MWANAHALISI katika mtandao

Mara baada ya Mdee kuwasilisha nyaraka, wajumbe wote walionekana kushangazwa na nyaraka za vikao vya CCM, zimeeleza taarifa za ndani ya kikao.

Baadhi ya nyaraka ambazo Mdee amewasilisha na kufanya wajumbe wabatuke nywele kichwani ni pamoja na Muhtasari wa Kikao cha Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam cha 20 Mei 2008; Kamati ya Usalama na Maadili ya CCM ya Mkoa; na Kamati ya Siasa ya Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni ya 15 Machi 2008.

Hii imenifurahisha .
 
Kweli tujitahidi kununua copy ili tuwa support hawa jamaa wawe strong kidogo maana najua wameyumba kidogo
 
Asanteni sana kwa habari hiyo nzuri.

Sisi tulioko mbali hatupati hard copy, naomba mtuwekee website yao ili angalau tulisome. Ile website yao ya zamani ina tole namba 0978 la May 21 2008
 
Hongereni sana Mwanahalisi,tafadhali mjitahidi ku-update ukurasa wenu pale itakapobidi.
 
Ni mojawapo ya magazeti machache sana hapa kwetu yanayoandika habari za uchunguzi tuwaunge mkono hawa jamaa ili waendelee kufichua maovu kwenye jamii yetu!
 
KARIBU MWANAHALISI ILA EPUKANA NA UDAKU
Nimefurahi kuliona MwanaHalisi mitaani. Ni ahueni kubwa kwa wapenda demokrasia ya kweli na uhuru wa vyombo vya habari. Hata sisi waandishi wa habari, tunaponea MwanaHalisi pale ambapo stori zetu zinakwama kwenye vyombo vyetu vinavyomilikiwa na mafisadi.

Nawapongeza MwanaHalisi, lakini wakati huohuo nampa tahadhari kaka yangu Kubenea kuwa anabeba dhamana kubwa, hivyo atumie zaidi waandishi waadilifu, shupavu, jasiri na waliosomea taaluma kama akina Ndimara Tegambwage na Ansbert Ngurumo. Akianza kuokoteza articles kutoka kwa makanjanja na watunga habari wa vijiweni, basi heshima ya MwanaHalisi itapotea haraka sana katika jamii.

Mfano halisi ni makala ya "Wazo Mbadala" ukurasa wa 4 wa toleo "mwali" la MwanaHalisi. Unapochapisha makala ya kumtuhumu kiongozi mwenye mvuto kwa wapiga kura wake, kama Dk. Mwakyembe, kwa kutumia vyanzo visivyo vya uhakika, ni rahisi kuwavunja moyo wapenda uwazi na ukweli wanaolipenda gazeti hili.

Mimi na waandishi wa habari wenzangu watatu wa Majira, Mwananchi na Uhuru tulikuwepo "uwanja wa siasa" mjini Kyela kumsikiliza Dk. Mwakyembe. Yaliyonukuliwa kwenye makala hayo, hakuyasema Dk. Mwakyembe. Aidha hata nukuu kutoka kwenye gazeti la Mwananchi toleo la tarehe 14 Januari, 2009, imeongezwa maneno kwa sababu ambazo huyo "mwandishi mwanafunzi wa SAUT" anazijua. Wananchi wengi wa mjini Kyela ambao ni wapenzi wa MwanaHalisi, kama mwanaharakati Mzee Benson Mwaikeke, wameshtushwa na kuanza kujiuliza kama MwanaHalisi nalo limeanza kutumiwa na mafisadi.

Wilayani Kyela, taarifa za Mbunge wao kuhujumiwa na mafisadi zimeenea sana kutokana na fedha nyingi kutumika kwenye uchaguzi wa viongozi wa jumuiya za CCM ili kuwaengua wale wote walioonekana kumuunga mkono Dk. Mwakyembe. Fedha za kampeni, kwa mujibu wa Diwani wa Kyela Mjini, Viski Mahenge, ambaye alipata kura nyingi kuwa Mwenyekiti wa Wazazi wa Wilaya, zilitoka kwa Karamagi na Lowassa kupitia kwa mfanyabiashara mmoja wa malori aishie Dar es Salaam kwa jina Elias Mwanjala.

Hivyo basi, si vibaya kukumbushana kuwa MwanaHalisi lina jina katika jamii. Jina hilo tulilee kwa uandishi mzuri na wa makini.
 
Lazaro

Kama Mwakyembe mwenyewe hakuzikanusha habari ambazo ni za uongo zilizoandikwa kwenye magazeti matatu ya kila siku, una mlaumu vipi Mwandishi wa Makala mwanafunzi wa SAUT ambaye amechambua habari hizo na kumshangaa Mwakyembe kutoa kauli hizo?

Ukitaka mjadala uwe mzuri tuwekee hapa habari zenyewe na makala ambayo umeizungumzia ili watu wengi zaidi wajadili

........ndiyohiyo
 
Ni mwanzo mzuri sana, kinachotakiwa ni ku- update website yenu mara kwa mara. Hii itatufanya sisi ambao hatuwezi kupata Hard copy kilisoma kupitia mtanadaoni.
 
Kwani kumekuwa na speciality gani kuhusu gazeti la mwana halisi?
Lina tofouti gani na magazeti mengine?
 
Lazaro

Kama Mwakyembe mwenyewe hakuzikanusha habari ambazo ni za uongo zilizoandikwa kwenye magazeti matatu ya kila siku, una mlaumu vipi Mwandishi wa Makala mwanafunzi wa SAUT ambaye amechambua habari hizo na kumshangaa Mwakyembe kutoa kauli hizo?

Ukitaka mjadala uwe mzuri tuwekee hapa habari zenyewe na makala ambayo umeizungumzia ili watu wengi zaidi wajadili

........ndiyohiyo

Ahsante mkuu,
Pengine hukunielewa. Mimi ni mwandishi na nilikuwepo kwenye huo mkutano! Hayo yaliyoandikwa na MwanaHalisi, hayakusemwa kwenye huo mkutano. Vilevile, hakuna gazeti lolote lililoripoti hayo yaliyonukuliwa na MwanaHalisi! Nukuu inayodaiwa kutoka kwenye stori ya gazeti la Mwananchi, vilevile ina utata, maana imeongezewa maneno ambayo hayakusemwa! Mimi nimetoa tahadhari tu, kuwa MwanaHalisi ni silaha nzuri kwa wapenda ukweli na demokrasia. Lisiharibu sifa hiyo kwa kuokoteza makala. Liwe makini!

Mzee Habarindiyohiyo unasema kwa nini Mwakyembe hajakanusha. Mimi siwezi kumwongelea, lakini kitaaluma kama mwandishi wa habari mkongwe, mtu anaweza kukanusha stori lakini siyo tahariri au commentary kama iliyoandikwa na huyo mwanafunzi kwenye MwanaHalisi!
 
Mzee Lazaros Mtindi, anayetaka kukuelewa kakuelewa. Tahadhari yako ni nzuri yenye nia njema na MwanaHalisi. Sasa tuangalie mbele.
 
Back
Top Bottom