Mwanafunzi wa darasa la pili atekwa na kuuawa Busega mkoani Simiyu

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,364
2,000
Mwanafunzi wa shule ya msingi Lukungu kata ya Lamadi wilayani Busega mkoani Simiyu Joyce Joseph miaka 8 aliyekuwa akisoma darasa la pili katika shule hiyo ametekwa na watu wasiojulikana na kumuuwa na kisha mwili wake kutelekezwa kichakani.

ITV imefika nyumbani kwao na marehemu katika kijiji cha Lukungu na kukuta umati mkubwa wa waombelezaji wakiwa wamejawa na majonzi.

Wakiongea kwa jazba baadhi ya wananchi waliokuwepo katika msiba huo wamesema kwa hivi sasa wanaishi kwa hofu kubwa kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo kwani hadi hivi sasa watoto wadogo wanne na binti wa miaka 21 wameshauawa.

Matukio hayo sasa yamewafanya wananchi wa kata ya Lamadi na wilaya ya Busega kuishi kwa hofu kubwa huku wazazi wakilazimika kuwasindikiza watoto waendapo mashuleni kwa kuhofia watoto wao kutekwa na kuuwawa
 
kantalambaz

JF-Expert Member
Dec 24, 2017
1,647

Hizi habari zimethibitishwa na mamlaka ipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwameh

JF-Expert Member
Dec 3, 2011
1,353
2,000
Mwanafunzi wa shule ya msingi Lukungu kata ya Lamadi wilayani Busega mkoani Simiyu Joyce Joseph miaka 8 aliyekuwa akisoma darasa la pili katika shule hiyo ametekwa na watu wasiojulikana na kumuuwa na kisha mwili wake kutelekezwa kichakani.

ITV imefika nyumbani kwao na marehemu katika kijiji cha Lukungu na kukuta umati mkubwa wa waombelezaji wakiwa wamejawa na majonzi.

Wakiongea kwa jazba baadhi ya wananchi waliokuwepo katika msiba huo wamesema kwa hivi sasa wanaishi kwa hofu kubwa kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo kwani hadi hivi sasa watoto wadogo wanne na binti wa miaka 21 wameshauawa.

Matukio hayo sasa yamewafanya wananchi wa kata ya Lamadi na wilaya ya Busega kuishi kwa hofu kubwa huku wazazi wakilazimika kuwasindikiza watoto waendapo mashuleni kwa kuhofia watoto wao kutekwa na kuuwawa
ITV MEDIA, li chombo la li nchi la watu ambao hawakusoma, hawana uchambuzi.

Mwandishi ameshindwa kueleza zinazodhaniwa kuwa ni sababu au motives za watoto kutekwa na kuuawa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom