Mwanahalisi sio wanafki

AMARIDONG

JF-Expert Member
Jun 24, 2010
2,502
0
VIGOGO kadhaa wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) wametajwa “kuingilia” Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), MwanaHALISI limegundua.
Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya idara hiyo zinaeleza kuwa vigogo hao wana mahusiano ya karibu na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe.
Anayetajwa rasmi kuwa na mahusiano na Zitto ni Naibu Mkurugenzi wa TISS, Jack Zoka.
Kufichuka kwa taarifa za kuwapo “uswahiba” kati ya Zoka na Zitto kumekuja katika kipindi ambacho CHADEMA kimekuwa kikituhumu maofisa wa juu wa usalama wa taifa kuvuruga uchaguzi mkuu uliopita.
Aidha, kuibuka kwa tuhuma hizi kumekuja wiki moja baada ya gazeti hili kuchapisha taarifa mbalimbali za mawasiliano kati ya Zitto na Rais Jakaya Kikwete.
Baadhi ya mawasiliano hayo, ambayo Zitto ameyapeleka kwa rais, aliyapeleka pia kwa baadhi ya watuhumiwa ufisadi nchini.
Kwa mujibu wa mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa ambaye alitangazwa kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Kikwete; viongozi wa TISS walihusika, kwa kiasi kikubwa, katika kile alichoita, “Kuchakachua matokeo ya uchaguzi.”
MwanaHALISI limefanikiwa kupata rekodi ya mshororo wa mawasiliano kati ya Zitto na Zoka.
Kuna mwingiliano wa simu za mdomo na maandishi (sms) kutoka kwa Zitto kwenda kwa baadhi ya vigogo wa ngazi ya juu serikalini na TISS, hasa Zoka.

Nyaraka za mawasiliano zinaonyesha kuwa Zitto amekuwa akiwasiliana na naibu mtendaji mkuu wa TISS huyo zaidi ya mara tatu kwa siku.

Kwa mfano, Zitto na Zoka walifanya mawasiliano ya simu mara tisa hapo tarehe 8 Agosti. Simu iliyotumika katika mawasilino hayo, ni Na. +255756809535 ambayo hutumiwa na Zitto na +255754787550 ambayo hutumiwa na Zoka.
Wakati mawasiliano hayo yanafanyika, Zitto alikuwa katika maeneo tofauti.
Mawasiliano ya kwanza kati ya Zitto na Zoka yalipokuwa yanafanyika, simu ya Zitto ilisomeka kuwa alikuwa katika maeneo mbalimbali.
Mathalani, wakati mwingine simu ilikuwa ikisomeka kuwa yuko Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam, Kigoma Urban (Mjini), Kigoma Rural (Vijijini), Mtwara, Uwanja wa ndege-Ilala, Oyster Bay, Ukonga, Upanga na katikati ya mji.
Gazeti hili halikuweza kugundua mara moja undani wa mawasiliano ya Zitto na Zoka.
Kinachofanya baadhi ya wachunguzi wa mambo kujenga shaka ni kwamba mmoja ni mwanasiasa, tena kutoka chama kilichopo nje ya utawala; na mwingine ni mtumishi wa idara ya usalama inayolalamikiwa kukandamiza upinzani nchini.
Hata hivyo, taarifa zinaonyesha kuwa mawasiliano kati ya Zitto na Zoka yalianza kupamba moto kuanzia tarehe 6 Agosti 2010, siku moja baada ya CHADEMA kuzindua kampeni zake za urais.
Kulingana na uchunguzi, siku hiyo, tarehe 6 Agosti, simu ya Zitto ilisomeka kuwa yuko Kigoma Urban.
Katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni, CHADEMA kupitia kada wake mashuhuri, Mabere Marando, iliibuka na lundo la tuhuma dhidi ya vigogo kadhaa wa serikali, CCM na idara ya usalama wa taifa.
Akizungumza na maelfu ya wananchi katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam, Marando alisema wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya Benki Kuu ya taifa (BoT), ulifanywa na serikali na washirika wake.
Miongoni mwa vigogo aliodai kuwa walihusika kufanikisha wizi huo, ni rais wa sasa, Jakaya Kikwete, rais mstaafu Benjamin Mkapa, mbunge wa Igunga, Rostam Aziz na Edward Lowassa.
Akiongea kwa kujiamini, Marando alisema, “fedha za EPA ni wizi uliotiwa baraka na serikali ya CCM na ndio uliomsaidia rais Kikwete kuingia madarakani mwaka 2005.”
Kuanzia hapo hadi sasa, Zitto na Zoka wamekuwa na mawasilino ya mara kwa mara, na karibu kila siku huzungumza kwa simu.
Mawasiliano mengine ya mara kwa mara yalifanyika tarehe 7 Agosti 2010, siku mbili tangu hotuba kali ya Jangwani. Yalianza saa 10:17 na kuendelea tena saa 10:50, saa 10:51:31, saa 11:46:13, saa 12: 14:46, saa 12:26:48 na saa 13:50: 21.
Lakini Zitto alipoulizwa kuhusu sababu ya yeye kufanya mawasiliano ya mara kwa mara na vigogo wa TISS, alisema hajui na hakumbuki lolote kuhusu kuwapo mawasiliano hayo na Zoka au mkuu yeyote wa idara hiyo.

Zitto amesema yeye, akiwa mwanasiasa na kiongozi, anazungumza na watu wengi kutoka katika taasisi na mashirika mbalimbali ndani na nje ya nchi, lakini hajui kitu kuhusu usalama wa taifa.

Alipobanwa kuhusu mazungumzo yake na Zoka, hasa yale ya 3 Novemba 2010, saa nne na dakika 56 asubuhi, siku mbili baada ya uchaguzi kumalizika, Zitto alisema, “Siku hiyo nilizungumza na watu wengi sana. Siwakumbuki ni akina nani hasa.”

Alisema, “Hicho ndicho kipindi ambacho matokeo ya uchaguzi nchini kote yalikuwa yakizuiwa ikiwamo kwetu Kigoma. Na ukumbuke mimi nilipigwa mabomu na polisi na usalama wa taifa. Nakumbuka viongozi wengi wa vyombo vya ulinzi na usalama walinipigia simu kunijulia hali na kupata taarifa ya kilichotokea,” anaeleza.

“Sasa kama Zoka naye alinipigia siku hiyo sikumbuki; lakini nilipigiwa na wengi…Naomba uniambie kitu, hivi mnachokitafuta hasa ni nini?” aliuliza.

Katika njia ya kujitetea, Zitto aliuliza, “Mwanasiasa kuongea na wakuu wa vyombo vya usalama ni kosa? Maana, hata kama ningekuwa nimezungumza naye, kosa langu liko wapi?” alieleza mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini.

Alipoelezwa kuwa haoni hiyo ni hujuma dhidi ya chama chake kwa kuzungumza na viongozi wa TISS na kile ambacho amekuwa akikizungumza kikiwa hakifahamiki kwa viongozi wake, Zitto alisema, “Sijawahi kukihujumu chama changu mahali popote, siku yoyote.”

Jitihada za gazeti hili kuzungumza na Zoka hazikufanikiwa katika kipindi chote
cha mwishoni mwa wiki, kwa vile kila alipopigiwa, simu yake ya mkononi ilikuwa haipokelewi.

Hata ujumbe mfupi wa maneno uliotumwa kwenye simu yake saa 2:53 asubuhi ya Jumapili; ukieleza sababu za gazeti kuzungumza naye, haukujibiwa.

Aidha, tarehe 2 Novemba, siku moja baada ya kuzungumza na Zitto, Zoka alinukuliwa akikana madai ya Dk. Slaa, kuwa TISS imesaidia kuvuruga uchaguzi.

Katika taarifa yake aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari, ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Zoka alisema, “Dk. Slaa amekuwa akidanganywa na watu wanaojiita maofisa wa usalama wa taifa.”
Hata hivyo, kuna meseji mbalimbali kuhusu udini na uamuzi wa CHADEMA kususia hotuba ya rais Kikwete ambazo zilitumwa na Zitto kwa baadhi ya wabunge wa CHADEMA ambazo zinadaiwa kuandaliwa na idara ya usalama wataifa.
Ujumbe huo unadaiwa kuandaliwa kwa ustadi mkubwa katika kukuza suala la udini na kuleta mtafaruki katika chama.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom