MwanaHalisi, Tz.Daima, Dira,Raia Mwema, Mwananchi yafungwa mdomo kuhusu Manji

Kuna Watanzania wenzetu wanatanua na wanakula maisha kwa kuwalinda na kuwatetea kwa nguvu zao zote kina Manji. This is serious maana wengine ni watu wanaoheshimika na kuaminika sana, lakini wajue wanaonekana, wanajulikana na wataumbuka maana Watanzania wa sasa si wa mwaka 47 na si mabwege tena

Na mbaya zaidi, baadhi yao wameamnzisha vyombo vya habari, nasi kama vichaa, kila wanachoandika tunakishabikia. Wengine tumewatunuku vyeo kwenye vyama tunavyotegemea kuja kutukomboa. Nimekuwa najiuliza Marando kumsaidia Manji kuzuia ushahidi wa nyaraka za ufisadi wake Kagoda mahakamani na kukosa majibu.
 
Kesi hiii itazimwa .Kesi hii imelenga kumzuia Msemakweli na magazeti kutosema lolote kwa kuwa watakuwa wanaongelea jambo lililoko Mahakamani .Hapa ma CCM yanazima issue kijanja na hapatakuwa na kesi .Kama unabisha wewe hebu nieleze kesi aliyo fungua Rizwan iko wapi sasa.Huyu Manji anafungua kesi na wakati majuzi alikuwa anarusha matusi hadharani kwa Msemakweli ama kesha sahau ?

Ukimdai mtu deni lako , ukafikia kumpiga maana yake umeamua kuachana na deni unalo dai sasa Manji karudha matusi na leo anataka haki je kutukana ilikuwa haki yake yeye ?

Sarakasi hizi wacha nipande ndege niende safari nitasoma huko huko kinacho tokea .

Hivi Ridhwan amewahi kufungua kesi?

Kama Manji alitukana aliyetukanwa si aende mahakamani? Au hatuziamini mahakama zetu kwamba zitatoa haki? Mahakama ndiyo sehemu ambapo haki inaweza kutolewa na si kwenye magazeti wala TV au matusi!
 
Na mbaya zaidi, baadhi yao wameamnzisha vyombo vya habari, nasi kama vichaa, kila wanachoandika tunakishabikia. Wengine tumewatunuku vyeo kwenye vyama tunavyotegemea kuja kutukomboa. Nimekuwa najiuliza Marando kumsaidia Manji kuzuia ushahidi wa nyaraka za ufisadi wake Kagoda mahakamani na kukosa majibu.

Mwanasheria wa Chadema wakati huo huo mwanasheria wa watuhumiwa wa ufisadi!! Hapo patamu. Hivi Silaa akisimama akasema Manji ni fisadi Marando inabidi aseme Manji si Fisadi kwa kuwa anamtetea mahakamani na anaamini si fisadi.

Kwa kweli kiungwana ingebidi Marando aachane na kitu kimoja; kama ni CHADEMA basi aachane na mafisadi na kama ni mafisadi basi aachane na CHADEMA. Kwa kifupi inabidi Marando ajivue gamba na kama CHADEMA inaona kujivua gamba ni neno la CCM basi na wao watafute neno lao lakini likiwa na maana ya kujitakasa.
 
Manji waonee huruma masikini kwa kurudisha hela yote uliyoiba kumbuka we ni muislamu safi fanya hivyo na Mola atakulipa!!
 
Ugomvi wa Manji na Mengi ndio umeibua yote haya
Ni mategemeo yangu kuwa wataendelea kuumbuana mpaka yote yatajulikana na hatimaye VYOMBO VYA SHERIA VITAMALIZIA.
 
jalada la kesi hiyo namba 135 ya 2011, lilipofika kwa Jaji Jundu...baada ya Jaji Kiongozi Fakihi Jundu
Bongo bana, kesi za kukandiana zinaanzia kwa Jaji Kiongozi, kesi za wizi wa mabilioni zinaenda kwa hakimu wa kata!
 
[jfmp3][/jfmp3]
kazi nzuri manji... Waache kukurupuka!
Chonde chonde.. Ukishinda kesi yako usimuadabishe mengi kwa kumdai sh. 1
uwe na mapenzi ya dhati kwa taifa lako na watu wake,usipende ku support ujinga.au na mhindi nini?au ni mtanzania mwenye asili ya ki asia?!!!!
 
Huyu mtu anatoa wapi ujasiri huu?

Anapata jeuri toka kwa mkulu kabisa, kwani hata wakati ule alipoiba mabilioni ya NSSF ni huyu mkulu ndiye alimpa ujanja wa kwenda kujichimbia Yanga, na kweli alifanikiwa kwani aliitumia Yanga kama sabuni na manukato kiasi kwamba wabongo wameshasahau kuwa huyu fisadi alikwapua fedha za walala hoi,leo hii ukitaja Manji unataja Yanga.
 
hata kijinga cha taa huwa hakiwekwi chini ya kitanda mana hakitatoa mwanga hvo ukweli utajulikana tu
 
Mwanasheria wa Chadema wakati huo huo mwanasheria wa watuhumiwa wa ufisadi!! Hapo patamu. Hivi Silaa akisimama akasema Manji ni fisadi Marando inabidi aseme Manji si Fisadi kwa kuwa anamtetea mahakamani na anaamini si fisadi.

Kwa kweli kiungwana ingebidi Marando aachane na kitu kimoja; kama ni CHADEMA basi aachane na mafisadi na kama ni mafisadi basi aachane na CHADEMA. Kwa kifupi inabidi Marando ajivue gamba na kama CHADEMA inaona kujivua gamba ni neno la CCM basi na wao watafute neno lao lakini likiwa na maana ya kujitakasa.

Marando anasema manji ni fisadi dagaa,mapapa na nyangumi hawajakamatwa.source:mdahalo(Nape alimchana vibaya marando kwenye mdahalo maana marando anapambana na mafisadi huku akiwatetea!!!!!!!!!!!!!)
 
Kuna mtu anasema njaa zetu zinatuponza, mimi nasema UJINGA wetu unatuponza maana hata India, Indonesia, Msumbiji,zimbabwe, Rwanda, Uganda kuna wenye njaa zaidi yetu lakini watu wanathamini utu wao, si kulamba watu mata.. Kama tulivyo sisi Watanzania na bado watu na heshima zao wanasota na mijitu kama wabunge na madiwani eti waliungishwa foleni pale Nyerere road kupewa laki tano.
 
Mbona anaanza kutapatapa hata kabla moto haujawashwaaa??!!?? c'mon! ningeshauri hati yake ya kusafiria ikamatwe kwanza maana dalili zinaonyesha atakimbia nchi kama mwenzake wa fukuto la wanyama pori alivyofanya! sasa naanza kuamini kuwa mafisadi ni hatari.
 
Ugomvi wa Manji na Mengi ndio umeibua yote haya

Ni mategemeo yangu kuwa wataendelea kuumbuana mpaka yote yatajulikana na hatimaye VYOMBO VYA SHERIA VITAMALIZIA.

Wengi wameingia mtego wa mafisadi, na sasa wanaimba nyimbo zao, "ugomvi binafsi wa Mengi na Manji", "Sita alitaka Uwaziri Mkuu ndio akamfanyia fitina Lowassa", "ugomvi binafsi wa kibiashara kati ya Rostam na wenzake", na sasa hakuna tena facts kuhusu Kagoda (hata humu JF unaona kigugumizi),hakuna tena wizi wa Comodity Import Support (CIS), hakuna tena utapeli wa pension fund zetu, na hakuna tena ufisadi katika richmond, hakuna tena wizi wa Meremeta, hakuna tena uhamishaji wa fedha kwenda UK, hakuna lolote, ni wivu na maugomvi ya kisiasa na kibiashara na sasa hata Msemakweli ametumwa na wagomvi wa kibiashara wa Manji na Rostam na kwamba ushahidi alioutoa amepewa na wagomvi wa Manji na Rostam (hakuna anayesema ushahidi wa uongo, akiwamo Manji),...

Nchi imekua ya majuha na walafi wa mlo wa leo na kulala vizuri na kutanua bila kujali vizazi vijavyo, hatujali athari za giza lilipo, uhaba wa maji, elimu duni na vifo vya watoto wadogo ni zao la ufisadi? Tumekua taifa la watu wasioona wala kusikia. Inasikitisha hata vyombo vya dola ambavyo katika mbinu za upelelezi inafundishwa kwamba source mzuri wa taarifa ni mtu aliyekua karibu ama aliyeshirikiana na mhalifu. Mara nyingi majambazi husaidia kukamatwa kwa majambazi, ama marafiki ama ndugu wa wahalifu husaidia kupatikana kwao, ama mtu aliyegombana na mhalifu ama akiwa mke, rafiki, mfanyakazi na huwa taarifa zao huwa muhimu, watu wenye chuki husaidia kufichua uhalifu wa mmoja wao, lakini ajabu sana kuna wenzetu wamefumbwa macho hawajadili facts wanajadili majina ya watu, wamechotwa na ujinga wa mafisadi kujificha nyuma ya pazia la "ugomvi" ama "chuki" na sisi tunawalamba miguu.

Tutalaaniwa na kulaanika na vizazi vijavyo na vitafukua makaburi yetu; hii haitasameheka milele hata ahera: MUNGU IBARIKI TANGANYIKA, MUNGU WAANGAMIZE MAFISADI NA WAPAMBE WAO.
 
Back
Top Bottom