Mwanafunzi SAUT Mwanza afariki dunia baada ya kushikwa kifafa na kuanguka kwenye Ziwa Viktoria

Manchid

JF-Expert Member
May 29, 2016
217
445
Mwanafunzi wa mwaka wa tatu BAEC chuo kikuu cha St. Augustine Mwanza amefariki dunia ziwani leo asubuhi.

Inadaiwa alikuwa na kifafa hivyo aliangukia pembezoni mwa ziwa na hakuwa na watu wa kumpatia msaada wa haraka. Inauma Sana

Mungu amlaze mahali pema peponi.
8b15010b089c7650eb5dd47aff0d90b0.jpg
 
Maelezo yako mkuu sijayaelewa vizuri, kuna uhusiano wa kifo na dhehebu alilokua anaamini au hicho kitambulisho.
 
Hiyo ni picha na jina lake hakuna uhusiano na dhehebu marehemu anawezaje kutoa taarifa?
 
Unajua humu tunapeana taarifa kama hizi tukiamini inaweza kumgusa mtu humu humu so tupunguze majungu kidogo wadau
 
Hyo ni picha na jina lake hakuna uhusiano na dhehebu marehemu anawezaje kutoa taarifa??? Kuna watu mapunguani humu
Sasa mwenye tatizo hapa ni nani, mleta taarifa au wachangiaji, ukiona hivyo jua kilicholetwa maelezo hayajitosholeze kuelewa kulichokusudiwa.
 
Na tena anaongezea eti hakukuwa na umuhim wa kuanzisha thread,angekuwa na uhusiano na marehem nadhan angejua umuhim wa hiyo habar
kila msiba ukitikea tukaja kuanzisha thread je kwa siku tutakua na thread ngapi? just imagine kila jf members akipost misiba unafikiri hata habari tutapeana za matukio muhimu tutapeana kweli? all in all nawaomba mods muanzishe jukwaa la misiba ili tuhabarishane,......kama kuna mtu nimemkwaza kwa kauli yangu naomba mnisamehe
 
Nimerudi kwenye kichwa cha habari, sasa kina uwuano na kilichopo ndani, kichwa cha habari mwanzo, kilikua hakienda na maelezo ndani yaani kusudi ya habari nini, ilikua inakosekana.
 
Ulitaka maelezo gani kwa mfano
Sijui hii habari imeandikwa na watu wawili tofauti ila kwa kusudi moja na MOD wakaamua kuinganishwa au la. Mwanzo ilikuwa na kichwa cha habari, alibakiza siku, kumaliza chuo, siku zilitajwa ila sizikumbuki. Mletaji wa mwanzo unaonekaka sio wewe, ila sasahivi ukisoma kichwa cha habari kinajieleza dhumuni lake.
 
kila msiba ukitikea tukaja kuanzisha thread je kwa siku tutakua na thread ngapi? just imagine kila jf members akipost misiba unafikiri hata habari tutapeana za matukio muhimu tutapeana kweli? all in all nawaomba mods muanzishe jukwaa la misiba ili tuhabarishane,......kama kuna mtu nimemkwaza kwa kauli yangu naomba mnisamehe
Nilitegemea kwa id yako ungekuwa ni mtu wa busara.
Kila nafsi ni lazima itaonja umauti tu.Suala linalotatiza ni namna kifo kinavyotokea.
Labda nikuulize zile taarifa za ajali za barabarani gar kupinduka au kugongana na vifo kutokea kwako unachukuliaje labda?
Kwangu mim hii habar imenihuzunisha kwa kuangalia namna tatizo la kifafa linavyoweza kusababisha kifo kwa mtu.
Pia ni funzo kwang kama kuna nina kifafa au ndug mwenye kifafa ni suala la kuchukua tahadhar pindi ninapokuwa au anapokuwa pembezoni mwa maji.
Kuwa muungwana ustadh
 
Mleta mada hiki ulichowasilisha ni taarifa rasmi ya polisi au hisia zako tu
 
R.I.P Dan Allen Kinanda.
msiba huu unahuzunisha sana jinsi ulivyotokea .poleni sana SAUT
 

Attachments

  • Allen 20160703_125226.jpg
    Allen 20160703_125226.jpg
    8.3 KB · Views: 47
Back
Top Bottom