MwanaHalisi acheni ubabaishaji

Wewe bana acha kutuletea longolongo hapa, mwandishi amesema kabisa ana barua za mawasiliano kati ya EL na na Bazil Mramba zinavyoonyesha jinsi mikakati ya dili ilivyokwenda pamoja na tarehe za 2007 wewe unaleta longolongo humu. Umetumwa umsafishe Lowassa nini?

Heshima Mzittokabwela,

Soma tena bandiko langu vizuri utaelewa ni kwanini nawaambia Mwanahalisi & Co waache ubabaishaji.Sijakataa kuwepo mawasiliano baina ya Lowassa na Mramba,kama kweli hayo mawasiliano yapo basi yatakuwa yanazungumzia mkopo mwingine wa u$ 3 milioni mzee.Mkopo wa u$ 10 milioni ulitoka mwaka 2005 na si 2007 kama mawanahalisi wanavyotaka kutudanganya.Mawasiliano baina ya Lowassa na Mramba yalifanyika wakati tayari mkopo wa tsh 13.2 zilishatolewa na kumalizika bila uzalishaji wa maana kufanyika.Pia Mramba alishaondoka wizara ya fedha na kuhamia wizara ya viwanda na biashara.

Mawasiliano baina ya Lowasa na Mramba yalihusu mkopo mwingine wa u$ 3 mil ambao kama ungetoka Bi Meghji angehusika kwasababu wakati huo alikuwa waziri wa fedha.
 
swala la msingi hapa si Shelukindo kafanya nini, wote wanaohusika na kuingiza taifa hasara wawajibishwe mara moja, sasa hayo mambo sijui ukimuona anashikia bango mafisadi halitusaidii, kama nae fisadi mshikie bango ukija na uthibitisho, dhambi ni dhambi tu.

Heshima kwako Nguvumali,

Kwanza unapaswa kuelewa kwamba Mheshimiwa W Shelukindo alikuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi.Kufa kwa kiwanda cha General Tyre kulichangiwa sana na uongozi mbovu.Ebu fikiria bodi ya General Tyre ilikuwa inakutana mara nne kila mwaka [vikao vya kawaida] halafu hamjadili financial position ya kampuni kwa miaka mitatu mfululizo,badala yake wanaidhinisha uuzwaji wa nyumba za kampuni,magari na magodown ya kampuni.

General Tyre inapata mkopo u$ 10 milioni bado hakuna kuuliza fedha zimetumikaje ?.Mkuu Nguvumali mimi siandiki habari za kusadikika kama MwanaHalisi,nilikuwa mfanyakazi tena division ya finance chochote ninachoandika si habari ya kuambiwa au kusikia ndio maana napinga habari za MwanaHalisi kwakuwa nakijua kilichokuwa kikifanyika.

Zipo habari za general Tyre si vyema kuanza kuelezea kila kitu upya nakuomba zitafute uzisome kwa makini utanielewa ninchokwambia
 
Wewe bana acha kutuletea longolongo hapa, mwandishi amesema kabisa ana barua za mawasiliano kati ya EL na na Bazil Mramba zinavyoonyesha jinsi mikakati ya dili ilivyokwenda pamoja na tarehe za 2007 wewe unaleta longolongo humu. Umetumwa umsafishe Lowassa nini?

Mzittokabwela

Kubenea hana lolote gazeti lake Lowasa lowasa ikiatokea jamaa leo katangualia mbele ya haki gazeti litakufa kwa kukosa cha kuandika.
 
Code:
Heshima Mzittokabwela,

Soma tena bandiko langu vizuri utaelewa ni kwanini nawaambia Mwanahalisi & Co waache ubabaishaji.Sijakataa kuwepo mawasiliano baina ya Lowassa na Mramba,kama kweli hayo mawasiliano yapo basi yatakuwa yanazungumzia mkopo mwingine wa u$ 3 milioni mzee.Mkopo wa u$ 10 milioni ulitoka mwaka 2005 na si 2007 kama mawanahalisi wanavyotaka kutudanganya.Mawasiliano baina ya Lowassa na Mramba yalifanyika wakati tayari mkopo wa tsh 13.2 zilishatolewa na kumalizika bila uzalishaji wa maana kufanyika.Pia Mramba alishaondoka wizara ya fedha na kuhamia wizara ya viwanda na biashara.

Mawasiliano baina ya Lowasa na Mramba yalihusu mkopo mwingine wa u$ 3 mil ambao kama ungetoka Bi Meghji angehusika kwasababu wakati huo alikuwa waziri wa fedha.
Code:
Wameripoti wizi....sisi ndo tunachokitaka. Waliiba mwaka jana, mwaka 1982 au mwaka huu wizi ni wizi tu. Hata kama wangecheza dili la kuiba shilingi 20 bado ni wizi tu. Sabuni unayotaka kumsafishia Lowassa HAINA POVU!
 
Code:
Mzittokabwela

Kubenea hana lolote gazeti lake Lowasa lowasa ikiatokea jamaa leo katangualia mbele ya haki gazeti litakufa kwa kukosa cha kuandika.
Code:
Kwahiyo kama Lowassa kafanya madudu wasiandikwe? Nenda kamuulize Kubenea nakala wanazouza ndo utajua kama EL akifa wataendelea kuuza au . Mwanahalisi ni watu wa kupongezwa kwa sababu wanafichua UJAMBAZI wa Lowassa na RA, na kwa taarifa yako wanamsema Muungwana kwa mlango wa nyuma hawawezi kumlipua sasa sababu ya katiba yetu inampa uungu Rais aliyepo madarakani lakini huwezi kumchafua EL na RA ukasema Muungwana ni safi. Wote ni majambazi tu. Lidumu Mwanahalisi.....
 
Mzittokabwela

Kubenea hana lolote gazeti lake Lowasa lowasa ikiatokea jamaa leo katangualia mbele ya haki gazeti litakufa kwa kukosa cha kuandika.
toa sababu kwanini Lowasa sio habari nnchi hii, kwanini Lowasa akikwapua mali ya UMMA ASISEMWE ? SI SWALA LA KUBENEA KUMWANDIKA, HOJA KILE KINACHOANDIKWA KINA MANTINKI KIASI GANI.
 
Kwahiyo kama Lowassa kafanya madudu wasiandikwe? Nenda kamuulize Kubenea nakala wanazouza ndo utajua kama EL akifa wataendelea kuuza au . Mwanahalisi ni watu wa kupongezwa kwa sababu wanafichua UJAMBAZI wa Lowassa na RA, na kwa taarifa yako wanamsema Muungwana kwa mlango wa nyuma hawawezi kumlipua sasa sababu ya katiba yetu inampa uungu Rais aliyepo madarakani lakini huwezi kumchafua EL na RA ukasema Muungwana ni safi. Wote ni majambazi tu. Lidumu Mwanahalisi.....

Heshima kwako Mzittokabwela,

Sijawahi kumtetea Lowassa na wala mimi si mtetezi wa mafisadi.Lowassa ana dhambi zake nyingi ambazo kama nchi yetu tungekuwa makini tungeshamsahau siku nyingi lakini tusipende kuwa washabiki hata kwa mambo ambayo si ya kweli.Ukijaribu kutafuata mabandiko yangu kuhusiana na RICHMOND utabaini mara moja nilivyomstari wa mbele kuwabonda kina Lowassa & Co.
 
Wameripoti wizi....sisi ndo tunachokitaka. Waliiba mwaka jana, mwaka 1982 au mwaka huu wizi ni wizi tu. Hata kama wangecheza dili la kuiba shilingi 20 bado ni wizi tu. Sabuni unayotaka kumsafishia Lowassa HAINA POVU!

Heshima kwako mzittokabwela,

Inaonekana unapenda ligi ya ubishi hutaki kuelewa kabisa sijui unataka nikupe majibu ya aina gani ?.
 
Code:
Heshima kwako mzittokabwela,

Inaonekana unapenda ligi ya ubishi hutaki kuelewa kabisa sijui unataka nikupe majibu ya aina gani ?.
Code:
tatizo sio ligi, tatizo ni wewe kutaka nikubaliane na hicho unachokitaka. Watu wametajwa kwa majina, documents pamoja na kumbukumbu namba zimeandikwa, tarehe zimetajwa...sasa wewe unakuja tu humu na maelezo mepesi unataka watu waamini. Toa vielelezo mkuu acha kupiga porojo. Scan hiyo barua ya mwaka 2005 iatach hapa wenye akili waijadili ndipo tutawaona mwanahalisi hawana maana, lakini ukija na mapambio ya New Habari cooperation tegemea kubishiwa!
 
Na Saed Kubenea

MABILIONI ya shilingi za walipa kodi, ambayo Edward Lowassa alishinikiza yalipwe kwa kampuni ya kutengeneza matairi ya General Tyre (GT), yameteketea.
Taarifa kutoka kiwandani, mkoani Arusha zinasema kiwanda kimefungwa na haijulikani kitapata wapi na lini mtaji mwingine wa kukifufua.
Lowassa, kabla ya kujiuzulu nafasi ya waziri mkuu, alishinikiza wizara ya fedha na mipango, chini ya Zakia Meghji, kutoa Sh. 10 bilioni kwa General Tyre ili “kulinda kiwanda hiki” kisifilisike.
Hivi sasa suala hili liko mezani kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye General Tyre inaomba “akubali” kuwa fedha zilizotolewa zilitumika vizuri, kinyume cha taarifa ya maodita waliopitia hesabu za kampuni hiyo.
General Tyre inaomba pia serikali iongeze fedha nyingine, juu ya mabilioni ambayo matumizi yake hadi sasa bado ni utata mtupu.
Kwa mujibu wa barua ya Katibu wa Lowassa wakati huo, B. Olekuyan kwa Katibu wa Meghji, Kumb. Na. PM/P/I/567/40 na iliyobeba kichwa cha maneno, “General Tyre East Africa LTD Arusha,”
Lowassa aliagiza kama ifuatavyo:
“Tuliishaliamulia suala hili kwamba wapewe government guarantee kulinda kiwanda hiki, mkopo wa awali na ajira za Watanzania. Kama WF (waziri wa fedha) ana maoni tofauti alete kwenye kikao. Vinginevyo atekeleze kabla ya tarehe 15/7/2007.”
Katika barua hiyo, ambayo katibu wa Lowassa alikuwa anapeleka pia kwa waziri wa viwanda biashara na masoko, wakati huo Basi Mramba, anaelekeza nakala yake ipelekwe kwa mawaziri wote wanaohusika ili wajue msimamo wa waziri mkuu.
Taarifa zinasema Mramba na Lowassa waliafikiana serikali itoa fedha kwa GT, kwa mujibu wa barua ya 28 Juni 2007 iliyotoka kwa Mramba kwenda kwa Meghji.
Naye Mramba anajenga hoja ya kutolewa kwa fedha hizo haraka na bila masharti. Anaonya kwamba kuchelewa kutekeleza agizo la Lowassa kutasababisha kiwanda kufungwa.
“Ushauri wangu kwako (Meghji) ni kwamba ujitahidi kuweka dhamana kwa ajili ya fedha hizo za NSSF haraka iwezekanavyo. Kama fedha zikikosekana, kiwanda hicho chaweza kufungwa,” inasema barua hiyo ya Mramba kwa Meghji.
Hata hivyo, pamoja na kutolewa kwa mabilioni hayo ya shilingi, kiwanda hicho kimefungwa mwaka jana.
Aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya kiwanda hicho, William Shelukindo, mbunge wa Bumbuli (CCM), amethibitishia gazeti hili kuwa kiwanda kimefungwa pamoja na mabilioni ya shilingi yaliyomwagwa humo.
Hata hivyo mabilioni hayo ya shilingi yameghubikwa na utata. Nyaraka ambazo gazeti hili limepata zinaonyesha kuwa siyo fedha zote zilizopelekwa kiwandani Arusha.
Nyaraka zinaonyesha kuwa Sh. 1 bilioni zililipwa kwa kampuni ya ukaguzi ya DAI Consulting kutoka nchini Afrika Kusini. Kampuni ya DAI ilipewa fedha hizo na NSSF kama gharama za ushauri kwa GT.
Lakini GT inalalamika, katika barua yake kwa Pinda, kuwa malipo ya Sh. 1 bilioni zilizotolewa kwa DAI Consulting ni fedha nyingi ikilinganishwa na kazi iliyofanyika.
Meneja Mkuu wa GT, Deven Lohani, raia wa Nepal, katika barua yake ya 17 Agosti 2009 kwa Waziri Mkuu Pinda, anaorodhesha malalamiko kuhusu usahihi wa matumizi ya mabilioni hayo.
Hata hivyo, kampuni ya matairi inasema haikuwa na njia nyingine ya kupinga malipo hayo kwa kuwa hiyo ilikuwa sehemu ya mkataba wa kupewa fedha hizo na NSSF. Kampuni ya DAI iliteuliwa na NSSF, inasema GT.
“…Ni muhimu kufahamu kwamba kampuni ya DAI Consulting ilipendekezwa kwetu na NSSF. Katika kipindi hicho GT ilikuwa na matatizo makubwa ya kifedha na ililazimika kukubali sharti hilo,” inasema sehemu ya barua ya GT kwenda kwa Pinda.
Meneja Lohani ameeleza kuwa tatizo kubwa lilikuwa ni kiasi hicho kutolewa kwa mafungu-mafungu na si kwa jumla kama ilivyokuwa ikitarajiwa.
Shellukindo, hata hivyo, aliliambia MwanaHALISI kuwa kwa kadri anavyofahamu, nyingi ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya kuifufua GT, zilitumika kwa ajili ya kulipa madeni mbalimbali yaliyokuwa yakiikabili kampuni hiyo.
“Siwezi kusema kwa hakika ni kiasi gani kilitolewa na serikali katika kuifufua GT. Nilicho na uhakika nacho ni kuwa fedha nyingi zilitumika kulipa madeni ya kampuni,” alisema Shellukindo.
Kwa kauli ya Shellukindo, Sh. 10 bilioni zilizotolewa na NSSF kwa udhamini wa serikali hazikutumika kufanya kazi iliyokusudiwa.

Source: Mwanahalisi
 
Ufisadi wafilisi General Tyre

na Halfani Lihundi, Arusha

amka2.gif
IMEBANIKA kuwa, kufilisika kwa Kiwanda cha kuzalisha magurudumu ya magari cha General Tyre, mjini hapa, kumesababishwa na ufisadi wa matumizi mabaya ya sh bilioni 10, zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kukiendesha.
Akizungumza na wafanyakazi kiwandani hapo jana, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Shabani Mjaka, alisema lengo la serikali kutoa pesa hizo ilikuwa ni kufufua kiwanda, lakini wajanja wamezitumia kwa matumizi tofauti.
Mjaka alisema mwaka 2005, kiwanda kilikuwa kinadaiwa sh bilioni tano ambapo serikali ilitoa sh bilioni 10 kwa ajili ya kulipia madeni, na zilizobaki kukiwezesha kuendelea na kazi, lakini kilichofanyika ni kinyume.
Alisema uongozi wa kiwanda hicho, ulitumia dola za Kimarekani milioni moja kuilipa Kampuni ya Deta iliyokuwa kwenye mpangilio wa malipo hayo na kiasi cha sh bilioni 3.4, walisema wangezitumia kununulia malighafi ambazo hazina vielelezo vya manunuzi na havijulikani vilipo hadi sasa.
Mjaka alisema, uongozi huo pia umeshindwa kutoa maelezo ya matumizi ya dola za Kimarekani 368, wanazodai zimetumika kwa matumizi ya kiwanda, lakini hazina maelezo ya kimsingi na wala hazieleweki zilipo kwani serikali haina taarifa.
Alisema uongozi uliokuwepo wakati huo ulichangia kiasi kikubwa kukifilisi kiwanda hicho kwani lengo halikutekelezwa kama ilivyokusudiwa na mbia aliyekuwepo mwanzo.
Kwamba baada ya kuharibu, aliondoka na sasa serikali inatafuta mbia wingine ili kukifufua kiwanda hicho.
Dk. Mjaka alisema serikali imeahidi kuwa Agosti 5, mwaka huu, itawalipa wafanyakazi wote zaidi ya 300 wa kiwanda hicho kiinua mgongo pamoja na malimbikizo yao yote.
Alitangaza kuwa kiwanda kimesimamisha rasmi uzalishaji na kwamba atakapopatikana mbia mpya, ajira zitatangazwa upya, lakini kwa sasa mkataba wa kiwanda na wafanyakazi hao umekwisha.
Akielezea kuhusu umakini wa serikali kama itaweza kufanya makosa kama yaliyotokea kwa mbia mwingine na kupata hasara kama hiyo, alisema serikali imejifunza, hivyo itakuwa makini kuzisimamia pesa zitakazotolewa kwenye makampuni na kuhakikisha zinatumika kwa matumizi husika.
Kwa upande wao, wafanyakazi wameitaka serikali kuwachukulia hatua za kisheria viongozi waliofanya ubadhirifu huo, kwani pesa za serikali haziwezi kupotea kwenye mazingira ya kutatanisha, kisha na wahusika wasichukuliwe hatua za kisheria hali itakayosababisha tabia hiyo kuendelea sehemu zingine.
Walisema mara kadhaa, imeonekana watu wachache wamekuwa wakitumia fedha za umma kwa manufaa yao binafsi na serikali imekuwa ikiwafumbia macho.

Source Tanzania Daima dated 01/08/2009.

Imekuwa ni vigumu kupata nakala za nyuma za magazeti ya mwananchi na Nipashe amabyo nayo yalimnukuu vizuri naibu katibu mkuu wa wizara ya viwanda biashara na masoko Dr Mjaka.

Heshima kwenu Mzittokabwela,Fact1 na wengine wote mnaopinga kwamba General Tyre ilipata mkopo mwaka 2005.

Ni vizuri kwanza kuzingatia muda katika suala la mkopo wa General Tyre kutoa hukumu nani alikuwa nani badala ya kukimbilia kupakazia watu tuhumu ambazo hawakuhusika kwa hali yoyote.
 
Mzittokabwela,Nguvumali na Fact1 vipi mbona mmeingia mitini,Kubenea ajipange upya hii ni safari ya tatu MwanaHalisi linakosolewa, badala ya kutumia nguvu kubwa kutetea uzembe mwambieni ajipange upya.

Nakumbuka toleo lililopita walikuja na habari za Mbeya (Kyela) ambazo wakuu wa huko walizikosoa vibaya sana nikadhani Kubenea atajipanga vyema lakini kwa msahangao wa wengi bado anaendeleza habari za kuokoteza.
 
mkuu ngongo mie nilishaacha kulisoma gazeti hili muda mrefu. Nadhani ujasiri ni kuachana na media zisizotenda haki ktk kuhabarisha. Shukrani mlongu wangu kwa details za kutosha juu ya hili la mwanahalisi. Wajipange, wawarudie wananchi ili imani irejee na tujifunze vitu hali toka mwanahalisi na si vitu visivyo halisi

mzittokabwela,nguvumali na fact1 vipi mbona mmeingia mitini,kubenea ajipange upya hii ni safari ya tatu mwanahalisi linakosolewa, badala ya kutumia nguvu kubwa kutetea uzembe mwambieni ajipange upya.

Nakumbuka toleo lililopita walikuja na habari za mbeya (kyela) ambazo wakuu wa huko walizikosoa vibaya sana nikadhani kubenea atajipanga vyema lakini kwa msahangao wa wengi bado anaendeleza habari za kuokoteza.
 
janjaweed na nanu. Wote story yenu ni 'Mwanahalisi huwa ni personal attacker tu'
Who has been personally attacked bila reason?
1. Lowassa - Richmond
2. Rostam - Dowans
3. Balali - EPA
4. Idrisa - Dowans and 600million house
5. JK - mismanagement of state
6. Karamagi - Buswagi na Ticts
7. Chenge - Radah, plane, contracts
8. etc
Aren't these issues of national interest? Show they not mention waovu eti Janjaweed na Nanu watasema ni personal attacts.
You are being shallow minded guys. I thought you were intelligent enough to see that the paper is only exposing ufisadi na mafisadi. Which side are you on?
Pity Tz. With such folks, sijui kama tutaenda.
 
Tatizo ni kwamba
vyanzo vingi vya habari vinaamua kwa makusudi kutotoa ushirikiano halafu wakishaandikwa ndo wanakuja kukanusha. Naamini wahusika walitafutwa lakini hawakutoa ushirikiano wakidhani habari haitatoka, lakini wanasahau kwamba ignorance ya Law haina excuse ambapo principle hii inaaply ktk sehemu nyingi za jamii
 
janjaweed na nanu. Wote story yenu ni 'Mwanahalisi huwa ni personal attacker tu'
Who has been personally attacked bila reason?
1. Lowassa - Richmond
2. Rostam - Dowans
3. Balali - EPA
4. Idrisa - Dowans and 600million house
5. JK - mismanagement of state
6. Karamagi - Buswagi na Ticts
7. Chenge - Radah, plane, contracts
8. etc
Aren't these issues of national interest? Show they not mention waovu eti Janjaweed na Nanu watasema ni personal attacts.
You are being shallow minded guys. I thought you were intelligent enough to see that the paper is only exposing ufisadi na mafisadi. Which side are you on?
Pity Tz. With such folks, sijui kama tutaenda.
You beat me to it ndugu...... the tz learned community is a stranger lot than the strangiest you have ever seen!!
 
Back
Top Bottom