Mwanafunzi wa UDSM akamatwa kwa kusambaza taarifa na Takwimu za uongo za Covid-19 WhatsApp

Wamsamehe tu,hii sheria huko mbeleni inabidi wake waifute,Uhuru wa kutoa maoni Hapa unakiukwa,kila mtu anajua takwimu rasmi Ni zipi na kila mtu anafuatilia taarifa rasmi kwa umakini Sana,
Hakuna Uhuru wa namna hii Chief

Mwenye kujua Takwimu Sahihi ni Serikali ikishirikiana na Wizara husika
Mtu Binafsi hawezi kujua usahihi mpaka atakapoambiwa na Dola

Lau tutaruhusu hili
Madhara yake ni Makubwa sana katika Jamii

Tuwe makini
Na tuiunge Mkono Serikali yetu
Mola Ibariki Tz
Mola Ibariki Afrika
Mola Ibariki Dunia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taarifa sahihi ni ipi? Askari wamejuaje kuwa hio taarifa sio sahihi? Je, ilileta madhara gani kwa jamii?
Acha uzembe wa kuwaza na ushabiki. Serikali inatoa taarifa zake kila mara kupitia wizara ya afya na PM, sasa hizo za kwake ataenda thibitisha mahakamani na ataonesha makaburi na vyeti vya kifo kwa hao watu wanne vikiwa na sababu ya kifo kuwa korona
 
Suley2019,
Watanzania kwa nini tunatafuta matatizo kwa lazima?

sasa akiambiwa hao watu 230 awataje atawataja?

binafsi ndugu na jamaa zangu wote ambao nawafahamu sina mtu yeyote mwenye dalili za #covid19.

kama na wewe watu waliokuzunguka hakuna mwenye #covid19 unayemjua kwa uhakika basi usisikilize propaganda za kwenye vijiwe vyakahawa
 
mambo madogo madogo kama haya yanaongeza stress kwa jamii, mitandao skuiz kila mtu anajua kumi shika 1, mwanafunzi uyo mtoto wa 23 utanfanya nini mahakamni
 
Hizi nguvu za kupambana na hawa watu minor tungezielekeza kwenye kupambana na Covid - 19
 
Back
Top Bottom