Mwanafunzi wa sekondari apunguziwe mzigo wa masomo kwa mtindo huu

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,166
12,649
Naonelea History na Civics ziwe hazina mitihani wala notisi. Zifundishwe kwa njia ya masimulizi. Tena ili kurahisisha ugumu masomo haya yasimuliwe kwa lugha ya Kiswahili.

Pia mtaala wa kiswahili upunguzwe. Mambo ya mofimu na kuchambua sentensi yatolewe na ikiwezekana kidato cha pili iwe mwisho kukisoma, anayetaka anaweza kuendelea nacho akifika kidato cha tano.

Mambo ya mofimu na vitenzi hayasaidii kitu maishani.

Naomba tujadili hili na nyinyi wakuu sana mtoe maoni yenu jinsi ya kumpunguzia mzigo mwanafunzi wa sekondari.
 
Nilidhani vibaraka wa mabeberu wanaotuharibia nchi waliishilia pale Mr Mzungu alipotoroka na kukimbilia Belgium, kumbe bado wafuasi wake wapo still!? Hii ni hatari na theluthi.
 
... hizo history na civics hazitakuwa na mitihani au mitihani itajibiwa kwa masimulizi pia?
 
  • Kicheko
Reactions: BRB
Umeweka masomo ambayo hayatusaidii chochote Maisha ni sawa!
Ila pia ningependa kabla hatujaendela uweke list ya masomo yanayotusaidia na uweke hizo faida pia japo kwa uchache tu.
Biolojia inatusaidia kujua mwili na afya zetu, fizikia ndiyo msingi wa ufundi, hesabu tunatumia kila siku. Chemistry, tunatumia kila siku kemikali jiografi na kiingereza ni muhimu sana.
 
Naonelea History na Civics ziwe hazina mitihani wala notisi. Zifundishwe kwa njia ya masimulizi. Tena ili kurahisisha ugumu masomo haya yasimuliwe kwa lugha ya Kiswahili.

Pia mtaala wa kiswahili upunguzwe. Mambo ya mofimu na kuchambua sentensi yatolewe na ikiwezekana kidato cha pili iwe mwisho kukisoma, anayetaka anaweza kuendelea nacho akifika kidato cha tano.

Mambo ya mofimu na vitenzi hayasaidii kitu maishani.

Naomba tujadili hili na nyinyi wakuu sana mtoe maoni yenu jinsi ya kumpunguzia mzigo mwanafunzi wa sekondari.
Vijana mnataka vitu rahisi rahisi tu, mbona sisi tulisoma na tukasajili na masomo mengine na kuyafanyia mitihani? Nadhani tatizo la vijana siku hizi ni kuwa na mambo mengi kichwani, wanataka kuchanganya shule na mambo mengineyo. Hakuna hasara kusoma Civics na. Historia, yanasaidia kuongeza maarifa na ufahamu.

Vv
 
Biolojia inatusaidia kujua mwili na afya zetu, fizikia ndiyo msingi wa ufundi, hesabu tunatumia kila siku. Chemistry, tunatumia kila siku kemikali jiografi na kiingereza ni muhimu sana.

Vipi kuhusu historia inayotusaidia kutambua maendeleo/mabadiliko yanayotokea baada ya mwaka , karne baada ya Karne katika hayo masomo tajwa hapo juu?

,,,,Mfano historia kuhusu namna ya kupambana na magonjwa mfano wa corona yalitokea karne zilizopita.
Vipi hiyo historia haitusaidii?
 
Vijana mnataka vitu rahisi rahisi tu, mbona sisi tulisoma na tukasajili na masomo mengine na kuyafanyia mitihani? Nadhani tatizo la vijana siku hizi ni kuwa na mambo mengi kichwani, wanataka kuchanganya shule na mambo mengineyo. Hakuna hasara kusoma Civics na. Historia, yanasaidia kuongeza maarifa na ufahamu.

Vv
Zama zimebadilika. Elimu ya kukariri watu kwenye historia, kufaulu mtihani na kupatiwa kazi haisaidii tena. Ni bora kupunguza hayo mambo, tena bora wangeacha masomo ya biashara yanayomfundisha mtu vitu practical.
 
Masoma yanayohitajika kwa Sasa ni

1.mathematics
2.physics
3.geograph
4.biology
5.chemistry
6.economics
7.agriculture

ambayo yanahitaji modification

1.history and civics supposed to be one subject
2.kiswahili
3.language/English
4.kifaransa -lifutwe .
 
Vipi kuhusu historia inayotusaidia kutambua maendeleo/mabadiliko yanayotokea baada ya mwaka , karne baada ya Karne katika hayo masomo tajwa hapo juu?

,,,,Mfano historia kuhusu namna ya kupambana na magonjwa mfano wa corona yalitokea karne zilizopita.
Vipi hiyo historia haitusaidii?
Hizo tunaweza kusimuliana tu kama. Haihitaji concentration kubww kihivyo, mtu akitaka kubobea ataisoma chuoni.
 
Zama zimebadilika. Elimu ya kukariri watu kwenye historia, kufaulu mtihani na kupatiwa kazi haisaidii tena. Ni bora kupunguza hayo mambo, tena bora wangeacha masomo ya biashara yanayomfundisha mtu vitu practical.
Madhumuni ya elimu ni kuongeza ufahamu na maarifa ya kukabili mazingira yako. Hebu niambie huoni umuhimu wa kujua historia? Civics haikuongezei maarifa kweli?

Vv
 
Back
Top Bottom