Mwanaharakati atoa soma kwa serikali sheria ya uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanaharakati atoa soma kwa serikali sheria ya uchaguzi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Jatropha, Sep 4, 2010.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Nilikikuta kipindi cha Kipima Joto kikiwa ukingoni lakini Mchambuzi aliyekaribishwa alinikosha sana pale alipodai kuwa kama angeshirikishwa katika utungwaji wa Sherioa ya Gharama za Uchaguzi angetoa ushauri wa bure kuhusu namna ya kumaliza tatizo la Rushwa za Uchaguzi hapa Tanzania.

  Kilichonisikitisha ni kuwa licha ya fedha nyingi sana kutumika katika utugwaji wa sheria hii, bado imeshindwa kukidhi haja na kupendelea wagombea kutoka CCM.

  Matatizo ya Rushwa katika chaguzi zetu yatapungua au kuisha kabisa pale Serikali ya CCM itakapoacha kutoa rushwa kwa viongozi wanaochaguliwa na wananchi kwa minajili ya kuisimamia Serikali k.m wabunge na madiwani. Rushwa hiyo hutolewa kwa njia ya mishahara na marupurupu makubwa tofauti na wavuja jasho wa taifa hili.


  Rushwa hizi kubwa huwafanya maelfu ya wataalamu wa fani mbali mbali, wakiwemo madakatari, wahandisi n.k kukimbilia siasa na kuacha kuwahudumia wananchi na kujenga taifa kutokana na siasa kuofanywa kuwa inalipa zaidi.

  Katika kuthibitisha kuwa siasa inalipa zaidi hapa nchini hata wafanyabisahara nao wapo tayari kuacha biashara na kujiingiza kwenye siasa.


  Baada ya kuwalevya kwa rushwa hizi,wawakilishi wa wananchi hao hushindwa kutimiza matakwa ya vifungu 63 na 64 vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vinavyotamka kuwa wajibu wa Mbunge au Diwani ni "Kuisimamia na Kuishauri Serikali".

  Ni kutokana na CCM kuwapatia wawakilishi wa wananchi rushwa, hushindwa kusimamia utendaji wa Serikali ya CCM na watendaji wake na hivyo hupelekea kubweteka kwao na kutotoa huduma nzuri kwa wananchi. Aidha vitendo vya ubadhirifu na wizi wa mali ya umma hushamiri na utajiri wote wa Tanzania ikiwemo Bandari 3, Mito, maziwa na Bahari, Madini ya aina mbalimbali, vivutio vya watalii n.k navyo hukosa usimamizi na kuifanya Tanzania kuwa moja ya nchi maskini sana duniani licha ya kuwa ni moja ya nchi zenye utajiri mkubwa sana katika Afrika na Dunia.
   
Loading...