Mwanahabari Erick Kabendera akamatwa na Polisi nyumbani kwake; yadaiwa anaendelea na Mahojiano

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,991
12,343
Mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera anadaiwa kuvamiwa na 'watu wasiojulikana' nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es salaam baada ya watu kadhaa wakiwa na magari kuvamia na kuzingira nyumba na kuzuia watu kuingia.

Namba ya gari lililomchukua imetajwa ni T746DFS.

FB_IMG_1564420148189.jpg
Erick Kabendera, a Tanzanian journalist, has been abducted from his home in Mbweni, Dar es Salaam. He told one of his colleagues of a high presence of security vehicle and unknown people around his house shortly before he disappeared to never be reached by phone this evening.

UPDATES:
Baada ya watu hao kuzingira nyumba huku wakionekana kuwa na nia ovu, yeye na familia walifunga milango. Wananchi akiwemo M/kiti wa mtaa walipofika na kuhoji wao ni nani walisema wao ni Polisi (hawakuwa na sare wala gari la polisi). Sasa inadaiwa wamekwenda naye kituo cha Polisi Oysterbay.

UPDATES: 2100HRS
Jeshi la Polisi inadaiwa linaendelea kumhoji Kabendera kuhusu mambo ambayo hayajawekwa wazi na wala hawajasema anahojiwa kituo gani. Taarifa hii ni kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kinondoni.

Kabendera alichukuliwa na watu 6 waliokuwa na silaha na inadaiwa simu yake ilikuwa blocked tangu. Jumamosi huku Mtandao wa Vodacom wakimwambia wamefanya hivyo kwa maagizo ya TCRA. Wakimtaka ajisalimishe Voda Shop

45EB6BDD-9C90-42BF-BE60-7E63C8FBEAB6.jpeg

Wananchi waliokusanyika nyumbani kwa Erick walijitahidi kuwazuia watu hao na kuwataka wajitambulishe. Pamoja na jitihada za wananchi kutaka kupiga picha, simu zao zimechukuliwa kwa kudaiwa kuwa hawaruhusiwi kupiga picha.

05:20am - July 30, 2019
Chanzo kinabainisha Erick alikamatwa na Maafisa wa Polisi waliotokea Kituo cha Polisi Mbweni lakini njiani inadaiwa magari yalibadilishwa na bado hakuna taarifa rasmi za kituo gani anahojiwa.

10:20am - July 30, 2019
IGP Simon Sirro amethibitisha Kabendera anashikiliwa na Jeshi la Polisi na kuwa Polisi kupitia Kamanda Mambosasa wataongea na Vyombo vya Habari ifikapo saa 7 mchana

10:25am - July 30, 2019
TCRA wamekanusha kuhusika kwa namna yoyote na uzimwaji/ukatwaji wa mawasiliano ya simu ya Kabendera na kusisitiza kuwa wao wanahusika na kudhibiti simu zisizotakiwa (fake)

10:28am - July 30, 2019
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amesema suala la Erick Kabendera kuhojiwa ni la Polisi na si la Serikali

UPDATES1400HRS
- Erick Kabendera anashikiliwa na Polisi, anahojiwa kuhusu Uraia wake.

ZAIDI, SOMA:
VISA DHIDI YA WANAHABARI WENGINE WA TANZANIA:
 
MWANDISHI wa habari za kiuchunguzi, Erick Kabendera, amevamiwa na “watu wasiojulikana,” nyumbani kwake Mbweni, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kabendera, leo jioni watu kadhaa wakiwa na magari, walivamia nyumbani kwake na kuzingira nyumba hiyo na kuzuia mtu yeyote kuingia.

Anasema, kabla ya hapo, simu zake zote zilifungwa; na alipopiga simu Vodacom aliambiwa kuwa hayo ndio maelekezo waliyopewa na Mamlaka ya Mawasiliano ya taifa (TCRA).

Naye mtoa taarifa mmoja ameliambia MwanaHALISI ONLINE, kwamba “…inawezekana wamemchukua tayari; sababu hata simu za ndani ya nyumba hazipokelewi.”

Kabendera ni mmoja wa waandishi wa habari nchini anayeandikia magazeti mbalimbali, likiwamo gazeti la Africa Confidential linalochapishwa Uingereza.

432BA719-183E-4268-9C7D-F150CF31E781-620x330.jpeg
 
Back
Top Bottom