Mwanahalisi: JK apora nyumba Dar, mwenyewe aja juu

Naamini hiyo nyumba ni kati ya zile zilizouzwa na serikali kwa wafanyakazi wake kwa hiyo kama kapora basi pamoja na kiwanja kingine. Lakini km ndio hivyo mbona wapo wengi hapa ndipo hoja ya Pr.Safari ya kurudisha nyumba zote zilizouzwa kwa watumishi wake na mahawara zao ina kuwa ya msingi si kikwete tuu wapo wengi waliojipendelea nyumba za serikali.
 
Nyumba ya Kikwete yazua utata


Rais Jakaya Kikwete anatuhumiwa kuchukuwa nyumba ya mkazi mmoja wa dare s Salaam na kuigeuza yake, MwanaHALISI limeelezwa.

Nyumba hiyo iko kiwanja namba 64, chenye eneo la futi mraba 23,239 kwenye makutano ya barabara ya Ursino na Migombani eneo la Mikocheni, Das es Salaam.

Hii ni nyumba ambamo wamekuwa wakikaa maofisa wa ngazi za juu serikalini, lakini warithi wanadai Kikwete ameibomoa, kijenga upya na ‘kujimilikisha.’

Nyumba hii, kwa mujibu wa warithi ni mali ya Amiral Abdulrasul Alarakhia Dewji na Yusufali Kassamali Remtula Parpia, ambao wote ni marehemu.

Mmoja wa warithi ni Amiral Yusufal Parpia ambaye anawakilishwa na kampuni ya mawakili ya H.H. Mtanga & Co Advocates ya Dar es Salaam.

Kwa kuwa nyumba hii imekuwa ikikaliwa na maofisa wa serikali, na kwa kuwa sechi kuhusi mmiliki wa kiwanja ya 22 Julai 2002 bado inaonyesha kuwa wamiliki ni wale wale, warithi wanapanga kuifikisha serikali mahakamani kwa kubomoa nyumba yao.

Tayari mawakili wa warithi wameitaarifu serikali kuhusu kusudio la kuifikisha mahakamani wakati wowote kujibu madai ya wateja wao………….

……….Hivi sasa Rais kikwete na familia yake wanaishi Ikulu, Magogoni. Lakini kabla ya kupata madaraka ya urais mwaka 2005, alikuwa akiishi katika nyumba hiyo kwa takriban miak 15 akiwa kama mtumishi wa serikali.

Hata sechi ya awali ya kiwanja hicho ya 22 Agosti 1982 iliwataja wamiliki kuwa hao hao, Dwewji na Parpoia.

Bali sechi nyingine ya wizara juu ya kiwanja hicho hicho ya 5 Novemba 2010 inasema, pamoja na mamobo mengine, kuwa imeshindikana kupata rekodi zinazoonyesha mmiliki wa kiwanja hicho……

Habari zaidi katika MwanaHalisi.


My Take:
Huu ni unyang’anyi wa hali ya juu. Hata hivyo hii habari iliwahi kutoka huko nyuma katika miezi ya awali ya utawala wa JK ingawa siyo katika details nyingi kama hivi.

Kwa mantiki hiyo basi hata waliouziwa nyumba za msajili wa majumba ambazo serikali ilizitaifisha
wamewapora wenye nyumba zao.
Mimi nafikiri kwamba baadhi ya taarifa zingine tusizikurupukie tu. Nyumba hiyo imetumiwa na maafisa wengi tu wa serikali sasa labda mwandishi atujulishe kama kwa kipindi chote hicho hao wahindi wakiipangisha serikali na leo wameporwa.La sivyo taarifa zingine ni za uzushi.
 
Back
Top Bottom