Mwanafunzi wa darasa la sita abakwa na watu sita

Mwili wote unasisimka....! Hao wazazi wamuone.mkuu wa kituo husika, yamkini hao polisi wameshapewa chao hivyo hawataki kufungua jalada.
Jamani Mungu awe nae binti huyo aliyefanyiwa unyama huo.
 
Joyce Kilia saidia huyu mtoto walio mtendea uovu wapate adhabu inayo wastahili hakuna mambo ya kuyamaliza kifamilia.
Wanyongwe
 
Mi namlaum na mama pia kwa malezi yasiyo na kiwango. Sababu mtoto ameonekana asubh na shangazi. Yeye alipogombana na mwanae hakuchukua hatua yakuulizia amelala wapi. Hebu wazazi tuwalee watoto ktk maadili tumekuwa tunatingwa nakutafuta pesa bila kujali afya, elimu na ulinzi wa watoto tumewaachia wasichana wa kazi, walimu na kujilea wenyewe. Mungu atusamehe na kutufanya upya mioyo yetu
 
MWANAFUNZI wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 13 wa shule ya msingi ya Themi iliyopo jijini Arusha mkoani Arusha hali yake siyo nzuri baada ya kunajisiwa na watu sita.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa 1 usiku Oktoba 7 mwaka huu katika kata ya Daraja Mbili jijini hapa. Imeelezwa kuwa sehemu yake ya kizazi imeharibika kutokana na unyama huo.

Akizungumza na gazeti hili jana nyumbani kwake Daraja Mbili mara baada ya kuruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Kanisa Katoliki ya Father Babu ya jijini na kuendelea na matibabu Hospitali ya Serikali ya Mount Meru Arusha mwanafunzi huyo alisema pamoja na kuruhusiwa kutoka hospitali lakini hawezi kutembea kutokana na maumivu makali yanayomsumbua.

Alisema siku hiyo kulitokea ugomvi nyumbani na mama yake Zukhura Said (40) na aliamua kukimbilia kwa mjomba wake ndipo njiani alipokutwa na dhahama hiyo ambayo katika maisha yake hataisahau.

Mwanafunzi huyo alisema alifanyiwa unyama huo karibu sana na nyumbani kwao na watu waliomfanyia unyama huo anawafahamu kwa majina na sura na watatu wameshakamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha na watatu bado hawajakamatwa.

Mwanafunzi huyo akizungumza alisema wakati akifanyiwa unyama huo alipoteza fahamu na alijikuta asubuhi akiwa nje ya chumba cha mmoja wa watuhumiwa hao.

‘’Nimefanyiwa unyama mkubwa sana nilipoteza fahamu kutokana na unyama huo na kwa mujibu wa daktari kizazi changu kimetoboka shangazi yangu ndio aliyepiga simu nyumbani kujulisha hali hiyo kwani alinikuta hapo nje asubuhi majira ya saa 2 asubuhi’’, alisema mwanafunzi huyo.

Akizungumzia tukio hilo mama mzazi wa mtoto huyo, Zukhura Said (40) alisema anasikitishwa na jinsi upelelezi wa tukio hilo unavyoendeshwa kwani mpelelezi wa tukio hilo {jina tunalo} amekuwa mstari wa mbele kutaka wazazi wa pande zote wamalizane kwa kukaa mezani.

Mama huyo alisema wahalifu waliosalia wako mtaani na wazazi wao kwa kushirikiana na kiongozi wa mtaa {jina tunalo} wanafanya kila njama na fitina kutaka kesi hiyo iondolewe Polisi na kurudishwa nyumbani.


Chanzo: Habarileo
hukumu wabakaji na wao wabakwe tu kilazima..
 
Raisi wa hii jamuhuri alishawahi kusema wanabakwa sababu ya viherehere vyao.Tehe tehe tehe utagombanaje na mama yako kama si kiherehere hicho?
 
tusisingizie taifa lililolaaniwa, huko ni kukwepa majukumu, wazazi tuna kesi ya kujibu, itakuwaje binti yako alale nje bila ridhaa yako mzazi?vibinti vya siku hizi vinapenda kujaribu, lakini vijana wa kiume wanapenda kukomoa, hapo inakuwa ngoma droo, pole binti huo ndio ukubwa uliokuwa unautafuta
 
kuongezeka kwa matukio ya ubakaji wa wanawake na watoto wa kike wao wenyewe ndio chanzo(baadhi)..Hii style ya kwenda na wakati mavazi ya kuvaa(nusu Uch) nguo za kuonyesha maumbile ya jinsia ya kike A-Z tene wanapita chochoroni na njia za panya.Ndio imepelekea vibaka na wanaume ambao hawajiheshimu kushindwa kukontrol hisia zao..(wanawake na watoto wa kike jaribuni kuvaa nguo za heshima)
 
huyo askari mk.undu sana.ku.mamaye yaani katoto kanabakwa yeye anataka wakae mezani?kuna kesi za kumaliza mezani na kuna kesi lazima wapumbavu kama hao waadhibiwe.angebakwa askari wa kike wabgemshauri amalizane nao mezni?angebakwa mke wake,mama yake au binti yake angekaa nao meza moja?
 
huyo mama yake nae akili hana mtoto wa kike unamruhusu anakimbia halafu yeye amekaa tu! alishindwa nini kufunga mlango na kumwadhibu usiku huo au asubiri kukuche..!? lakini mtoto umleavyo....! serikali ichukue hatua stahiki ni jambo ambalo linahitaji sheria kali ili iwe fundisho kwa wapumbavu wengine kama hao.
 
Hivi hawa waendesha mashtaka na wanasheria huwa hawatafuti lopholes za kisheria kuwaunganisha wanaowasaidia wahalifu na kuwaunganisha na washtakiwa? Kwanini hawawasaidii wanaonyimwa haki? Au mpaka uwe na pesa? Hebu watenge nafasi za kuwasaidia wengine bila gharama kama sadaka yao kwa muumba wa wote. Wakumbuke ipo siku watauhitaji msaada wa jamii inayowazunguka.
Kamata huyo afande njaa na wazazi wa wahalifu kwa kuwasaidia wahalifu kisha tuone matokeo. Hebu wajiweke kwenye maumivu ya huyo binti japo kwa sekunde tu!

Wanasheria wanahusika vipi hapo?
 
Naamini hili tukio haliwezi ishia hapo, bila kujali Kama mtoto alikuwa Ana tabia gani, ubakaji Ni ubakaji Tu, tena huu wa gang rape, Ni mbaya Sana.
 
Back
Top Bottom