Mwanafunzi wa Chuo Cha IFM afikishwa Mahakamani kwa kumwingiza mtoto vidole sehemu za siri

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Mussa Msafiri (23), alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni jana akituhumiwa kumwingizia vidole sehemu za siri mtoto mwenye umri wa miaka minne.

Mbele ya Hakimu Issa Kasailo, Wakili wa Serikali, Matarasa Maharagande, alidai mtuhumiwa alitenda kosa hilo Januari 7 mwaka huu maeneo ya Sinza alikokuwa anaishi mwanafunzi huyo.

“Mtuhumiwa ulitenda kosa hilo wakati ukitambua kwamba ni kinyume cha sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alidai wakili.

Baada ya maelezo hayo mtuhumiwa alikana kutenda kosa hilo na upelelezi unaendelea.

Hakimu Kasailo alisema shitaka hilo linadhaminika hivyo alimtaka mtuhumiwa kuwa na wadhamini wawili waaminifu watakaoweka saini ya maandishi ya Sh milioni tano kwa kila mmoja.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Febuari 27 mwaka huu na mtuhumiwa aliachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
 
Yaani ushenzi kama huu huwa hauhitaji kudhaminiwa :mad:!!! Hata kama ni not guilty until proven so..
 
Yawezekana toka azaliwe hajawahi ku-do na papuchi ya Kike hajawahi kuiona Live anaiona kwenye mitandao tu hivyo labda akaamua aangalie imekaaje?... teh..teh..teh.. Domo zege..
 
Uswahilini kuna Mengi!! Acha hukumu itoke ndio tujue!! Watoto wa siku hizi anaweza akapangwa ushahidi wa Uongo na akatiririka Mahakamni kama vile vitoto vinavyoigiza kwenye Bongo Movies.
Kuna kesi moja katoto kalitengenezwa kakatoa ushahidi wa Uongo dhidi ya Kaka yake anaechangia Baba kwa kufundishwa na Mama yake, tulivyo kahoji kirafiki zaidi kwa kalieleza ukweli mpaka Mkuu wa Kituo cha Polisi akabaki Mdomo wazi, Tuepuke kuhukumu kabla
 
mkuu naunga mkono hoja yako!unajua kuna vitoto hapa duniani vimejaaliwa vichwa na upeo mzuri wa kumeza mambo,na wengune wanaconfidence ya kutosha kabisa,kumbe ni uongo aliopikwa nao na anautiririka utasema kweli na kulia anaweza kulia aise...hatari sana.
 
Hakuna haja ya kumuukumu mtu mpka hapo mahakama itathibitsha kweli katenda hivyo kwani dunia ya sasa ina kila aina ya hila, nidhamu kwa binadamu wengi wawe watoto, watu wazima imetoweka, kweli mtu anaweza tenda kosa tofauti na jamii inavyomchukulia au mtu awe mtoto au mkubwa anaweza lishwa maneno kwa nia tu ya kukuaribia au kukomeshwa uione dunia chungu
 
Zamani mtoto alikuwa anasikilizwa sana lakini sikuiz mambo mengi watu hawaaminiki,wanawatumia watoto kujipatia kipatoh hasa akiwa mtoto mwenye IQ kubwa.kama kweli amefanya hivyo Mungu atasema nae,na kama hajafanya basi Mungu aseme na upande wa pili
 
Yaani ushenzi kama huu huwa hauhitaji kudhaminiwa :mad:!!! Hata kama ni not guilty until proven so..
Acha mihemko bidada. Mtuhumiwa pia ana haki zake. What if ni minyukano ya mitaani, kashikishwa na mama mtoto kwa bifu zao?
 
Back
Top Bottom