MwanaHalisi, Tz.Daima, Dira,Raia Mwema, Mwananchi yafungwa mdomo kuhusu Manji

Prof

JF-Expert Member
Feb 24, 2010
1,578
2,410
Ndugu wana jamii, katika sakata la mwanaharakati msemakweli kumlipua Manji dhidi ya wizi wa fedha za umma, manji amejibu mapigo kwa kufungua kesi dhidi ya mwanaharakati msemakweli, akimwunganisha Mengi kwenye kesi hiyo.

Nimebahatika kupata nakara ambayo nime attach lengo wote tupate habari.

Mfanyabiashara Yusuf Manji, anachotaka ni kuwafunga midomo watu wanane na mitandao yote kuzungumzia kuhusika kwake na wizi wa kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, baada ya Jaji Kiongozi Fakihi Jundu kusita hata kupangia tarehe maombi ya mfanyabiashara huyo mtata ya kutaka asikilizwe pekee mahakamani.

Katika maombi yake mahakamani aliyowasilisha mahakamani Alhamisi Septemba 8, 2011, Manji alitaka kufungwa midomo kwa watu wanane wakiwamo Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, Mwanaharakati, Kainerugaba Msemakweli, waandishi wa habari Saed Kubenea na Islam Mbarak.

Hata hivyo, jalada la kesi hiyo namba 135 ya 2011, lilipofika kwa Jaji Jundu, halikupangiwa tarehe ya kusikilizwa, jambo ambalo lilikwamisha mpango wa Manji kuzima kabisa kuzungumzwa kwa Kagoda hadharani na mtu yeyote.

Wengine ambao Manji alitaka mahakama iwazuie kuzungumza lolote kumhusu hata bila upande wa pili kusikilizwa (Ex-Parte) ni Sabas Kiwango, Silvanus Chingota na Zuberi Kiponda.

Manji katika maombi yake hayo ambayo pia anaishitaki Kagoda, anaiomba mahakama bila kusikiliza upande wowote kuamuru maandiko yote yaliyopo katika mitandao ya intaneti, blogs na tovuti kuondolewa mara moja na kuzuiwa mitandao yote kuzungumzia lolote kumhusu bila ya yeye kutoa kibali cha maandishi.

Pamoja na kuzuia na kutaka mahakama iamuru taarifa zote katika mitandao zinazomhusu ziondolewe na mtu yeyote asiweke katika mtandao taarifa zake, Manji pia ametaka mahakama iamuru watu wote wanane aliowalalamikia na washirika wao kukabidhi nyaraka zote walizonazo zinazomhusu, makabidhiano ambayo anataka yaambatane na kiapo.

Manji pia anataka pia mahakama iwazuie watu aliowalalamikia wazuiwe kufanya mawasiliano na watu wote ambao wanahusiana kibiashara, kisiasa na hata kijamii, kwa jambo lolote linalomhusu yeye, kampuni zake ama washirika wake kwa namna yoyote ile.

Manji katika kesi hiyo anawakilishwa na wakili Nasir Hussein Rattansi, katika nyaraka zilizoandaliwa na kampuni ya Law Associates, zenye ofisi zake jengo la CRDB, mtaa wa Azikiwe, Dar es Salaam.

Malalamiko ya Manji yanatokana na mkutano wa waandishi wa habari uliofanywa na Msemakweli na kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwamo televisheni ya ITV ambayo mfanyabiashara huyo pia anaitaja katika hati yake ya kiapo aliyoiwasilisha mahakamani.

Katika mkutano huo, Msemakweli alitaja wahusika wa Kagoda akiwamo Manji na watu wengine kadhaa pamoja na kuwasilisha nyaraka kadhaa, ambazo awali aliziwasilisha kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).

Tayari serikali imekwishachukua hatua kwa kuunda kikosi kazi cha kuchunguza sakata hilo huku Msemakweli akiitwa kutoa ushirikiano kwa kuandika maelezo.

Mawakili, Ratansi na Law Associates wanahusika na Kagoda, na majina yao yamo katika nyaraka alizowasilisha Msemakwali kwa DPP na DCI. Ratansi ndiye aliyasaini nyaraka za mkataba kati ya Manji na Kagoda wakati Law Associates walihusika katika kampuni ya Afritainer iliyohusika pia katika EPA ya mwaka 2000 na ina uhusiano na Kagoda. (Docs zote zimo humu JF)
.

Baada ya kufanikiwa kupata uamuzi wa mahakama ya Temeke kuzuia Mwanahalisi lisimuandike na kubenea kukabidhi nyaraka zote kumhusu, Manji sasa amepata uamuzi wa mahakama ya kinondoni kuzuia raia mwema lisimuandike na kuzuia raia mwema na marafiki zake kutoandika wala kutoweka ktk mitandao habari zozote kuhusu Kagoda na Manji. Pia imefahamika kwamba ameshafanikiwa toka Julai 2001 kupata hukumu Mahakama ya kinondoni kuzuia magazeti yanayotolewa na Mwananchi Communication ya Mwananchi na Citizen kumuandika kuhusu jambo lolote bila kibali chake. Pia kesho anataka mahakama ya kinondoni izuie Tanzania Daima lisimuandike. Tayari Manji amekwama kumzuia Mengi, Msemakweli na wengine kumuandika ama kumsema. Manji amefungua kesi mbili tofauti zinazofanana mahakama kuu na zote anataka kuzuia uhuru wa habari kwa kutaka mitandao yote (Ikiwamo JF) izuiwe kumuandika na itoe habari zake zote haraka iwezekanavyo na wote wenye uhusiano na aliowashitaki kisiasa, kijamii na kibiashara kuzuiwa nao kumsema kwa njia yoyote.

kesi-manji.jpg


attachment.php

attachment.php

attachment.php


Zaidi, angalia attached images chini
 

Attachments

 • 111017.jpg
  111017.jpg
  80.7 KB · Views: 132
 • Manji 1.jpg
  Manji 1.jpg
  56.7 KB · Views: 63
 • Manji 2.jpg
  Manji 2.jpg
  29.5 KB · Views: 49
 • Manji 3.jpg
  Manji 3.jpg
  39.1 KB · Views: 44
 • Manji 4.jpg
  Manji 4.jpg
  57 KB · Views: 883
 • Manji 5.jpg
  Manji 5.jpg
  50.1 KB · Views: 873
 • Manji 6.jpg
  Manji 6.jpg
  52.2 KB · Views: 42
 • Manji 7.jpg
  Manji 7.jpg
  49 KB · Views: 42
 • Manji 8.jpg
  Manji 8.jpg
  47.5 KB · Views: 39
 • Manji 9.jpg
  Manji 9.jpg
  43.4 KB · Views: 41
 • Manji 10.jpg
  Manji 10.jpg
  48.7 KB · Views: 898
 • Manji 11.jpg
  Manji 11.jpg
  33.5 KB · Views: 37
 • Manji 12.jpg
  Manji 12.jpg
  6.6 KB · Views: 49
 • Manji 13.jpg
  Manji 13.jpg
  6 KB · Views: 52

Rejao

JF-Expert Member
May 4, 2010
9,236
4,041
Kazi nzuri Manji... waache kukurupuka!
Chonde chonde.. ukishinda kesi yako usimuadabishe Mengi kwa kumdai sh. 1
 

lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,470
9,013
DPP alishindwa kuipeleka kesi hii mahakamani kwa kukosa ushahidi sasa "imeenda yenyewe". Pamoja na kuwa tuna macho lakini tutakuwa tayari kama wanaanchi wa kawaida kusidia itakapotakiwa kufanya hivyo!
 

Omr

JF-Expert Member
Nov 18, 2008
1,160
99
Mdosi dume huyo, anajiamini sana. safari hii lazima wamlipe nyingi tu.
 

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,869
9,820
Mahakama si ndio chombo cha kutoa haki? Basi Manji anafanya vema kuitafuta haki mahakamani. Mwisho wa siku tutajua nani muongo ama mkurupukaji. Manji amechukua njia sahihi
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
Kesi hiii itazimwa .Kesi hii imelenga kumzuia Msemakweli na magazeti kutosema lolote kwa kuwa watakuwa wanaongelea jambo lililoko Mahakamani .Hapa ma CCM yanazima issue kijanja na hapatakuwa na kesi .Kama unabisha wewe hebu nieleze kesi aliyo fungua Rizwan iko wapi sasa.Huyu Manji anafungua kesi na wakati majuzi alikuwa anarusha matusi hadharani kwa Msemakweli ama kesha sahau ?

Ukimdai mtu deni lako , ukafikia kumpiga maana yake umeamua kuachana na deni unalo dai sasa Manji karudha matusi na leo anataka haki je kutukana ilikuwa haki yake yeye ?

Sarakasi hizi wacha nipande ndege niende safari nitasoma huko huko kinacho tokea .
 

IGWE

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
9,337
6,882
Tutaona mwisho wa sakata hili,...ila naomba Mungu manji na waizi wenzie washindwe hii kesi,.maake mmmmh
 

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
19,412
23,581
anakurupuka.kuna wanaomdanganya ili wamlie hela.vya mjinga huliwa na mwelevu.mia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

6 Reactions
Reply
Top Bottom