Mwanahalisi imeamua kupotosha kwa makusudi kauli ya mbunge Mwanaisha Mlenge au wametumwa?

Mfalme wa Genge

Senior Member
Mar 30, 2018
190
224
Mwanahalisi imeamua kupotosha kwa makusudi kauli ya Mbunge wa Viti Maalum Tanga Mwanaisha Mlenge. Mwanaisha ameshauri Serikali iwe na Ofisi moja tu ya Tathmini na Ufuatiliaji (Monitoring and Evaluation) badala ya kuwa na ofisi ndogo sita ambazo hazina nguvu kwa kuwa zipo chini ya Wizara mbalimbali mathalani Utumishi, TAMISEMI, Wizara ya Fedha nk.

Mwanahalisi kwa kupotosha inadai kwamba ushauri huo mzuri uliotolewa na mbunge huyo una lengo la kuundwa kwa chombo kitakachoiweka Serikali mfukoni na kitaipunguzia Serikali mamlaka.

Mwanaisha ametoa ushauri mzuri tena uliojikita kuisaidia Serikali na ametoa mifano ya Nchi zenye chombo hicho kimoja na jinsi zinavyofanya vizuri tofauti na kuwa na ofisi ndogo nyingi zinazofanya kazi moja. Hii itasaidia kuweka umakini katika ufuatiliaji na kutathimini changamoto za utekelezwaji wa miradi yetu ikiwemo udhibiti wa fedha za umma.

Kinachofanywa na wanahabari wenzetu hawa kinaondoa kabisa ile taswira na mapambano ya Uhuru wa Vyombo vya Habari.

Ni kweli tunataka uhuru wa vyombo vya habari lakini kwa upotoshaji huu hapana. Mwanahalisi hebu mjitafakari upya na mfanye kazi kwa maslahi ya umma badala ya wachache mnaowatumikia.

Mwandishi wa kujitegemea
Juma Rashid
 
Ungeweka kauli ya mbunge hapa iwe kwa mfumo wa audio au video na report ya upotoshaji ya MwanaHalisi, ingekuwa jambo la maana sana na ungeweza kutusaidia sana wachangiaji...

Lakini kwa hiki ulichofanya tunaweza kusema bila shaka yoyote kuwa tuhuma zako pia ni baseless, hazithibitiki na unataka uwateke wasiofikiria tu ili wakuunge mkono...
 
Kweli tupu
 
Back
Top Bottom