ambalo si la kweli
Mwalimu Veronica anafundisha katika shule ya sekondari ilkidiga iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha akifundisha masomo ya kiingereza
Amesema mpaka sasa ajui hatma ya maisha yake ya ualimu kwani ndio ajira anayo tegemea kwani katika familia yake wamezaliwa watoto saba na yeye ndio aliye bahatika kupata elimu huku wadogo zake wakimtegemea yeye baada ya wazazi wake kufarikia dunia na kubaki yatima