Mwanafunzi wa kiume abakwa na wanawake 10

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,072
1,250
IMEZOELEKA sehemu nyingi duniani kusikia kesi nyingi za ubakaji huwahusisha wanaume. Lakini yaliyotokea Papua New Guinea yameshtua ulimwengu baada ya kesi ya kijana mdogo wa kiume kubakwa na kundi la wanawake.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 ambaye jina lake halikuwekwa hadharani, mkazi wa kijiji kimoja kilichopo nchini humo, amelazwa hospitali akipatiwa matibabu baada ya kubakwa na genge la wahuni wanawake 10.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Southern Highland, nchini humo, Teddy Tei, kijana huyo alikumbana na zahama hilo siku ya Ijumaa iliyopita wakati alipovamiwa na wanawake hao.

Kamanda huyo alieleza kuwa kijana huyo ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari iliyopo pembezoni mwa mji wa Mande, alikuwa kirejea nyumbani kutoka shule na kukumbana ana kadhia hiyo mbaya.

Wanawake hao wakiwa na visu walimshambulia kijana huyo kabla ya kupokezana kumbaka kwa zamu.

"Hii ni kesi tunayoifuatilia kwa ukaribu zaidi, tunawatafuta wanawake waliofanya unyama huu", alisema kamanda huyo wa polisi.

Taarifa ya polisi ilisema baada ya kumshambulia kwa visu, wanawake wanne kati yao walianza kumuingilia kijana huyo.Kamanda Tei aliongeza kuwa kijana huyo aliwahishwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Kijana huyo anafanyiwa uchunguzi ili kujua kama ameambukizwa magonjwa ya zinaa au la.

"Ugonjwa wa Ukimwi ni tatizo kubwa hapa nchini, ninahofia baadhi ya wanawake waliombaka huenda wakawa ni waathirika", alisema Kamanda Tei na kuongeza;

"Nimekuwa nikiwaonya wanawake wawe waangalifu sasa inanibidi nianze kuwaonya na wanaume nao wawe waangalifu mitaani wasije wakabakwa".

Hata hivyo, polisi bado wanaendelea na uchunguzi na haikuwekwa wazi ni sehemu ipi ambapo tukio hilo lilitokea kutokana na kijana huyo kupoteza fahamu na kutupwa eneo la mbali.

Wiki iliyopita binti mmoja nchini Australia alibakwa akiwa anarejea kutoka shuleni kaskazini magharibi mwa nchi hiyo na inadaiwa kuwa ameambukizwa ugonjwa wa Ukimwi.

Mwaka 2008 shirika la UNICEF liliripoti kuwa nchi ya Papua New Guinea ni nchi inayoongoza kwa kuwa na kasi ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa ukiwamo Ukimwi.

Katika ripoti hiyo ilielezwa kuwa asilimia nane ya wanawake waliripotiwa kubakwa, lakini kuna idadi kubwa ya tatizo hilo ambalo limekuwa haliripotiwi katika vyombo husika.

Ripoti hiyo ilifafanua kuwa nusu ya wanawake wanaoripotiwa kubakwa ni wenye miaka chini ya 15 na asilimia 13 ni wadogo chini ya miaka saba.

Imeandaliwa na Herieth Makwetta kwa msaada wa Mtandao wa kompyuta
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom