Mwanafunzi wa chuo apigwa risasi na polisi, Mashuhuda waelezea tukio zima

Huo ndiyo ujinga wenu ulipolala, hamkuona jinsi watanzania na serikali walivyowajibika baada ya hilo unfortunate event?, kwanza haikuwa intended kumuua kwa hiyo ni kosa kusema brutally murdered labda kama kiingereza hukijui vizuri, it was accidentally murdered, huyu mwanafunzi wa Meru ndiyo brutally murdered.

Tuachozungumza hapa ni reactions baada ya tukio, wakati Tanzania nzima shughuli zilikaribia kusimama kutokana na hicho kifo cha bahati mbaya, huko kwenu hamjali na hakuna mtu anayeshughulika kwa kifo cha makusudi kabisa, wakati huko DRC wamemfunga kifungo cha maisha askari aliyempiga risasi na kumuua muandamanaji, huko kwenu hata uchunguzi hakuna.
Blah blah blah who told you nothing is being done about it. dont expose your ignorance any further.

Kenyans up in arms against police over brutal killing of Meru University student leader
 
BBC News Swahili
menu
Kiongozi wa wanafunzi auawa kwa kupigwa risasi Kenya
  • 28 Februari 2018
Sambaza habari hii Email Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Whatsapp
Image copyrightHISANI, FACEBOOK
_100214170_742c4f55-f124-47c6-ba11-29790fe35ead.jpg

Image captionBango la kampeni la Evans Njoroge
Kifo cha Mwanafunzi wa Chuo kikuu nchini Kenya kimezuaa shutuma mpya za mauaji yanayodaiwa kutekelezwa na maafisa wa polisi nchini humo.

Ripoti zinasema Evans Njoroge, mwanafunzi ambaye alikua kiongozi Chuo kikuu cha Meru nchini humo, aliuawa kwa kupigwa risasi na anayedaiwa kuwa polisi.

Mwandishi wa BBC, Ferdinand Omondi anasema pichaza mwili wa kijana huyo, damu yake ikionekana imetapakaa kote, zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii huku raia wa Kenya wakighadhabishwa na kile walichodai kuwa mauaji yanayotekelezwa na polisi.

Evans alipigwa risasi Jumanne wakati wa maandamano ya wanafunzi waliokuwa wakilalamikia ongezeko la ada dhidi ya chuo cha Meru.

Vyombo vya habari nchini Kenya vimemnukuu shuhuda mmoja akisema polisi walimkimbiza Evans wakamfikia kisha mmoja wao akampiga risasi na kuondoka.

Mkuu wa polisi Jenerali Joseph Boinnet ameamuru kufanyika uchunguzi kuhusu kifo hicho baada ya kuwepo kwa wanasiasa na makundi ya wanaharakati waliokuwa wakitaka mauaji yanayodaiwa kutekelezwa na polisi kukoma mara moja.

Shirika huru la kiraia linalofuatilia shughuli za polisi (IPOA) limesema limewatuma maafisa wake kuchunguza tukio hilo.

Mwanafunzi huyo aliuawa katika eneo la Nchiru, eneo la Tigania West katika jimbo la Meru ambalo linapatikana katika eneo la Mlima Kenya.

IPOA wamesema maafisa wa uchunguzi wametukwa kwa lengo la: "kuchunguza kuhusu yaliyotokea wakati wa mauaji hayo na iwapo kuna mtu anayefaa kulaumiwa, na kuhakikisha afisa yeyote wa polisi atakayepatikana na hatia anawajibishwa kisheria."

Wakenya mtandaoni wamekuwa wakishutumu mauaji hayo.

Shutuma hizi mpya zimekuja siku kadhaa baada ya shirika linalotetea haki za binadamu la Human Rights Watch kuwasilisha ushahidi mpya kuwa polisi nchini Kenya waliua watu takriban 23 wakati wa kipindi cha marudio ya uchaguzi nchini humo mwaka jana.

Kwa mujibu wa ripoti,uchunguzi umebaini kuwa wengi wa waathirika walifyatuliwa risasi na silaha za nguvu.

Polisi wameendelea kukana shutuma hizo.
 
Leo ni siku ya pili hata kulizungumzia hawalizungumzii, lini wataadamana, au wanasubiri sherehe zao za sikukuu ya jamhuri ndiyo waunganishe maandamano yawe makubwa?. Chris Msando na Jacob Juma walipouliwa, mbona hawakuandamana, watu 60 waliouliwa katika vipindi vya uchaguzi, mbona wanazika wafu wao kimya kimya hawaandamani?. Nafuu Tanzania alipokufa Akwilina watu walipaza sauti na serikali japo iliomba radhi, Kenya hata hawazungumzi lolote, kwanza wajaluo wanafurahi kwasababu huyo mwanafunzi ni mkikuyu, kamwe usilinganishe Kenya na Tanzania katika eneo hilo.
Si busara kujipima afya yako kwa kujilisha na mgonjwa aliyelazwa chumba cha wagonjwa chumba wagonjwa wanohitaji uangalizi maalum (ICU)
Tanzania inashida usijifariji kwa kuilinganisha na Kenya
Tanzania no mbaya zaidi kwa sababu mauaji ya namna hii ndiyo yanaanza kuongezeka wakati Kenya yanapungua
 
Watawala wa Africa mashariki wanafanana kwa mambo mengi haswa masuala ya ukandamizaji wa demokrasia Wakati mwingine nafikiria huenda viongozi wa nchi hizi wamezaliwa kwenye ukoo mmoja . Sijui tu lakini akili yangu imeshindwa kufikiri zaidi.

RIP mwanafunzi . Poleni wazazi
 
Kama ana mdogo wake atasomeshwa mpaka chuo kikuu.
Inasikitisha sana.
 
Si busara kujipima afya yako kwa kujilisha na mgonjwa aliyelazwa chumba cha wagonjwa chumba wagonjwa wanohitaji uangalizi maalum (ICU)
Tanzania inashida usijifariji kwa kuilinganisha na Kenya
Tanzania no mbaya zaidi kwa sababu mauaji ya namna hii ndiyo yanaanza kuongezeka wakati Kenya yanapungua
Tunaomba data zinazoonysha Kenya yanapungua na Tanzania yanaongezeka, ninaweza kukubaliana kwamba Tanzania yanaongezeka, kwa sababu kama hakuna ugonjwa wa kipindupindu, akitokea hata mgonjwa mmoja inahesabika ugonjwa unaongezeka, lakini Kenya hali ndiyo inazidi kuwa mbaya, mwaka uliopita Kenya imeongoza Afrika katika mauaji ya kiholela, utasemaje mauaji yanapungua?
 
Leo ni siku ya pili hata kulizungumzia hawalizungumzii, lini wataadamana, au wanasubiri sherehe zao za sikukuu ya jamhuri ndiyo waunganishe maandamano yawe makubwa?. Chris Msando na Jacob Juma walipouliwa, mbona hawakuandamana, watu 60 waliouliwa katika vipindi vya uchaguzi, mbona wanazika wafu wao kimya kimya hawaandamani?. Nafuu Tanzania alipokufa Akwilina watu walipaza sauti na serikali japo iliomba radhi, Kenya hata hawazungumzi lolote, kwanza wajaluo wanafurahi kwasababu huyo mwanafunzi ni mkikuyu, KAMWE USILINGANISHE KENYA NA TANZANIA KATIKA ENEO HILO.
Umeuaa... Ha ha ha ha saa..
 
Kiongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Meru nchini Kenya, Evans Njoroge ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi jana Februari 27,2018 katika maanadamano chuoni hapo wakishinikiza chuo hicho kupunguza ada yao kwa kiasi cha shilingi 8,500 za Kenya ambazo ni sawa na Tsh 188,566 na kuboreshewa miundombinu chuoni hapo.

Mashuhuda wa tukio hilo waliohojiwa na kituo cha runinga cha NTV wamesema kuwa wanafunzi wa chuo hicho baada ya vurugu walikimbia nje ya chuo na kwenda kujificha mashambani baada ya kuona gari la polisi.

Shuhuda mmoja ambaye mwanafunzi huyo ameuawa kwenye shamba lake la viazi vitamu, amesema kuwa maaskari baada ya kuwakosa chuoni walikuja uraiani walipomuuliza kama amewaona wanafunzi hao alikataa kuwajibu, lakini baadaye mtoto wake aliwaelekeza polisi wanafunzi hao walipojificha.

Baada ya dakika mbili mama huyo ambaye jina lake halijatajwa kwa sababu za kiusalama alisema alisikia mlio wa bunduki na alipotoka alimkuta askari anabadilisha mavazi yake na kubakia na nguo za kiraia.

Niliona wanafunzi wakikimbia nje ya geti la nyumba yangu wengine wakielekea mashambani, muda mfupi baadae nikaona polisi wakiingia getini kwangu wakiniulizia walikojificha sikuwajibu! hadi mtoto wangu alipowaambia, baadaye baada ya kumuona mwanafunzi huyo amejificha kwenye mti alimpiga risasi wakati alipotaka kumkimbia na akabadilisha nguo zake na kurudi kwenye gari,“amesema shuhuda kwenye mahojiano yake na Kituo cha NTV Kenya.

Kwa upande wa mashuhuda wengine wamesema kuwa polisi huyo aliyemuua mwanafunzi anafahamika ni Afisa wa jeshi la polisi la kituo cha Nchiru.

Taarifa kutoka kituo kingine kikubwa cha polisi cha Tigania, kupitia kwa msemaji mkuu wa kituo hicho, Kamanda Adamson Furaha amesema kuwa alisikia kuna maandamano na alituma polisi wa kuzuia maandano hayo.

Kwa upande wa uongozi chuoni hapo umesema kuwa umepata taarifa hizo na mwili wa mwanafunzi umepelekwa Hospitali kwa ajili ya majibu ya kitabibu. Tazama video aliyorekodiwa kabla kuuawa muda mfupi baadaye.

Hata hivyo baada ya tukio hilo wanafunzi waliendelea kushinikiza makamu wa Rais wa chuo hicho, Japheth Magambo kujiuzulu nafasi yake kwani ndiye anayeharibu chuo hicho. Baadhi ya Wakenya wakiwemo viongozi na wanaharakati wamelaani vikali tukio hilo la askari kujichukulia sheria mkononi, wengi wakisema kuwa ni tukio la kinyama.

Tayari jeshi la polisi nchini Kenya linafanya uchunguzi juu ya tukio hilo, na Chuo hicho kilichotakiwa kufunguliwa leo Februari 28, 2018 kupitia mtandao wake kimatangaza kuahirisha hadi Machi 6, 2018.

View attachment 702510





Bongo 5

Tanzania: Send Army to Curb Coast Killings, Opposition Says
Tagged:


tweet

share

Google+

comment


email


more

Related Topics
00360598:dacb8603ebac14b4b22d3dd78b46bc2b:arc614x376:w285:us1.png
Photo: Morgan Mbabazi/The East African
Tanzanian soldiers in training (file photo).
By Athuman Mtulya
Dodoma — The Opposition camp in Parliament yesterday asked the government to deploy the Tanzania People's Defence Forces (TPDF) in three districts of Coast Region to halt the wave of killings.

In his alternative budget speech, the Deputy Shadow Minister for Defence and National Service, Mr Mwita Waitara (Ukonga-Chadema), said the Opposition was concerned by the series of attacks by unknown assailants that have so far resulted into the deaths of 30 people, mostly local government leaders. Police officers have also not been spared either.

Mr Waitara termed the incidents "terror attacks" perpetrated by well-trained individuals, that is why they have so far managed to escape arrest, without their names known or whereabouts exposed.

"There's every indication that police have been tactically beaten by the terrorists. It is for this reason, the Opposition suggests that the TPDF, especially its intelligence unit, should chip in and assist in collecting intelligence and reconnaissance information to expose and take on the killers," reads the Opposition speech.

The latest victim was gunned down on Saturday. The assailants' motives have remained a mystery. The most affected districts are Mkuranga, Kibiti and Rufiji in Coast region.

Police have tightened their guard in the area, but that alone did not stop them from falling prey to the merciless assailants. In April 14 seven police were gunned down. They were returning to camp after a daylong shift. Their camp is 100km from Dar es Salaam and was established in response to activities linked to a shadowy group along the coast that has mounted sporadic attacks on security personnel and local leaders.

The Minister for Home Affairs last week told the parliament as he was tabling his office's budget that the government plans to establish a special police zone in Kibiti to arrest the wave of brutal killings in the area.

Earlier, reading his budget speech in parliament, the Minister for Defence and National Service Dr Hussein Mwinyi said TPDF has continued to work shoulder to shoulder with other security organs to flush out among other things terror elements in the country.
Tanzania: Send Army to Curb Coast Killings - Opposition
 
Leo ni siku ya pili hata kulizungumzia hawalizungumzii, lini wataadamana, au wanasubiri sherehe zao za sikukuu ya jamhuri ndiyo waunganishe maandamano yawe makubwa?. Chris Msando na Jacob Juma walipouliwa, mbona hawakuandamana, watu 60 waliouliwa katika vipindi vya uchaguzi, mbona wanazika wafu wao kimya kimya hawaandamani?. Nafuu Tanzania alipokufa Akwilina watu walipaza sauti na serikali japo iliomba radhi, Kenya hata hawazungumzi lolote, kwanza wajaluo wanafurahi kwasababu huyo mwanafunzi ni mkikuyu, kamwe usilinganishe Kenya na Tanzania katika eneo hilo.

Kwa hiyo wamezoea kuuana kama wanyama, hawa Manyangau akili zao wanazijua wenyewe
 
Unyama wa polisi wa Kenya hauna mfano hapa Afrika na dunia nzima, watu wameshakimbia na kujificha, bado mnawasaka na kuwapiga risasi kinyama kabisa, Kenya is really a failed state.
Kwani hapa ukikimbia wanakuacha?
 
Back
Top Bottom