Mwanafunzi Mzee Kuliko Wote duniani Afariki Kabla ya Kumaliza Shule ya Msingi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanafunzi Mzee Kuliko Wote duniani Afariki Kabla ya Kumaliza Shule ya Msingi

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Aug 16, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Babu Maruge akiwa darasani Saturday, August 15, 2009 9:35 AM
  Mkenya aliyeingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia, Guinness kama mwanafunzi mzee kuliko wote duniani, amefariki kabla ya kumaliza shule ya msingi akiwa na umri wa miaka 90.
  Mkenya Stephen Kimani Maruge, aliingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia kama mwanafunzi mzee kuliko wote duniani wakati alipoanza elimu ya shule ya msingi mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 84.

  Maruge amefariki jana kutokana na ugonjwa wa kansa ya tumbo akiwa kwenye nyumba ya kutunza wazee jijini Nairobi.

  Taarifa zilisema kwamba Maruge alifariki saa saba mchana ndani ya chumba chake akiwa pamoja na mmoja wa watoto wake. Maandalizi ya mazishi yake yanaendelea.

  Mwaka 2003, Maruge aliishangaza dunia alipoamua kujisajili kuanza darasa la kwanza baada ya serikali ya rais Kibaki kutangaza kutoa elimu ya shule ya msingi BURE.

  Maruge alijipatia umaarufu wa ghafla na aliingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia Guinness akitambulika kama mwanafunzi mzee kuliko wote duniani.

  Maruge amefariki akiwa darasa la saba akiwa amebakiza darasa moja tu kujipatia cheti cha kumaliza elimu ya msingi. Elimu ya msingi Kenya ni miaka minane.

  Katika maisha yake ya kiuanafunzi, Maruge alichaguliwa kuwa kaka mkuu wa shule mwaka 2005.

  Mwaka huo huo mwezi septemba, Maruge alipanda ndege kwa mara ya kwanza na kwenda New York, Marekani kuhutubia katika mkutano wa umoja wa mataifa, umuhimu wa kutoa elimu ya msingi bure.

  Mwaka 2007-2008 wakati wa vurugu za uchaguzi Kenya, vibaka walimliza mzee huyo kwa kumuibia baadhi ya mali zake kwenye nyumba yake.

  Maruge alienda kuishi kwenye kambi ya wakimbizi mwanzoni mwa mwaka 2008 wakati vurugu hizo zilipopamba moto lakini aliendelea kuhudhuria shule kila siku.

  Mke wa Maruge alishafariki miaka mingi sana iliyopita. Maruge alikuwa na wajukuu 30, wajuu wake wawili kati yao alikuwa akisoma nao shule moja ya msingi.

  Kuna filamu kuhusiana na maisha ya Maruge, inayoitwa "The First Grader" iko jikoni ikiandaliwa na watengeneza filamu wa Marekani nchini Afrika Kusini. Kaa mkao wa kula kuisubiri filamu hiyo.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2819702&&Cat=2
   
 2. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  Hii habari mbona imetundikwa kwenye udaku?
   
 3. senator

  senator JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2009
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Ipelekwe kwenye sehemu yake huku naona imekosewa mods imuvuzishe
   
 4. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135

  Exactly! this aint a joke..mods hamisheni to jukwaa la elimu etc.
   
Loading...