Mwanafunzi wa shule ya msingi abakwa na wavulana 3 wa sekondari

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,492
9,266

Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mbugani Geita mwenye umri wa miaka 14, amedai kubakwa na wanafunzi watatu (3) ambao wawili wanasoma Shule ya Sekondari Nyanza na mmoja Shule ya Sekondari Geita wote ni wa kidato cha pili wakikadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 14-15.

Anayedaiwa kubakwa amesema Wanafunzi hao walikutana nae shuleni kwao wakati wa mapumziko na kumtaka awasindikize nyumbani ndipo walipofika kwenye chumba wanachoishi (GHETO) na kumsukuma ndani kisha kumziba mdomo na kuanza kumbaka mmoja baada ya mwingine.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Geita, Dismas Kisusi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nakusema kati ya watuhumiwa 3 mmoja ndiye anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano zaidi na pindi upelelezi utakapokamilika hatua za Kimahakama zitafuatwa.
 
hao watoto wapuuzi sana. pia binti nae unawasindikizaje jamaa wapuuzi tena ghetto
 
Mwanamke anaweza kulawitiwa pia. Hao hawajafikisha 18 years hivyo nahisi hawatapigwa miaka 30
 
Back
Top Bottom