Mwanahabari Jerry Muro ahoji uhalali wa tume ya Mhe. Nape Nnauye

mshumbue-soi

JF-Expert Member
Aug 28, 2013
1,842
1,148
JERRY C. MURO _____ ANAANDIKA:-

Moja ya maswali ya Tasnia kwa Mhe waziri ni hili la ukakasi wa Members wake wa kamati

1. Balile ni mhariri mtendaji wa Jamhuri gazeti ambalo leo limeweka kilichopo je huyu atakuwa na uhalali wa kuhojiana na Mhe Makonda?

2. Jesse Kwayu ni mhariri kiongozi wa Gazeti la Nipashe ambalo mmiliki wake ni Mwenyekiti wa MOAT ambae hana mahusiano mazuri na Mhe makonda, je huyu Jesse nae ana uhalali wa kuhojiana na makonda?

3. Iweje aunde kamati ambayo idadi kubwa ya wajumbe wana utaalamu wa taaluma ya print media yaani magazeti, wakati tukio limetokea kwenye kituo cha radio na Luninga? Hapa kuna masuala ya broadcasting ethics na print ethics, je kanuni za kuingia news room ndio hizo za kuingia studio ya tv au chumba cha kurushia matangazo tx?

4. Mjumbe kutoka tcra anasimama kama regulator au kama nani?kwani hilo jambo linahusiana na regulator ?

5. Suala la uvamizi hilo ni suala linalohusiana na jinai haoni haja ya kuongeza wajumbe kama polisi au usalama wa taifa?

6. Makonda anasimamiw na ofisi ya Rais-TAMISEMI wakuu wake wana taarifa za mfanyakazi wao kuhojiwa na Kamati?

7. Kituo kinatchotajwa kuvamiwa ni kituo binafsi, na tume ina watu wengi kutoka vyombo binafsi ambao kimaslahi wana crush of interest na serikali katika baadhi ya mambo je wajumbe watakuwa huru kumuhoji Mhe makonda bila mihemuko?

8. Tayari Mhe waziri Nape ameonyesha kukerwa na tukio hilo, ameshatoa muhemko wake, je anapounda tune ambayo iko chini ya msaidizi wake kikazi haoni hapo kuna suala litaleta ukakasi?

Baada ya maswali ni Ushauri

1. Mhe waziri haoni hili jambo angelipeleka kwenye mamlaka zingine mfano jeshi la polisi, au angelipeleka TCRA au baraza la habari na kuwaomba wao kama watu huru walifanyie kazi kwa kuwa hawana mwingiliano wa moja kwa moja na hili suala?

2. Mhe Nape haoni kuna haja ya kuongeza idadi ya wajumbe huru kutoa vyuo vya kitaalumu mfano SAUT?IJMC?
Pia ofisi ya mwanasheria mkuu?

Najua hadidu rejea kuu ya kamati ni kuhoji, ila likiwekwa vizuri ili kupata mahojiano mazuri yenye maswali magumu huenda kamati ikawa BORA zaidi.

Ni maoni yangu mimi kama mwanahabari ambae napenda kujua zaidi katika sakata hili.
Jerry Cornel Muro
C & P

Je waoni yako?
 
1. Makonda kwa nini ulienda clouds kudai story ambayo Si yako? Hujasomea journalism, sio employee wa Clouds na Wala sio mmiliki. Tabia uliyoionyesha Ni ya kuidhalilisha Serikali kwa kujihusisha na story za uongo dhidi ya Gwajima ukiwa kama RC, kiongozi Serikalini. Pamoja na kazi nzuri uliyoianzisha ya vita vya dawa za kulevya, ulichofanya hakikubaliki.

2. Nape Kesi ya RC na Clouds haikupaswa kuingiliwa bila facts. Ukiwa kama kiongozi wa Serikali ulipaswa uwe upande wa Serikali hata kama umekosea, that is what we call collective responsibility. Umeibuka na kumlaani RC kanajisi uhuru wa Habari. Then una unda Kamati ya uchunguzi ili ibariki tamko Lako la kulaani kabla ya kusikiliza upande wa pili. KU bula wewe si Rais, VP AU Pm. Mteule wa Rais huchunguzwa na wateule wa Rais sio mtu ambaye Yuko chini yake kicheo. Uliowateua wako chini kicheo kuliko wanaemchunguza. Haiwagi hivyo. Pia unaonekana umetoka upande wa Serikali ukahamia upande wa pili. Si sawa .

3. Clouds, its unprofessional kumpa story source aweze edit story yake unless ni tangazo. I have never seen a journalist showing her or his story to a source before publishing it or air it. This is amazing. Ni vema mkaajiri professionals wawasaidie. Mambo ya kumwambia RC kuwa mna story negative ya Gwajima inaonyesha kuna kitu mlipokea kutoka kwa RC na ndio maana mlimshirikisha. Angejuaje mna story ya aina hiyo? Si sawa. Jiangalieni upya. mlikosea.

4. Kamati ya Nape haikuwa na sifa ya kumhoji RC. Wote ni wateule wa Waziri wakati Makonda ni mteule wa Rais. Pili mwenyekiti ni Mkurugenzi kwenye Wizara anayoiongoza Nape na Katibu wa Kamati ni Mmiliki wa Gazeti la Jamhuri ambalo toleo lake la jana lilikuwa na 8 pages of a negative story of the RC. Hamna sifa za kufanya uchunguzi kwani mtaelemea kwa mawazo ya aliyewateua kama alivyosema jumatatu kwa ku condemn kitendo cha RC.

Tumejifunza. Hii ni Semina elekezi kwa viongozi wa Serikali kuacha mihemuko wakati wa crisis, you have to work as a team. Media should adhere to the journalism athics and weledi. Si sawa source ajue story yako au kipindi chako kabla ya kutangaza hatotaka story ya upande wa adui. That is normal. Walipeni mishahara waandishi ili wasijiingize kwenye kuombaomba kwa source. Kuna media house kubwa tu Watu hawajalipwa mishahara tangu Desemba mwaka jana. Nape ili uwatendee haki waandishi ni vema ukapita kwenye hivyo vyombo kuwakumbusha wamiliki Juu ya wajibu wao wa kuwalipa mishahara waandishi kwa wakati

Waandishi lets be realistic matatizo Haya yameletwa na nyinyi wenyewe kwa kuendekeza HABARI za mshiko. Tubadilike. Tusijidanganye. Wabaneni wamiliki wawalipe ni haki yenu kwa mujibu wa Sheria.
 
Hivi kwa nini DG wa baraza asifumbe macho na kutufungie mjadalah huu? How much does it take to print one certificate?
 
Muro anajiunga kwenye mbio za 42-km marathon wakati wenziwe wame-cover 30 km??
 
Back
Top Bottom