MwanaHALISI: Lowassa ashinikiza uwaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MwanaHALISI: Lowassa ashinikiza uwaziri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Nov 17, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mbunge wa Monduli, Edward lowassa anadaiwa kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete amrejeshe katika Baraza la mawaziri, imefahamika.

  Lowassa ameomba kupatiwa nafasi ya kuongoza wizara yta mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa, wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa, au wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa.

  Habari zilizothibitishwa na mmoja wa viongozi wa ngazi za juu katika Chama cha Mapinduzi (CCM) na ambaye yuko karibu na rais Kikwete na Lowassa, zinasema shinikizo la Lowassa limekuwa kubwa kiasi ambacho linamuweka Kikwete njiapanda.

  “Lowassa anataka kurewjeshwa katika Baraza la mawaziri. Ameomba apewe nafasi ya kuongoza wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa, au wizara ya mambo ya nje,” ameeleza mtoa taarifa wa MwanaHalisi.

  Amesema, “Mheshimiwa Lowassa anasema, iwapo hilo likishindikana, basi ateuliwe kuwa waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa.”

  Kigogo mwingine ambaye ameomba kurejeshwa katika baraza la mawaziri ni Andrew Chenge ambaye anataka kuwa waziri wa miundombinu.

  Chenge ambaye anakabiliwa na lundon la tyuhuma za ufisadi ikiwamo kashfa ya ununuzi wa rada, ameomba kupatiwa uwaziri katika wizara ya miundombinu au sheria na katiba.

  Taarifa zinasema Chenge ameshinikiza kuwa iwapo wizara ya miundombinu iutagawanywa kwa kurejeshwa kama ilivcyokuwa zamani, ambapo kulikuwa na wizara ya mawasiliano na uchukuzi, na ile ya ujenzi, basi yeye akabidhiwe wizara yaujenzi……...

  …….Mtoa taarifa anamtaja anayeshikia bango Kikwete kumrejesha Lowassa katika Baraza la Mawaziri kuwa ni mfanyabiashara na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.

  Rostam amekuwa akitajwa kuwa anajitapa kwamba hatua ya chama hicho kufanikiwa kumuengua Samuel Sitta italeta amani katika chama na kwamba kwa sasa hakuna kizingiti kingine kinachomzuia Lowassa kurejeshwa katika serikali.

  Hata hivyo Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka alipoulizwa kama hatua ya kumuondoa Sitta inaweza kurejesha umoja katika chama, haraka alisema, “Vita haijaisha.”

  Alisema “Ugomvi wetu haukuwa ubinafsi. Ulihusu maslahi ya nchi na watu wake. Kama Rostam, Chenge na Lowassa wanadhaniu vita imekwisha kwa Sitta kutokuwa Spika, basi hawajui kiini cha ugomvi. Hiki ni kicheko cha muda tu.”…………………


  Habari zaidi katika MwanaHALISI ya leo – Uk. wa 6.
   
 2. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2010
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,548
  Likes Received: 1,307
  Trophy Points: 280
  Kwa nini wanamshinikiza mheshimiwa???????

  Kwa nini wanataka wizara zenye tender kubwa kubwa ama nyeti Ulinzi?????

  Kuna jambo gani litatokea kama matakwa yao hayatatimizwa?
   
 3. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  kwa nini walilie hizo nafasi kuna ulazima kwa wao kuongoza si wanaongoza majimbo yao basi watilie mkazo huko sio kulazimisha mambo, ikiwa hivyo na January makamba Naye atalazimisha apewe uongozi wa wizara ya habari na michezo.!
   
 4. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  lowassa big man very influential and still very controversy.
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Inaonekana hawa jamaa(chenge na Lowasa) wanahusika kwa kiasi kikubwa ktk jitihada tena za mali kumweka JK madarakani hivyo asipotimiza matakwa yao si unajua cha mtu hakiendi bure!
   
 6. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwanini wanataka nafasi hizo?Majibu yako wazi:
  1. Wanataka waendelee na kazi iliyobaki ya kujisafisha baada ya kumwondoa Sitta.
  2. Baada ya kujisafisha waendelee na kujiandaa kwa mwaka 2015 kwa nafasi nyeti ya kuongoza nchi au mtu wao aongoze nchi.
  3. Kwa ujumla wanataka wajilinde kwa gharama yoyote ile dhidi ya tuhuma na mashtaka kuhusiana na ufisadi.

  Sidhani kama kuna kitu kingine zaid ya hicho.
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kitu kimoja kibaya sana JK anachoweza kukifanya ni kumpa EL Wizara ya Habari., Utamaduni na Michezo. Atayashughulikia vilivyo, na pengine kuyafungia magazeti kama MwanaHALISI, Raia Mwema, Tanzania Daima na hata Mwananchi. ITV ya Mengi nayo itakuwa hatarini kufungiwa ikiwa itazidi kujiweka mstari wa mbele katika vida dhidi ya ufisadi.

  Kina EL na RA hawataki kuona vita hiyo ikiendelezwa kwenye vyombo vya habari kwani itakuwa kila mara inawagusa wawili hao na hivyo kuondoa ndoto zao za kushika nchi mwaka 21015.
   
 8. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kitu kingine zaidi ya hilo ni kwamba wanataka waendelee kujilimbikizia mali zaidi kwa walizonazo hawatosheki nazo.
   
 9. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #9
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Who is this Lowassa guy? Yaani ana nguvu gani za kumshinikiza Rais?
   
 10. f

  freshmind Member

  #10
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Udictator unataka kudhihirishwa kwenye nchi hii!enough is enough!
   
 11. Thomas Odera

  Thomas Odera Verified User

  #11
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 644
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hivi kwa nini EL asipewe wizara ya watoto na wamama kama ana nia njema na watu wa nchi hii Vinginevyo ana agenda ya siri
   
 12. T

  Tofty JF-Expert Member

  #12
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 6, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mmmh hawajamaa wakikubaliwa matakwa yao basi tutakuwa tunakwenda pabaya kwani wanaangalia kujiweka pazuri kwa ajili ya 2015
   
 13. s

  seniorita JF-Expert Member

  #13
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Haya sasa mambo ya kulipa fadhili, will JK manage to return favor without jeopardizing his position, (which is acquired not earned), is already shaky? Kazi kwako mkubwa,
   
 14. w

  watarime Senior Member

  #14
  Nov 17, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 105
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mafisadi wana nguvu ndani ya CCM na JK nazani hana uchungu na Taifa hili kuna uwezekano mkubwa akatii SAUTI zao mana ndio waliomweka madarakani kwa njia za Ufisadi since his 1st Elect 2005
   
 15. M

  Micho Senior Member

  #15
  Nov 17, 2010
  Joined: Apr 12, 2009
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Tumechoshwa......ufisadi umekua ni mradi..na mradi huo shareholders wanaonekana hata vipofu wanawaona...sasa enough is enough japokuwa mmeshauliza si vibaya na mimi kurudia tena...who is RS? who the hell are they? to be very frank they are just to i.d.i.o.t.s with their dirty money but does that mean they have all the power to infridge the rights of 45mil - 2ppl(EL and RS) Please I need answers?....Just now
   
 16. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #16
  Nov 17, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Jamani jamani! hivi hawa watu wamejisahau kabisa na kuona hili linchi ni lao kabisa! kwani ni kazima wawe mawaziri?? ohh, Ugly & vicious!!
   
 17. m

  mamanalia JF-Expert Member

  #17
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 671
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  lowassa ni big man kwa rais weak kama kikwete, usimsifie hapa, ni mzembe fulani tu, angekuwa strong asingehangaika na kuomba kupewa vyeo angeweka mkazo kwenye strong businesses kama walivyo kina Mengi.

  To me lowasa is just a naughty guy.
   
 18. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  EL anataka wizara ya aina yoyote ile ilimradi tu aweze kuwemo katika baraza la mawaziri......Cha kujiuliza ni kwa nini anataka awepo humo????? easy...AFANYE MAAMUZI wa maslahi yake na familia yake target ikiwa 2015...Jamaa anasupport kubwa sana kwa watu ambao ameshawachomeka katika ukuu wa mikoa, wilaya, na wenyeviti wa CCM mikoani na wilayani...Ila kama jamaa atamuweka mtu yeyote mwnye kashfa then CCM itakua inajipalia makaa ya mawe tena RED HOT...........................


  NO MORE USWAHIBA HAPA KAZI TU......................Hope JK is sayin this ryt now.................
   
 19. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #19
  Nov 17, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mwanahalisi linapoamua kuandika udaku! Sioni chembe yenye ukweli hapa......
   
 20. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #20
  Nov 17, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Yote haya ni maandalizi ya kumusafisha Lowasa aweze kuwania urais 2015. Hivyo mbio za Chege za kutaka uwaziri zinaweza kuishia sakafuni lakini siyo za Lowasa. Iweje ni lazima Lowasa arudishwe kundini.
   
Loading...