Mwanahalisi yaanika hoja zilizotikisa Ikulu na CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanahalisi yaanika hoja zilizotikisa Ikulu na CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Dec 8, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  RAIS Jakaya Kikwete hakufahamu kwa undani kilichomo kwenye muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba (Constitutional Review Bill 2011), uliopitishwa na bunge hivi karibuni, MwanaHALISI limeelezwa. Taarifa kutoka serikalini zinasema Rais Kikwete alipata undani wa muswada huo pale alipokutana na ujumbe wa viongozi wa ngazi ya juu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  Rais Kikwete alikutana, Jumapili na juzi Jumatatu, ikulu Dar es Salaam na ujumbe wa CHADEMA, ambao imeelezwa kuwa ndio ulimfafanulia rais undani wa mapungufu makubwa katika muswada huo.Taarifa zinasema, mara baada ya Rais Kikwete kusikikiliza zaidi ya hoja 15 zilizopangiliwa kwa ustadi mkubwa na CHADEMA, alisikika akisema, "Nimewaelewa. Mnazo hoja, tena za msingi." Mtoa taarifa amelieleza gazeti hili kuwa baada ya kikao cha pande zote mbili, Rais Kikwete "ameonyesha kukubali" kufanyia marekebisho makubwa katika muswada uliopitishwa na bunge hivi karibuni.

  Imefahamika kuwa hoja ya kuacha kutia saini muswada ilishindikana kupatiwa ufumbuzi baada ya Rais Kikwete kueleza hatari inayomkabili mbele ya chama chake iwapo ataacha kusaini muswada ili uwe sheria. Rais amenukuliwa akisema, "Hata mimi naona mnazo hoja za msingi, lakini nikigoma kutia saini, wenzangu kwenye chama hawatanielewa."Hata hivyo, mtoa taarifa anasema Rais Kikwete amekubali ombi la CHADEMA la kutafuta ushauri mpana zaidi kutoka kwa watu wengine mbalimbali juu ya umuhimu wa yeye kutosaini sheria hiyo kwa sasa.

  Taarifa zinasema Kikwete alikuwa makini kusilikiza kila hoja ambayo CHADEMA walikuwa wanaieleza na kuitolea ufafanuzi. Kuna wakati alisema, "Kama hoja ni hii, mbona imeshindikana bungeni?" zimeeleza taarifa.Ujumbe wa CHADEMA uliokwenda kuonana na Rais Kikwete uliongozwa na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, makamu wenyeviti Bara, Saidi Arfi na Zanzibar, Said Issa Mohamed na mjumbe wa Kamati Kuu (CC) na mshauri wa siasa wa chama hicho, Profesa Mwesiga Baregu. Wengine walikuwa mwanasheria wa chama hicho, Profesa Abdallah Safari, mbunge wa Ubungo, John Mnyika, mkurugenzi wa masuala ya bunge na halmashauri ya chama hicho, John Mrema na mwanasheria mwingine wa chama hicho, Tundu Lissu ambaye ni katibu wa kamati hiyo. MwanaHALISI limeelezwa na mtoa taarifa kuwa, kauli ya Kikwete ilitokana na uchambuzi wa kina wa hoja uliofanywa na Lissu hasa katika eneo linalohusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, adhabu zilizowekwa kwa watakaokiuka sheria na jinsi ya kupata Bunge Maalum la Katiba.

  Akiongea kwa kuelekeza macho kwa baadhi ya wasaidizi waliokuwa kwenye mkutano huo, Rais Kikwete alihoji, "Kitu gani kimetokea kabla ya kwenda bungeni mpaka ikashindikana?"Rais Kikwete alitaka kufahamu kilichotokea, hadi CHADEMA wakaamua kususia muswaada huo bungeni. Akijibu swali hilo Lissu alisema mambo mengi yametokea. Alisema kwanza, spika alikuwa anawaburuza na hakutaka kuwasikiliza tangu mwanzo. Alisema siku zote alikuwa anasikiliza serikali, badala ya kufanya kazi za bunge.

  Lissu alimweleza rais kuwa walimwambia spika kuwa muswada huo ulipelekwa bungeni kwa hati ya dharula, 9 Aprili 2011 na ukakataliwa; bunge liliagiza serikali itoe muda zaidi na iandae muswada huu kwa lugha ya Kiswahili ili wananchi wengi waweze kuusoma.Alisema baada ya kazi hiyo kukamilika, muswada ulipaswa kuchapishwa kwenye gazeti la serikali na kutangazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ili kutoa fursa kwa wananchi wengi kuuelewa.

  Lissu amenukuliwa akimwambia rais, "Hata hivyo, hakuna hata moja ya maagizo haya ya bunge ambalo lilitekelezwa. Kamati ya Sheria na Katiba haikukaa kuujadili muswada huu tena kati ya tarehe 15 Aprili na 24 Oktoba 2011 wakati muswada ulipoletwa kwenye Kamati ukiwa umefanyiwa marekebisho makubwa."Alisema tafsiri ya kiswahili ya muswada wa Aprili ililetwa bungeni, 5 Novemba 2011, siku tatu kabla ya bunge kuanza mkutano wake wa Tano. Kwa maana hiyo, Lissu alisema muswada wa sheria uliotolewa maoni na wadau kabla ya 24 Oktoba 2011, ulikuwa ule wa Aprili.

  Alisema wananchi hawakupatiwa fursa ya kutoa maoni yao juu ya muswada ulioletwa bungeni. Muswada uliopitishwa ulitolewa kwa kamati, tarehe 24 Oktoba 2011 na kugawiwa kwa wabunge wote tarehe 5 Novemba 2011.Hoja nyingine ambayo CHADEMA walimueleza Kikwete, ni kuhusu ubatili wa wabunge wa sasa wa Muungano katika Bunge Maalum la Katiba. Kwa mujibu wa muswada uliopitishwa, wabunge wa sasa wa bunge la Muungano, ni sehemu ya bunge la katiba. Hili si sahihi, alisema Lissu kama alivyonukuliwa na mtoa taarifa.

  Amesema, "Wabunge wa Bunge la Muungano na Baraza la Wawakilishi Zanzibar waliopo sasa, hawana uhalali kikatiba wa kutunga katiba mpya, kwani wote walichaguliwa kwa mujibu wa katiba ya sasa na wamekula kiapo cha kuilinda, kuihifadhi na kuitetea; na siyo kuiua."Mambo mengine ambayo yameripotiwa kujadiliwa kati ya rais na ujumbe wa CHADEMA ni Muungano. Katika hili, uongozi wa kamati ulimweleza rais kuwa hawapingi Muungano uliopo.

  Kamati ilisema kwa hali ya sasa, Muungano ni kama haupo kutokana na hatua ya serikali ya Zanzibar kubadilisha katiba yake ambayo imefuta mambo karibu yote yaliyokubaliwa kwenye mkataba wa Muungano wa mwaka 1964.Mtoa taarifa amesema, awali akiwasilisha mapendekezo ya CHADEMA, Lissu alimwomba Rais Kikwete kusaidia taifa lake kupata katiba mpya wakati taifa likiwa moja na wananchi wote wakiwa wameshikamana.

  Amenukuliwa akisema, "Mheshimiwa Rais, tusaidie kupata katiba mpya ya nchi tukiwa tumeshikamana. Tusitafute katiba mpya wakati tumefarakana. Wala tusipate katiba wakati wengine wako gerezani, wengine wanasubiri kufungwa na wengine tumeumia," alisisitiza."Muswada uliopitishwa na bunge na ambao wewe unatakiwa kuusaini, umepiga marufuku kufanyika kwa mikutano ya kuhamisisha wananchi kushiriki kwenye mchakato wa katiba na umetoa adhabu ya kifungo cha hadi miaka mitano au faini ya Sh. 15 milioni," alinukuliwa Lissu akiwasilisha kwa rais.Hoja nyingine za CHADEMA katika kabrasha walilomkabidhi rais, zinahusu uhalali wa kisiasa wa hoja ya kupatikana Bunge Maalum la Katiba; vigezo muhimu na wingi wa kura za kila chama katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

  Limo pia suala la mgawanyo wa wajumbe kwenye Bunge Maalum la Katiba ambako CHADEMA, chenye wabunge wengi, kina idadi ndogo ya wajumbe kuliko Chama cha Wananchi (CUF) chenye wabunge wachache, kwa mujibu wa muswada uliopitishwa. Mengine katika kabrasha la CHADEMA lililoko mikononi mwa Rais Kikwete ni muswada wa sheria uliopitishwa kuwa na masharti yanayokiuka misingi na matakwa ya wananchi walio wengi.

  Aidha, CHADEMA wamewasilisha kuwa Bunge Maalum la Katiba linaloundwa na muswada uliopitishwa linaendeleza hodhi ya CCM ya mchakato wa katiba mpya kwa kuipa zaidi ya nusu ya wajumbe wa bunge hilo.Jingine ni kuhusu Katiba ya Jamhuri kutamka kwamba, "Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano," wakati katiba ya sasa ya Zanzibar inatamka, "Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  "Maeneo mengine ya makabrasha ya CHADEMA yanahusu migongano kati ya katiba ya Tanzania na ile ya Zanzibar na sehemu kadhaa ambako sheria za kawaida zinaondoa kile ambacho tayari kimewekwa na sheria mama – Katiba. Unatolewa mfano wa mgongano ambapo katiba ya Muungano inasema, "Rais wa Jamhuri atakuwa mkuu wa nchi, kiongozi wa serikali na Amiri Jeshi Mkuu," wakati katiba ya Zanzibar ya sasa inasema, "Kutakuwa na rais wa Zanzibar ambaye atakuwa mkuu wa nchi ya Zanzibar... Rais wa Zanzibar atakuwa kamanda mkuu wa idara maalum."Katika makabrasha ya CHADEMA kwa rais yamo pia masuala ya ulinzi na usalama; mengine yakigusa migongano, hasa katika kuanzisha majeshi upande wa serikali ya Muungano na ule Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
   
 2. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  walikuwa wanamchanganya tu, wala hakuelewa!
   
 3. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Jamaa anajua bila ku sign chama chao kingeshuka thamani,kwani ingeonekana wabunge wake ni majuha
   
 4. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  lakini kwa kusaini mbona hata yeye amekuwa ****
   
 5. K

  KIROJO Senior Member

  #5
  Dec 8, 2011
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mpaka sasa hakuna anayeelewa katiba ni nini?ila kinachoendelea ni mizaha tu kwenye mambo ya muhimu kwa maisha ya yeye ambaye tupo madarakani akifikiria yeye ndo kabisa anahusika kutunga katiba,natakaye kuja ndo anajua mimi ndo nitafaidi hawa wakiondoka.Kweli watu wa kijijini ndo kabisaa! hata wanashangaa ,maana kama mpira hivi.
  Time will tell!
   
 6. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #6
  Dec 8, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  '' kwa kweli mnahoja nzuri lkn nisipo'sign wenzangu si watanishangaa'' jk
   
 7. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #7
  Dec 8, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Washauri wa rais wote vilaza akina Wassira, hapo unategemea nini?
   
 8. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #8
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Habari ndefu sana inaboa hata kusoma
   
 9. H

  HAKI bin AMANI Senior Member

  #9
  Dec 8, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Enzi ya Mwalimu
  Enzi ya mwalimu JKN akiwa Rais wa JMT aliwahi kusema; "Mimi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nikiwa ama bara ama visiwani" Ni kweli alikuwa anajitambua. Kwa wakati huo rais wa Zanzibar kama wanavyopenda aitwe, alitambulika kama RAIS WA SERIKALI LA MAPINDUZI ZANZIBAR na siyo rais wa nchi ya Z'bar. Ukweli ni kwamba si lazima neno RAIS awe mtawala wa nchi. Wapo marais wa vyama vya wafanyakazi, marais wa vyama vya michezo nk. Yupo Rais wa Mamlaka ya Palestina lakini si rais wa nchi.
  Tofauti na enzi ya Mwalimu, hivi leo tunashuhudia protokali ambayo tunashindwa kuelewa imetoholewa kutoka wapi.

  Tumeshuhudia katika sherehe za mapinduzi Zanzibar Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihudhuria sherehe kama mwalikwa wa kawaida ndani ya Jamhuri yake. Tumeshuhudia Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar akikagua majeshi ya Ulinzi na Usalama, huku mwenye majeshi hayo yaani Amiri Jeshi Mkuu akiwa amekaa kwenye benchi.

  Mambo haya yameanza kutendeka polepole na baadaye kukomaa, na kwa vile yanapofanyika hakuna wa kukemea, wenzetu wa Z'bar wametumia mwanya huo kufanya walivyofanya. Watu wana macho lakini wamejifanya vipofu, wana masikio lakini wamejifanya viziwi na wana midomo lakini wamejifanya bubu. Kuficha bomu kwenye kitanda unacholalia kila siku haina tofauti na mhanga anayejifungia mabomu ili ajilipue kwa makusudi.
   
 10. H

  HAKI bin AMANI Senior Member

  #10
  Dec 8, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [FONT=&amp]Enzi ya Mwalimu[/FONT]
  [FONT=&amp]Enzi ya mwalimu JKN akiwa Rais wa JMT aliwahi kusema; "Mimi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nikiwa ama bara ama visiwani" Ni kweli alikuwa anajitambua. Kwa wakati huo rais wa Zanzibar kama wanavyopenda aitwe, alitambulika kama RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR na siyo rais wa nchi ya Z'bar. Ukweli ni kwamba si lazima neno RAIS awe mtawala wa nchi. Wapo marais wa vyama vya wafanyakazi, marais wa vyama vya michezo nk. Yupo Rais wa Mamlaka ya Palestina lakini hana nchi.[/FONT]

  [FONT=&amp]Tofauti na enzi ya Mwalimu, hivi leo tunashuhudia protokali ambayo tunashindwa kuelewa imetoholewa kutoka wapi.

  Tumeshuhudia katika sherehe za mapinduzi Zanzibar Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihudhuria sherehe kama mwalikwa/mtazamaji wa kawaida ndani ya Jamhuri yake. [/FONT]


  [FONT=&amp]Tumeshuhudia Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar akikagua majeshi ya Ulinzi na Usalama, huku mwenye majeshi hayo yaani Amiri Jeshi Mkuu akiwa amekaa kwenye benchi.

  Mambo haya yameanza kutendeka polepole na baadaye kukomaa, na kwa vile yanapofanyika hakuna wa kukemea, wenzetu wa Z'bar wametumia mwanya huo kufanya walivyofanya; masikhara masikhara kumbe kweli. WAMETHUBUTU, WAMEWEZA NA WANASONGA MBELE, hakuna mtu wa kuwazuia. Watu wana macho lakini wamejifanya vipofu, wana masikio lakini wamejifanya viziwi na wana midomo lakini wamejifanya bubu. Ujanja eti ni kuficha bomu kwenye kitanda unacholalia kila siku kumbe haina tofauti na mhanga anayejifungia mabomu ili ajilipue kwa makusudi.[/FONT]
   
 11. fige

  fige JF-Expert Member

  #11
  Dec 8, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Akili ya binadamu ni ya ajabu sana,anaweza kusoma fiction ndefu lakini akashindwa kuelewa mistari michache tu ya biblia au quran
   
 12. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #12
  Dec 8, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Siyo hivyo tu, ndio tunavyoibiwa waafrika, kahabari kafupi mtu anadai inaboa. Kesho analetewa mkataba wa page 30, ndani wamechomekea "In case of any dispute, the matter shall be resolved by the CEO of this company. The decision shall be final and the government shall ABIDE it".

  Hawa ndio wanaoleta RICHMOND
   
 13. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #13
  Dec 8, 2011
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Duh! Inasikitisha sana. Tanzania=Afrika=Russia, lao moja! Hakuna demokrasia, ukibisha wanakuua!
   
 14. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #14
  Dec 8, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ndio kipimo cha uwezo wako wa kufikiri. Umezoea mipasho ambayo huwa mstari mmoja kama kwenye khanga eeh!
   
 15. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #15
  Dec 8, 2011
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nadhani ktk ujinga na upumbafu watanzania tutakao jutia ni hili suala la kunyimwa uhuru wa kujadili katiba, kwani CCM hawana tofauti na mkoloni, halafu walivyowajinga hawafahamu wanaweza kuja siku moja na wao kuwa wapinzani? au kuji John Shibuda?
   
 16. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #16
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,016
  Likes Received: 2,670
  Trophy Points: 280
  Kama hako ka kipande kamekushinda,je katiba utaweza kuisoma?punguza uvivu tutakuacha mbali.
   
 17. Prisoner 46664

  Prisoner 46664 JF-Expert Member

  #17
  Dec 8, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Nyie ndio mnaosababisha watu waseme ukitaka kutufichia watu weusi kitu weka kwenye kitabu..acha uvivu.
   
 18. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #18
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Ndio maana mnasaini mikataba kama vipovu, hiyo habari ina urefu gani? hivi mtu wa aina yako kweli unaweza kwenda kujisomea library kwa masaa matatu?
   
 19. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #19
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,094
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  mkuu acha uvivu,habari ndefu si ndo inafafanua vizuri??
   
 20. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #20
  Dec 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Anaesema hbr ndefu namfananisha na alosain muswada,NAE NI MVIVU
   
Loading...