Mwanafunzi mwingine wa Chuo Kikuu amuua 'Geroflendi" wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanafunzi mwingine wa Chuo Kikuu amuua 'Geroflendi" wake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Jun 18, 2009.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,450
  Likes Received: 22,396
  Trophy Points: 280
  POLISI nchini Uganda inamshikilia mwanafunzi wa mwaka wa tatu anayechukua masomo ya Sayansi ya Jamii na uongozi katika Chuo Kikuu cha Kyambogo nchini humo, Sam Buyinza kwa tuhuma za kumuua rafiki yake wa kike.

  Buyinza anashikiliwa pamoja na watu wengine wanne, wakituhumiwa kumuua Grace Rubanga kwa kumpiga kabari Jumanne wiki iliyopita, kuuficha mwili wake kwenye boksi lililokuwa na televisheni na kisha kuutupa karibu na uwanja wa Mandela huko Namboole.

  Wengine waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo ni ndugu wa Buyinza, Betty Wanzira, rafiki yake mwingine wa kike, Martha Kabasita na dereva wa teksi ambaye bado hajatajwa rasmi.

  Kaimu msemaji wa polisi, Samson Lubega alilieleza gazeti la Daily Monitor la Uganda kuwa Buyinza anashikiliwa kama mtuhumiwa muhimu katika mauaji hayo.

  “Lakini upelelezi bado unaendelea,” alisema Lubega.

  Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, binti hyo aliyeuawa aliondoka nyumbani kwao huko Kiyunga, Wilaya ya Mukono Jumanne ya wiki iliyopita kwa ajili ya kuhudhuria semina iliyoandaliwa na kikundi kimoja kutoka Afrika Kusini huko Wandegeya.

  Alihudhuria kipindi cha asubuhi tu na mchana wa saa nane aliondoka na kwenda nyumbani kwao Buyinza huko Kireka.

  “Muda wa usiku uliibuka ugomvi baina yao. Ugomvi huo uliwafikisha katika hatua ya kupigana na Buyinza alipiga mpenzi wake huyo kwa kutumia gongo hadi kufa,” ilieleza taarifa hiyo ya polisi.

  Kwa mujibu wa polisi, Buyinza alijaribu kuwaficha majirani zake na kuuacha mwili huo ndani hadi siku iliyofuata, yaani Jumatano ya wiki iliyopita, lakini alikuwa akifanya mipango ya kuuondoa kwa siri.

  “ Siku ya Alhamisi, aliukusanya, akaukunja na kuufunga mwili huo, kisha kuuweka kwenye boksi la televisheni. Baadaye aliusafirisha na kuutupa karibu na eneo la kuoshea magari katika barabara inayoelekea kwenye uwanja wa Mandela,” alisema Lubega.

  Mwili huo uligunduliwa na wakazi wa jirani na eneo hilo, ambao walitoa taarifa polisi. Wapelelezi walifanikiwa kupata kitambulisho cha Wanzira pembeni ya mwili wake ambao tayari ulishaharibika vibaya.

  “Uchunguzi wetu ulituwezesha kupata muunganiko wa Wanzira na Buyinza. “Yeye (Buyinza) alitueleza kuwa anahisi rafiki yake mwingine wa kike, Kabasita ndiye aliyehusika na uhalifu huo, lakini Kabasita alieleza kuwa alionana na Buyinza kwa mara ya mwisho zaidi ya mwezi mmoja uliopita,” alisema.

  Aliongeza kuwa Buyinza aliwachukua maafisa wa polisi hadi nyumbani kwake, ambapo uchunguzi wao uliwawezesha kubaini mabaki ya damu na rungu linalodhaniwa kutumika kumuua binti huyo.

  “Tumechukua mabaki hayo na kuyapeleka kwa wataalamau kwa ajili ya kupata ushahidi zaidi,” alisema,

  Mtuhumiwa huyo mkuu pia aliwapeleka maafisa wa polisi kwa dereva maalum wa kukodiwa ambaye anadaiwa kumsaidia kuusafirisha mwili huo kutoka katika eneo la tukio hadi sehemu walipoutupa.
  Hata hivyo, dereva huyo aliwaelza polisi kuwa alikodiwa na wanaume wawili akiwemo Buyinza, waliomweleza kuwa wana sanduku la dawa zilizoharibika na wanahitaji kwenda kuyatupa huko Namboole.

  Chanzo:- Mwananchi website
   
 2. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ni kiganda au?

  mm
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Guys don' recycle news. Hii habari ilikwisha kuletwa jamvini some days ago.
   
 4. c

  chuku Member

  #4
  Jun 18, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hawa wanafunzi na wao wamezidi kugombania ngono acha wauane,wao wanaenda chuo kwa kusoma lakini wanaendekeza ngono.
   
 5. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Inaonekana wameona kama fasheni? utasikia Kenya tena.
  ACHA UNYANYASAJI HUU HARAKA
   
 6. m

  mbwembwe Member

  #6
  Jun 20, 2009
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hawa watoto wanaendekeza sana ngono wakiwa shule na hata sijui kwa nini, ila wasipoangalia watakuja pata tabu kwenye maisha yao
   
Loading...