Mwanaharakati Joyce Kiria amtembelea Mwalimu aliyekatwa mkono na mume wake kwa madai ya wivu wa Mapenzi

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Mwanaharakati na mtetezi wa haki za wanawake nchini Joyce Kiria "the Super woman" amtembelea mwalimu aliyekatwa mkono na mume wake kwa madai ya wivu wa mapenzi .

Akiongea katika hospitali ya Selian iliyopo Ngaramtoni wilayani Arumeru, mwanaharakati huyo amesema kuwa amesikitishwa na tukio la mwanamke huyo kukatwa mkono kinyama kikatili na mume wake wa ndoa akidai mke wake sio mwaminifu katika ndoa.

Kiria akiwa katika wodi aliyolazwa mwalimu Veronica Daudi amewaasa wanawake kuacha kuvumilia vitendo vya unyanyasaji ambavyo wamekuwa wakifanyiwa na waume zao na badala yake kutoka taarifa kwa vyombo vya dola.

Amesema wanawake wengi wamekua wakikosa haki kwa kuvumilia vipigo na manyanyaso ndani ya ndoa wakiofia kutengana na familia zao jambo linalo leta madhara makubwa kwa kuchukuliana sheria mkononi.

Joyce ni miongoni mwa wanawake wanaharakati waliojitolea kusaidia wanawake kupata haki hasa kupitia kipindi cha wanawake live kinacho zungumzia manyanyaso na ukatili dhidi ya wanawake katika jamii.

Akizungumza mwalimu Veronica Daudi ameshukuru Joyce Kiria kufika wodini hapo alipo lazwa kumpa faraja na kumsaidia mchango wa kuanza kupata mkono wa bandia na baadae kurejea kazini kwakwe kufundisha wanafunzi kama mwanzo

Amesema kilicho pelekea yeye kukatwa mkono wake na mumewe ni wivu wa mapenzi, baada ya mume wake kumlalamikia Mara kwa Mara juu ya kuwa na mausiano na wanaume wengine jambo ambalo si la kweli

Mwalimu Veronica anafundisha katika shule ya sekondari ilkidiga iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha akifundisha masomo ya kiingereza

Amesema mpaka sasa ajui hatma ya maisha yake ya ualimu kwani ndio ajira anayo tegemea kwani katika familia yake wamezaliwa watoto saba na yeye ndio aliye bahatika kupata elimu huku wadogo zake wakimtegemea yeye baada ya wazazi wake kufarikia dunia na kubaki yatima
IMG_20201004_134620_4.jpg
IMG_20201004_131337_0.jpg
IMG_20201004_131000_3.jpg
 
Mwanaharakati na mtetezi wa haki za wanawake nchini Joyce Kiria "the Super woman" amtembelea mwalimu aliyekatwa mkono na mume wake kwa madai ya wivu wa mapenzi .

Akiongea katika hospitali ya Selian iliyopo Ngaramtoni wilayani Arumeru, mwanaharakati huyo amesema kuwa amesikitishwa na tukio la mwanamke huyo kukatwa mkono kinyama kikatili na mume wake wa ndoa akidai mke wake sio mwaminifu katika ndoa.

Kiria akiwa katika wodi aliyolazwa mwalimu Veronica Daudi amewaasa wanawake kuacha kuvumilia vitendo vya unyanyasaji ambavyo wamekuwa wakifanyiwa na waume zao na badala yake kutoka taarifa kwa vyombo vya dola.

Amesema wanawake wengi wamekua wakikosa haki kwa kuvumilia vipigo na manyanyaso ndani ya ndoa wakiofia kutengana na familia zao jambo linalo leta madhara makubwa kwa kuchukuliana sheria mkononi.

Joyce ni miongoni mwa wanawake wanaharakati waliojitolea kusaidia wanawake kupata haki hasa kupitia kipindi cha wanawake live kinacho zungumzia manyanyaso na ukatili dhidi ya wanawake katika jamii.

Akizungumza mwalimu Veronica Daudi ameshukuru Joyce Kiria kufika wodini hapo alipo lazwa kumpa faraja na kumsaidia mchango wa kuanza kupata mkono wa bandia na baadae kurejea kazini kwakwe kufundisha wanafunzi kama mwanzo

Amesema kilicho pelekea yeye kukatwa mkono wake na mumewe ni wivu wa mapenzi, baada ya mume wake kumlalamikia Mara kwa Mara juu ya kuwa na mausiano na wanaume wengine jambo ambalo si la kweli

Mwalimu Veronica anafundisha katika shule ya sekondari ilkidiga iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha akifundisha masomo ya kiingereza

Amesema mpaka sasa ajui hatma ya maisha yake ya ualimu kwani ndio ajira anayo tegemea kwani katika familia yake wamezaliwa watoto saba na yeye ndio aliye bahatika kupata elimu huku wadogo zake wakimtegemea yeye baada ya wazazi wake kufarikia dunia na kubaki yatimaView attachment 1590297View attachment 1590298View attachment 1590299
Huyu nae ni njaa tu,wapo wanawake kibao wenye matatizo,yeye hapa anatumia majanga ya watu kujipatia Umaarufu,Hana Cha maana anachokifsnya,je amemlipia gharama za hospitari?au ameenda kufata mahojiano ili youtube yake ipate viewers wengi?Yule Dada aliyeuliwa Kimara,ndugu zake kawapa msaada gani,kesi imeisha?au aliwatumia kujipatia Kiki.
 
Lakini Ticha kwa nini uchepuke wakati unajua mme wako hayuko vizuri kichwani hasa akiwa amepiga mambo zake kichwani(bange & kijiti)
 
Huyu nae ni njaa tu,wapo wanawake kibao wenye matatizo,yeye hapa anatumia majanga ya watu kujipatia Umaarufu,Hana Cha maana anachokifsnya,je amemlipia gharama za hospitari?au ameenda kufata mahojiano ili youtube yake ipate viewers wengi?Yule Dada aliyeuliwa Kimara,ndugu zake kawapa msaada gani,kesi imeisha?au aliwatumia kujipatia Kiki.
Nia ya Joyce ni kupaza sauti kupinga ukatili. Hajawahi kusema anatoa msaada wa pesa au kusimamia kesi mahakamani hadi iishe, mbona harakati zake zinaeleweka?
 
Huyo mbwa joyce hana msaada wowote zaidi ya kutafuta umaarufu
Ijapokua umemuita jina baya la mnyama ambayo sio sawa..ila nadhani ananufaika zaidi yeye kwa kujitangaza au kupata misaada kwa namna au jina la aina hiyo ya ukatiri.
 
Back
Top Bottom