Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,920
- 31,161
- Thread starter
- #41
Na Saed Kubenea
MABILIONI ya shilingi za walipa kodi, ambayo Edward Lowassa alishinikiza yalipwe kwa kampuni ya kutengeneza matairi ya General Tyre (GT), yameteketea.
Hakuna anayekataa mabilioni ya fedha za walipa kodi yamepotea kwasababu ya uzembe.Tatizo ninaloliona hapa ni kwa serekali kuacha kuchunguza waliosababisha upotevu wa fedha za wananchi.Ikumbukwe fedha hizi zimeingizwa kama deni la serekali[taifa].
Taarifa kutoka kiwandani, mkoani Arusha zinasema kiwanda kimefungwa na haijulikani kitapata wapi na lini mtaji mwingine wa kukifufua.
Taarifa kutoka kiwanda kamwe huwezi kuzipata kwakuwa hakuna wa kukupa hizo taarifa,nashukuru umenisaidi kukiri kiwanda kimefungwa.
Lowassa, kabla ya kujiuzulu nafasi ya waziri mkuu, alishinikiza wizara ya fedha na mipango, chini ya Zakia Meghji, kutoa Sh. 10 bilioni kwa General Tyre ili "kulinda kiwanda hiki" kisifilisike.
Hapana huu ni uongo ambao tunapaswa kuukata mchana kweupe kwasababu fedha zilishatolewa mwaka 2005 wakati huo Zakia meghji alikuwa wizara ya maliasili na utalii.Mheshimiwa E Lowassa aliagiza General Tyre ipatiwe tena mkopo mwingine wa tsh 3.3 bilioni hiyo ilikuwa mwaka 2007,lakini Mheshimiwa Z maghji alikataa baada ya kubaini fedha za mwanzo zilitumika vibaya.
Hivi sasa suala hili liko mezani kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye General Tyre inaomba "akubali" kuwa fedha zilizotolewa zilitumika vizuri, kinyume cha taarifa ya maodita waliopitia hesabu za kampuni hiyo.
Hapana hakuna ukaguzi uliofanyika wa maana uliofanyika,TAC walitumwa kufanya ukaguzi lakini walishindwa kwasababu data nyingi za mahesabu ya General Tyre zimehifadhiwa kwenye Computers,wakati huo umeme ulikuwa umekatwa pia wafanyakazi wengi wa idara ya Accounts walishaacha kazi.Kilichofanyika TAC walichukua baadhi ya nyaraka tu na kuondoka.