Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Mbunge wa Monduli, Edward lowassa anadaiwa kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete amrejeshe katika Baraza la mawaziri, imefahamika.
Lowassa ameomba kupatiwa nafasi ya kuongoza wizara yta mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa, wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa, au wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa.
Habari zilizothibitishwa na mmoja wa viongozi wa ngazi za juu katika Chama cha Mapinduzi (CCM) na ambaye yuko karibu na rais Kikwete na Lowassa, zinasema shinikizo la Lowassa limekuwa kubwa kiasi ambacho linamuweka Kikwete njiapanda.
Lowassa anataka kurewjeshwa katika Baraza la mawaziri. Ameomba apewe nafasi ya kuongoza wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa, au wizara ya mambo ya nje, ameeleza mtoa taarifa wa MwanaHalisi.
Amesema, Mheshimiwa Lowassa anasema, iwapo hilo likishindikana, basi ateuliwe kuwa waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa.
Kigogo mwingine ambaye ameomba kurejeshwa katika baraza la mawaziri ni Andrew Chenge ambaye anataka kuwa waziri wa miundombinu.
Chenge ambaye anakabiliwa na lundon la tyuhuma za ufisadi ikiwamo kashfa ya ununuzi wa rada, ameomba kupatiwa uwaziri katika wizara ya miundombinu au sheria na katiba.
Taarifa zinasema Chenge ameshinikiza kuwa iwapo wizara ya miundombinu iutagawanywa kwa kurejeshwa kama ilivcyokuwa zamani, ambapo kulikuwa na wizara ya mawasiliano na uchukuzi, na ile ya ujenzi, basi yeye akabidhiwe wizara yaujenzi ...
.Mtoa taarifa anamtaja anayeshikia bango Kikwete kumrejesha Lowassa katika Baraza la Mawaziri kuwa ni mfanyabiashara na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.
Rostam amekuwa akitajwa kuwa anajitapa kwamba hatua ya chama hicho kufanikiwa kumuengua Samuel Sitta italeta amani katika chama na kwamba kwa sasa hakuna kizingiti kingine kinachomzuia Lowassa kurejeshwa katika serikali.
Hata hivyo Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka alipoulizwa kama hatua ya kumuondoa Sitta inaweza kurejesha umoja katika chama, haraka alisema, Vita haijaisha.
Alisema Ugomvi wetu haukuwa ubinafsi. Ulihusu maslahi ya nchi na watu wake. Kama Rostam, Chenge na Lowassa wanadhaniu vita imekwisha kwa Sitta kutokuwa Spika, basi hawajui kiini cha ugomvi. Hiki ni kicheko cha muda tu.
Habari zaidi katika MwanaHALISI ya leo Uk. wa 6.