MwanaHalisi yamshambulia Sitta

kamatembo

JF-Expert Member
Sep 25, 2011
854
1,000
[Kibarua katika serikali ya JK, Kanyea kambi, APRIN kwa mamilioni, Nyumba ya spika Urambo duu? Mitambo ya mtumba then symbion, huyo aliyenyunyiza huo unga ni Mwakyembe, sitta: hapana, ni Manyanya, Sitta: hapana, ni Chenge Sitta: hahahahaha!, maboza ya maji yanalipwa na bunge kwenda kwa dada mmoja pale kinondoni, mimi ni mtumishi na Mage ni mtumishi lazima kila mmoja apate nyumba ya kununua ya serikali na bado ile ya mjengoni hataki kuhama, hayo ni machache tu niliyokutana nayo kwenye nuuz mbalimbali.
My take: Ningekuwa Rais huyu asingekuwa waziri wangu, ningekuwa mwanaurambo huyu asingekuwa mbunge wangu. Huyu ndo anatakiwa alipe hela ya Dowans, Tanesco walisema jamani tununue hii mitambo, Zito akapiga debe jamani tununue, Idrisa akataka kuachia ngazi Sitta akakomaa, wenye mamlaka wakamuogopa leo anasema hatulipi, kivipi? Wa TZ tusiwe mambumbu badala ya kujifanya wajuaji na kale kakampuni kanaitwa REX Attorneys kanaendelea kulipwa mabilioni kwa kukata rufaa bado interest ya deni inaongezeka kila siku, ilikuwa kama Bil 94, leo tuko 111 bil, mpaka tunalipa inaweza kuwa imefika 130 bil. Tumeuingia mkenge na wapiga debe kina Sitta bado wanatupoteza, wanaotaka kuandamana waelekee kwa sitta. Ngeleja nenda kwa Al-Azawi yule jamaa atakusikiliza tumpoze kidogo watu wakafanye kazi, hizi siasa zenu mkapige majimboni kwenu kazi za kitaalam muwaachie wenyewe.[]

wapambe bana eti sitta alipe yeye DOWANS..vp kwanini asilipe Lowassa au na ww ndio upo kwenye pay roll ya kapeni EL 4 2015?manaake naona unavyoshupalia mmasai na mkwele walipwe tu..sijui masaburi yakuwasha sijui au funza kichwani.IWEJE RICHMOND HARAMU IKAZAE DOWANS HALALI?
 

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,250
Nimewasoma wote watatu - anayejiita Mtanzania Huru, Mojo na Ngao One. Nawafahamu. Ninachosikitika ni kwamba hamumfahamu Kubenea. Huyu jamaa ni chuma cha pua. Si kweli kwamba Kubenea analipiwa safari zake za India na serikali ya Rais Jakaya Kikwete. Hili naweza kulithibitisha . Muache kucahfaua watu kwa hisia.

Kuhusu Kubenea kufadhiriwa na Mengi na sasa urafiki wa Mengi na Kubenea umekufa, na kwamba wakati wowote anaweza kumuandika Mengi, nadhani ninyi hamumfahamu vizuri huyu kamanda. Kubenea hana rafiki na yeyote ambaye anatia ulimi puani. Nani asiyejua kwamba Mengi anamtetea Kikwete, kwamba hahusiki na ufisadi wakati huohuo anasema nchi imejaa mafisadi?

Inawezekana kweli kwamba Kubenea haheshimiki na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari hapa nchini. Lakini kwangui mimi kutoheshimika kwake kunatokana na husda waliyonayo baadhi ya watu kwa kumuona Kubenea amepiga hatua kubwa ya kumiliki gazeti lake yeye mwenyewe.

Kuhusu hili la kumwagiwa tindikari kwa kuwa alikuwa na mke wa mtu, hizo ni poropaganda za wale waliotumwa kumdhuru. Tunawajua hata kwa majina.
We ndio humjui Said kweli kweli na kama anakutumia basi anakutumia vibaya, Kubenea unaweza kumtenganisha na Mengi wakati kila siku anashinda kwa Mengi na hata hizo safari za kwenda kutibu hilo jicho lake ni nani anaemfadhili amekwambia?

Kwa taarifa yako yeye anamwita Mengi eti ni babake!!! Njaa hii acha tu, mchagga na mmafia wapi na wapi..? Sasa kamuulize kwanini anamwita Mengi babake? Akikujibu urudi tena hapa na pia ukikupa nafasi muulize WAR CHEST ya dola milioni 500 ya kumsafishia njia LOWASSA imeshatumika kiasi gani na imebaki kiasi gani? Halafu pia akueleze kwanini huwa hamsemi vibaya Membe? Ana ajenda gani na Membe?

Hapo ndio utajua unafiki wa Kubenea, ila namsifu kwa elimu yake ya darasa la saba lakini anavyowaruga wasomi wa CCM kina Lowassa, Membe, JK, Rostam akimng'ata huyu na kumpuliza yule mpaka raha. Vipi ile issue aliyoianzisha huko ya kumtuhumu mama Shelukindo kuhamia kambi ya Lowassa baada ya kuambiwa na TB Joshua siku hizi mbona haisemi tena, unahisi nini kimetokea?
 

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,250
Is this what you guys mean by "Kubenea kanunuliwa? Tafakari! Rostam Aziz anacheza kama Pele | Gazeti la MwanaHalisi

Mkurupukaji mwingine huyu, mzee unamjua huyo Nyaronyo Kicheere alieandika hiyo habari ya ROSTAM anacheza kama Pele? Au umekurupuka tu!

Kwa taarifa yako huyo sio kubenea,huyo ni mwandishi wa habari nguli ambae kwa muda mrefu amekua kwenye vyombo vya habari vya mengi akiwahi pia kuwa mwanasheria wa mengi na katika uchaguzi uliopita aligombea ubunge wa tarime nadhani kwa tiketi ya NCCR sikumbuki sawasawa kwa taarifa za nyongeza amewahi kujaribu kusomea upadri sitaki kuingia sana ndani hapa, ila tu hiyo story hajaandika Kubenea na hawezi tena kuandika hivyo.

Kubenea katiwa mfukoni wadau sisi ni marafiki tunamjua anatujua na wala hatukukutana nae barabarani kama anavopenda kusema mkubwa mmoja hapa nchini, Saidi awadanganye nyinyi msiomjua, mimi sitaki kuwaita misukule ila maamuma. Hata kama anapenda, Said hawezi na hana ubavu tena wa kuwaandika vibaya mabwana zake wapya Lowassa na Rostam.

Tatizo watu wakimpenda mtu hata uwaeleze nini huwa hawaelewi mpaka yawakute mfano mzuri ni Zitto Kabwe alipoanza kutoka nje ya mstari, kuna watu tulikua wa mwanzo mwanzo kumshtukia tuliposema hapa tulizomewa ile mbaya lakini baadae alipokuja kutoa makucha ndio watu wakaanza kushtuka too late zitto harekebishiki tena tunaishia kumbembeleza tu cha kumfanya hatuna, ndio huyu kubenea wenu sasa mtamjua vizuri tu huko mbele
 

Kikarara78

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
1,496
2,000
WanaMabadiliko, JF
Siku zote wasema Mficha Maradhi, Ugonjwa humuumbua, mimi naamini Sitta alikuwa anajua ukweli wa mambo na alikuwa kwenye nafasi nzuri sana ya kurekebisha Uchafu na Uozo wa Ufisadi kwa nafasi yake kama Spika au Kiongozi wa Juu Serikalini. Tatizo moja kubwa ambalo linampata sasa alikubali kupozwa na tamaa ya kujengewa ofisi ya Bunge, Ubunge Urambo na ahadi za kitoto. Wakati ule alikuwa ana choice 2 moja kutoka na kukaa kando au kusema ukweli wa mambo.
Ukipanda mchicha utavuna Mchicha, sasa atavuna apandacho. Wanasema ukila nyama ya binadamu siku zote utataka na kula nyama ya binadamu, Aseme Ukweli na Ukweli utamweka HURU !!!!
 

Kikarara78

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
1,496
2,000
WanaMabadiliko,

Siku zote wasema Mficha Maradhi, Ugonjwa humuumbua, mimi naamini Sitta alikuwa anajua ukweli wa mambo na alikuwa kwenye nafasi nzuri sana ya kurekebisha Uchafu na Uozo wa Ufisadi kwa nafasi yake kama Spika au Kiongozi wa Juu Serikalini. Tatizo moja kubwa ambalo linampata sasa alikubali kupozwa na tamaa ya kujengewa ofisi ya Bunge, Ubunge Urambo na ahadi za kitoto. Wakati ule alikuwa ana choice 2 moja kutoka na kukaa kando au kusema ukweli wa mambo.

Ukipanda mchicha utavuna Mchicha, sasa atavuna apandacho. Wanasema ukila nyama ya binadamu siku zote utataka na kula nyama ya binadamu, Aseme Ukweli na Ukweli utamweka HURU !!!!
 

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
0
EDWARD Lowassa, waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, "amemtia kidole jichoni" Rais Jakaya Kikwete.
Ijumaa iliyopita, aliishambulia serikali kwa kushindwa kufanya maamuzi mazito, yakiwamo yale yanayohusu maslahi ya taifa.
Alisema, "…hivi sasa kuna ugonjwa umezuka nchini kwa viongozi wa serikali kushindwa kutoa maamuzi magumu. Ni bora ukubali kuhukumiwa kwa kutoa maamuzi magumu, kuliko kuogopa kuyatoa."
Akizungumza kwa mara ya kwanza bungeni tangu alipojiuzulu wadhifa wa waziri mkuu, Februari 2008, Lowassa alisema, "Hakuna jambo baya kama ugonjwa wa kuogopa kutoa maamuzi magumu."
Lowassa alikuwa akichangia, bungeni Dodoma, hotuba ya bajeti ya ofisi ya waziri mkuu kwa mwaka wa fedha 2011/2012.
Tayari baadhi ya wachambuzi wa mambo ya siasa nchini wamesema, kauli ya Lowassa itakuwa imetokana na "kufahamu udhaifu wa kiongozi mkuu wa nchi."
Rais Kikwete amekuwa akilaumiwa na viongozi wastaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali, viongozi wa vyama vya upinzani, asasi za kijamii na watu binafsi, kwa kutochukua hatua mwafaka pale zinapohitajika.
Haijafahamika iwapo Lowassa amejitathmini vya kutosha kabla ya kudandia hoja hiyo, ambayo pia iliwahi kushikiwa bango na Kongamano la Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) miaka miwili iliyopita.
Bali kuna orodha ya matukio yanayomhusu hata Lowassa ambayo Kikwete hakuyatolea maamuzi – mepesi au magumu.
Kwa mfano, Lowassa alijiuzulu kutokana na shinikizo la bunge baada ya kukamilisha uchunguzi kuwa ama alishiriki au aliwezesha au alishinikiza kutolewa kwa mkataba wa kufua umeme kwa kampuni ya Richmond Development Corporation.
Ilibainika Richmond haikuwa na fedha, utaalam wala uzoefu katika uzalishaji umeme na kwa hiyo ilibebwa. Lowassa alijiuzulu. Hakustaafu.
Lakini Rais Kikwete ameshindwa kufanya maamuzi, mepesi au mazito; kumwambia Lowassa kuwa hakustaafu na hivyo hastahili marupurupu yoyote ya waziri mkuu aliyestaafu.
Bali Lowassa, akihutubia bunge, alisema, "Hakuna jambo baya kama ugonjwa wa kuogopa kutoa maamuzi magumu."
Rais Kikwete ameshindwa kuwachukulia hatua watendaji wa serikali, akiwamo Lowassa wakati huo, kwa kuidhinisha mkataba tata wa Richmond na Dowans Holdings SA ya Costa Rica na Dowans Tanzania Limited (DHL).
Makampuni hayo ambayo yalikuwa vigumu kujua makazi ya ofisi zao na maofisa wake wanaowasiliana na serikali, yanawakilishwa nchini na mfanyabiashara na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ambaye amekiri mara kadhaa kufahamu wamiliki wake.
Licha ya rais kushindwa kufanya maamuzi, kama mitambo itumike au isitumike; lakini baya zaidi ameshindwa kununua mitambo mipya, hata kwa mkopo; na ameshindwa kuwabana, kuwawajibisha na hata kuwaadabisha waliohusika na maafa ya giza kwa taifa.
Rais ameshindwa kuchukua maamuzi – mepesi au mazito – kuhusu Lowassa. Hata baada ya jina lake kutajwa miongoni mwa watu watatu wanaotuhumiwa "kuchafua" chama kwa tuhuma za ufisadi zinazowakabili, Rais Kikwete ameshindwa kuchukua hatua.
Wengine wanaotuhumiwa na CCM kwa "kuichafua" ni Rostam na mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge. Majina yao yalitajwa na makamu mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa mbele ya Halmashauri Kuu ya chama hicho mjini Dodoma.
Rais Kikwete ameshindwa kuchukua hatua ya kuwafukuza kutoka kwenye chama au hata kuwapa barua za onyo. Kutochukua hatua kumefuatia maapizo ya viongozi wenzao kuwa "lazima mafisadi watoswe."
Rais Kikwete anatuhumiwa pia kushindwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa wizi wa fedha za umma kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Taifa (BoT).
Fedha hizo zilizoibwa katika kipindi kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, inadaiwa kuwa sehemu yake kubwa ilitumika kuwaingiza madarakani; yeye na wenzake.
Badala ya kuwasweka watuhumiwa mahakamani, Rais Kikwete aliwaingiza katika mkataba usio wa haki wa kukiri kuiba na kurejesha sehemu ya walichoiba ili wasifikishwe mahakamani.
Alishindwa ujasiri wa kutaja wezi hadharani; akawaonea huruma kwa kuwapa upendeleo unaovunja Katiba ya nchi. Alishitaki hawa na kuacha wale.
Rais Kikwete analaumiwa kwa kutochukua hatua kwa waliokwapua zaidi ya Sh. 40 bilioni kutoka BoT kwa jina la Kagoda Agriculture Limited. Miongoni mwa wanaotajwa kuwa na mkono katika mkakati wa kukwapua kiasi hicho ni Rostam ambaye Kikwete amekiri kuwa ni mmoja wa maswahiba wake.
Hata watu wawili wanaotajwa kuwa waanzilishi wa Kagoda, ingawa hali zao za maisha kwa sasa hazionyeshi kuwa waliwahi kushika hata Sh. 500,000 kwa wakati mmoja, hawajafikishwa mahakamani.
Hakuna ushahidi kwamba wakili wa kujitegemea wa jijini Dar es Salaam, Bhyidinka Michael Sanze, ambaye alinukuliwa na gazeti hili, katika andishi maalum kwa Kamati ya Rais kuhusu wizi wa Kagoda, aliishawahi kutumiwa kukama wezi.
Wote ambao wakili alitaja, akiwemo Rostam, ambaye anadai alimwita ofisini mwake, Na. 50 Mirambo jijini Dar es Salaam, ambako alishuhudia hati za Kagoda za kuiba fedha, hawajawahi kukamatwa.
Katika hili la Kagoda, Rais Kikwete hajawahi kuchukua uamuzi mzito au hata mwepesi katika kurejesha fedha za umma.
Hata baada ya Yusuf Manji kukiri kuwa anajua Kagoda; kwamba aliwalipia deni lao serikalini na kwamba anawadai, serikali ya Rais Kikwete haijachukua hata uamuzi mwepesi wa kukabiliana na Manji ili kupata fununu juu ya Kagoda.
Lakini ni Kamati ya rais ya kuchunguzi wizi iliyoamua kiasi gani Kagoda walipe iwapo hawataki kupelekwa mahakamani. Hivyo Rais Kikwete anajua Kagoda ni nani, alichukua kiasi gani na walimtaka alipe kiasi gani.
Katika hili, rais amebaki amenyamaza kama mlinzi mkuu wa mafisadi hao, badala ya kuwa tishio kwao. Ameshindwa kuchukua maamuzi; hata mepesi.
Aidha, Rais Kikwete ameshindwa kufanyia kazi tuhuma zinazoikabili kampuni ya Deep Green Finance Ltd., ambayo ilikwapua Sh. 8 bilioni kutoka BoT. Kampuni ya mawakili ya IMMA Advocates and Co. ya Dar es Salaam ndiyo ilisadia usajili wa Deep Green na ndiyo iliyowafilisi (!)
Deep Green Finance Limited ilichota fedha hizo kati ya Septemba na Desemba 2005 wakati wa mchakato kuelekea uchaguzi mkuu wa 2005.
Rais ameshindwa kuchukua maamuzi kuhusu tuhuma za ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi kutoka Hazina na BoT. Makampuni hayo ni pamoja na Tangold Limited na Meremeta.
Kampuni ya Meremeta pekee ilichota zaidi ya Sh. 155 bilioni kutoka BoT. Kwa miaka mitano sasa, serikali imekuwa ikijibaraguza kwa kusema Meremeta ni kampuni ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) iliyokuwa na kazi ya kuchimba dhahabu katika mgodi wa Buhemba, mkoani Mara.
Hata hivyo, MwanaHALISI lilithibitishia ulimwengu, kwamba kampuni hiyo ilianzishwa kwa kazi ya ununuzi na uchimbaji dhahabu nchini; iliandikishwa nchini Uingereza mwaka 1997 na baadaye kufilisiwa nchini humo mwaka 2006.
Katika hatua ya kujinasua, waziri mkuu Mizengo Pinda aliwahi kusema Meremeta ni mali ya serikali kwa asilimia 100, jambo ambalo halikuwa sahihi. Mali za Meremeta, kwa mujibu wa katiba yake, zinaweza kurithiwa na wazazi, ndugu na wengine kama binamu. Iko wapi serikali yenye baba, watoto, binamu na wajukuu?
Mpaka sasa, serikali ya Kikwete imeshindwa kuifanyia kazi au kuitoa hadharani ripoti ya wakaguzi waliokagua BoT, Juni 2006. Taarifa zinasema ndani ya ripoti hiyo ndimo sakata la Meremeta liliibuliwa.
Kwa yote haya, Rais Kikwete alikaa kimya na anaendelea kukaa kimya. Ngao yake kuu imekuwa kukaa kimya na bila kuchukua hatua yoyote – ngumu au nyepesi.
Kuna hili la gavana wa BoT Daudi Balali. Pamoja na kwamba wakati anaondoka nchini kwa kile kilichoitwa "kwenda kutibiwa Marekani," kashfa nyingi za ufisadi zilikuwa zimeibuliwa, serikali ya Kikwete ilimnyang'anya ugavana peke yake, bila hata kumshitati akiwa hayupo.
Juu ya hilo, serikali haikutoa maelezo ya wazi kabisa kuhusu ilichoita "kifo cha Balali nchini Marekani." Ukungu uliotanda juu ya kimya cha Balali ulihitaji kauli ya rais. Hakusema. Hakuchukua hatua ya kuondoa wananchi gizani.
Hata waandishi wa habari walipotaka kujua aliko Balali, wakati fulani waliambiwa na ofisi ya mkurugenzi wa mawasiliano ikulu kwamba "Serikali ina mkono mrefu. Balali akihitajika ataletwa…" Hakuletwa na haijulikani kama bado serikali ina uwezo wa kumleta.
Uuzaji holela wa mgodi wa mkaa wa mawe Kiwira na uuzaji wa nyumba za serikali ambazo Kikwete aliapa kuzirejesha, ni miongoni mwa mambo ambayo rais ameshindwa kufanyia maamuzi.
Rais Kikwete ameshindwa kushughulikia wizi uliofanywa katika ununuzi wa rada ya kijeshi. Rais anafahamu watuhumiwa, lakini amekataa kuwapeleka mahakamani.
Hata baada ya msaada wa Uingereza, hadi mbunge machachari mwanamke Clare Short kujiuzulu akipinga uuzaji rada hiyo kwa "nchi masikini" na kwa bei iliyopitiliza, bado serikali ya Kikwete ilikaa kimya.
Leo ndio serikali inajikakamua kupinga masharti ya kurejeshewa fedha zilizokuwa zimeibwa na kampuni ya BAE. Lakini haijaonyesha kuwajibika kwa kuchunguza, kukamata na kupeleka mahakamani wale wote waliokula mlungula katika ununuzi huo.
Miongoni mwa yaliyotajwa ambayo Rais Kikwete ameshindwa kuchukulia maamuzi mepesi au mazito, kuna ambayo yalitendeka Lowassa akiwa waziri au waziri mkuu.
Hili ndilo linafanya wachunguzi wa mambo ya kisasa wajiulize zaidi juu ya hatua ya Lowassa kumtia kidole jichoni. Ameamua kuingia "siasa za kuumbuana" au anatafuta upenyo wa kurejea kileleni kwa kutamka yale ambayo yaweza kumpa umashuhuri?
Kusema ni jambo moja. Kuaminika ni jambo jingine. Lakini ni siku sita tangu Lowassa ajiunge na wale ambao wamekuwa wakisema Kikwete na serikali yake wanashindwa kuchukua uamuzi mgumu juu ya masuala muhimu ya kitaifa.
Bado taifa halijasikia sauti ya Rais Kikwete kupinga au kukubaliana na tuhuma dhidi yake. Inawezekana hata kwa hili atashindwa kuchukua uamuzi mgumu au mwepesi wa kujibu tuhuma dhidi yake binafsi na serikali yake?
 

Mojo

Senior Member
Apr 27, 2011
153
225
Mkurupukaji mungine huyu,mzee unamjua huyo Nyaronyo Kicheere alieandika hiyo habari ya ROSTAM anacheza kama Pele???au umekurupuka tu!kwa taarifa yako huyo sio kubenea,huyo ni mwandishi wa habari nguli ambae kwa muda mrefu amekua kwenye vyombo vya habari vya mengi akiwahi pia kuwa mwanasheria wa mengi na katika uchaguzi uliopita aligombea ubunge wa tarime nadhani kwa tiketi ya nccr sikumbuki sawasawa kwa taarifa za nyongeza amewahi kujaribu kusomea upadri sitaki kuingia sana ndani hapa,ila tu hiyo story hajaandika kubenea na hawezi tena kuandika hivyo,kubenea katiwa mfukoni wadau sisi ni marafiki tunamjua anatujua na wala hatukukutana nae barabarani kama anavopenda kusema mkubwa mmoja hapa nchini,saidi awadanganye nyinyi msiomjua,mimi sitaki kuwaita misukule ila maamuma.Hata kama anapenda said hawezi na hana ubavu tena wa kuwaandika vibaya mabwana zake wapya Lowassa na Rostam,tatizo hapa jf watu wakimpenda mtu hata uwaeleze nini huwa hawaelewi mpaka yawakute mfano mzuri ni zitto kabwe alipoanza kutoka nje ya mstari,kuna watu tulikua wa mwanzo mwanzo kumshtukia tuliposema hapa tulizomewa ile mbaya lakini baadae alipokuja kutoa makucha ndio watu wakaanza kushtuka too late zitto harekebishiki tena tunaishia kumbembeleza tu cha kumfanya hatuna,ndio huyu kubenea wenu sasa mtamjua vizuri tu huko mbele

Watanzania wengine wanakuwa kama mbuzi, daima wanafuata mchungaji na hawana akili huru ya kufikiri wao wenyewe. Unaona mbuzi wakitoka kwenye banda lao kwenda kula majani, ukiweka kizingiti mlangoni mbuzi wa kwanza ataruka atoke, ukitoa kile kizingiti mbuzi wanaofuata wote wataendelea kuruka bila kuangalia kama kizingiti kimeshatolewa. Hivyo ndio jinsi the so-called Great Thinkers wa JF walivyoaminishwa kuwa Kubenea ni shujaa na anachukia ufisadi, basi wanaendelea kuamini hivyo tu bila kutumia akili za kawaida na kubaini huyu mtu kashanunuliwa na mabwana wapya siku hizi nao ni Rostam Aziz, Edward Lowassa na Andrew Chenge. Hana ubavu tena wa kuwaandika vibaya mabwana zake wapya.

Njaa mbaya, Kubenea kaolewa na mafisadi sasa!
 

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
0
Hata kama aliyeandika stori ya Rostam anacheza kama pele, siyo Kubenea, lakini gazeti la MwanaHALISI ni la Kubenea. Anayepitisha hizo makala na sdtori, ni Kubenea. Anayelipa waandishi wanaoandika ni yeye. Sasa nami nimeitafuta stori hii imeandikwa na Kubenea mwenyewe, Juni mwaka huu. Soma kisha wewe na Sitta wakp mthibitishe kwamba huyu jamaa amenunuliwa. Tatizo lenu mnataka kila kukicha amuandike Lowassa hata kama hajafanya jambo lolote.

Endelea Kubenea kafanye kazi ya kukomboa taifa achana na makuwadi wa Sitta, Nape na Mwakyembe.
 

MWANIKO

Member
Oct 3, 2011
23
20
sitta yupo juu ya kubenea ktk hii nchi kwa utendaji wa wazi na kuaminika kwa umma,hivyo mwanaHALISI jihadharini kwa kuanza kuonekana mmenunuliwa na mafisadi.Pia siku si nyingi,Gazeti lenu litaporomoka umaarufu ktk soko la Tanzania.
 

Marytina

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,365
2,000
Sitta pamoja na matatizo yake chungu nzima, lakini pale anaposimama kutetea maslahi ya nchi kwa mfano kupinga malipo fisadi ya sh 113 billioni kwa Dowans basi Watanzania wote tunabidi tumuunge mkono pamoja na kujua kwamba Sitta si safi. Kumbukeni umoja ni nguvu ni utengano ni udhaifu. Sijamsikia hata siku moja Kikwete, Pinda, Pinda au Lowassa wakisimama hadharani na kumuita Sitta ni mnafiki maana hawana ubavu wa kufanya hivyo ila wameamua kuwatumia vibaraka vyao kumshambulia Sitta ambaye ameamua kusimama kidete katika kuipinga Dowans.
Nachelea kusema huna akili timamu
Ikiwa SITTA ndiye aliyeuzima mjadala wa Dowans BUNGENI leo tumwamini vipi anapopinga malipo ya Dowans???
Ni SITTA aliyeunga POSHO bungeni kwa kuwaita wanaozikaa ni wanafiki-Ikiwa SITTA ana huruma na wanainchi kwa nini asingeunga mkono hoja ya kukataliwa POSHO ili bili 900 ziingie kwenye kusaidia jamii???
SITTA ni mnafiki sana
 

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,250
Hata kama aliyeandika stori ya Rostam anacheza kama pele, siyo Kubenea, lakini gazeti la MwanaHALISI ni la Kubenea. Anayepitisha hizo makala na sdtori, ni Kubenea. Anayelipa waandishi wanaoandika ni yeye. Sasa nami nimeitafuta stori hii imeandikwa na Kubenea mwenyewe, Juni mwaka huu. Soma kisha wewe na Sitta wakp mthibitishe kwamba huyu jamaa amenunuliwa. Tatizo lenu mnataka kila kukicha amuandike Lowassa hata kama hajafanya jambo lolote.

Endelea Kubenea kafanye kazi ya kukomboa taifa achana na makuwadi wa Sitta, Nape na Mwakyembe.

Labda wewe ndio kuwadi wa LOWASSA na genge lake,sie tupo hapa kuwaeleza ukweli wa nyuma ya pazia kumhusu huyu rafiki yetu said kubenea,kwa kuwa tunamjua anatujua na tumekua nae kwenye shida na raha hata alipomwagiwa tindikali alizodai kumwagiwa na hwa marafiki zake wapya ni sisi ndio tuliomsaidia,hiyo story ya june unayosema tuisome iko wapi sasa??mbona hukuiweka!Mwanahalisi tunapozungumzia limepoteza muelekeo tunaagalia heading father,siku zote msimamo wa gazeti uko kwenye heading sio makala za ndani ambazo huandikwa hata na waandishi wa nje ya gazeti husika,angeiweka mbele hiyo stori ya mzee nyaronyo tuone,mbona aliificha ndani...na tunapozungumzia mwanahalisi pengine mimi niwe wazi nazungumzia stori za kubenea ambazo ndio mara nyingi kama sio zote hukaa mbele na yeye huweka jina lake kwa kuwa anadai yeye huwa haandiki habari za maruhani a.k.a.na mwandishi wetu,hivyo kwa said tuliemjua huko nyuma ilikua hivi hata wewe kama mtu wa serikalini ukawa na kigongo unataka kuigonga serikali lakini unaogopa kupoteza kazi ikijulikana unampelekea said then yeye anachofanya ni kuweka jina lake na kukulinda wewe kama source ya habri kwa kutokutaja hata iweje,hiyo ndio kitu iliyompatia heshima saidi miongoni mwa watendaji waserikali wakajenga kumuamini sana na kumpelekea stori ambazo ndio pia zikakufanya wewe pia umjue...Lakini pia haimaanishi waandishi wote pale mwanahalisi wanakubaliana nae,kuna watu pale bado ni wazalendo wa kweli kama mzee NDIMARA ambae ndio kidogo haka kaheshima heshima kalikobaki ka mwanahalisi ni kwa ajili yake na bahati nzuri saidi hawezi kumpangia wala kumuingilia yule mzee,kwani yeye na saidi ni sawasawa na mlima kilimanjaro na kichuguu,hiyo ndio inayopelekea angalau watu kama kina Nyaronyo waweze kupeleka stori pale na zikachapishwa kama zilivyo japo sio mbele,mbele pale ni kwa ajili ya ROSTAM NA LOWASSA kuandikiwa wanachokitaka..habari ndio hiyo,mwenye kununa anune mwenye kucheka acheke!
 

DOUBLE AGENT

Member
Jul 3, 2011
37
0
Kubenea amepata mabwana wapya siku hizi, nao ni mafisadi papa wa Tanzania -- Edward Ngoyai Lowassa na Rostam Aziz. Watu wote wajanja wanajua hilo na muda si mrefu Watanzania wote watajua hilo. MwanaHalisi litakuwa kama Rai sasa hivi. Litaporomoka na kuwa kama toilet paper kwani Watanzania kamwe hawawezi kusoma gazeti la kifisadi. SAMUEL SITTA ni mpambanaji halisi, Watanzania wanamwamini na kumuhitaji aendelee na vita hii
 

trachomatis

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
3,752
2,000
Nachelea kusema huna akili timamu
Ikiwa SITTA ndiye aliyeuzima mjadala wa Dowans BUNGENI leo tumwamini vipi anapopinga malipo ya Dowans???
Ni SITTA aliyeunga POSHO bungeni kwa kuwaita wanaozikaa ni wanafiki-Ikiwa SITTA ana huruma na wanainchi kwa nini asingeunga mkono hoja ya kukataliwa POSHO ili bili 900 ziingie kwenye kusaidia jamii???
SITTA ni mnafiki sana
Nimezipenda hizo data na jinsi ulivyozitumia kuwakilisha ujumbe wako.
 

trachomatis

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
3,752
2,000
Nachelea kusema huna akili timamu
Ikiwa SITTA ndiye aliyeuzima mjadala wa Dowans BUNGENI leo tumwamini vipi anapopinga malipo ya Dowans???
Ni SITTA aliyeunga POSHO bungeni kwa kuwaita wanaozikaa ni wanafiki-Ikiwa SITTA ana huruma na wanainchi kwa nini asingeunga mkono hoja ya kukataliwa POSHO ili bili 900 ziingie kwenye kusaidia jamii???
SITTA ni mnafiki sana
Nimezipenda hizo data na jinsi ulivyozitumia kuwakilisha ujumbe wako.
 
Apr 20, 2011
27
0
Kubenea si mtu professional, hata hiyo editorial yake kaandika kidaku na kuonesha chuki na visasi dhidi ya Samuel Sitta ambaye ni kipenzi cha Watanzania wengi. Kubenea anasema Sitta ni "kibarua" kwenye serikali ya Kikwete. Huu ni utoto na kutojua sheria, Sitta ni waziri kwa mujibu wa katiba ya nchi kama mawaziri wengine wa serikali na ni mmoja wa viongozi wakubwa na wanaoheshimika sana Tanzania na nje ya nchi.

Kwa wasiomjua Kubenea, huyu mtu hajaenda shule kabisa na ana uwezo mdogo sana wa akili licha ya watu wengi kutojua hili na kumuona kama shujaa. Siyo siri kama Kubenea sasa anatumikia mabwana wake mafisadi na amenunuliwa. Kudhihirisha kuwa Kubenea ana matatizo ya akili ataanza kuandika makala za kumshambulia Sitta kuanzia sasa kuhusu tuhuma za uongo za ufisadi na CCJ.

Sitta ataendelea kuheshimika daima kama viongozi shupavu Tanzania!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom