Mwanafunzi mwingine(Ilboru) afa maji akiogelea St. Gaspar Hotel dodoma

Nsoji go Nvaa

JF-Expert Member
Oct 15, 2019
757
1,442
Wimbi la wanafunzi kufa maji wakiogelea mkoan dodoma linazidi kushika kasi ambapo Jana jioni mwanafunzi mmoja wa ilboru kidato cha 5 aitwae Francis amefariki akiwa anaogelea katika hotel maarufu ya St Gasper iliyopo dodoma baada ya kunywa maji mengi na kusababisha kifo chake.

Mwanafunzi huyo alikimbizwa hospitali ya Nesuda lakini hadi anafikishwa pale alikuwa keshafariki njiani.

Itakumbukwa ni wiki hii tu mwanafunzi mwingine alifariki katika swimming pool ya Morena hotel ambapo alikutwa na dreva aliyekua amewapeleka maharusi kupiga picha huyo dreva alimuona mtoto anahangaika juu ya maji ndipo akajitosa na suti zake ndani ya maji kumuokoa bahati mbaya akafariki akikimbizwa general hospital Wakati tukio linatokea mama wa mtoto alikua amekaa akipata kinywaji hakujua mtoto kaingia swimming,

Tunaomba wenye hizo swimming waweke guide wa kuwacontrol watoto
 
Wimbi la wanafunzi kufa maji wakiogelea mkoan dodoma linazidi kushika kasi ambapo Jana jion mwanafunzi mmoja wa ilboru aitwae Francis amefariki akiwa anaogelea ktk hotel maarufu ya St Gasper iliyopo dodoma baada ya kunywa maji mengi na kusababisha kifo chake,mwanafunzi huyo alikimbizwa hosp ya Nesuda lkn hadi anafikishwa pale alikuwa keshafariki njian,itakumbukwa ni wiki hii tu mwanafunz mwingine alifariki ktk swimming pool ya Morena hotel ambapo alikutwa na dreva aliyekua amewapeleka maharusi kupiga picha huyo dreva alimuona mtoto anahangaika juu ya maji ndipo akajitosa na suti zake ndan ya maji kumuokoa bahati mbaya akafariki akikimbizwa general hospital wkt tukio linatokea mama wa mtoto alikua amekaa akipata kinywaji hakujua mtoto kaingia swimming,tunaomba wenye hizo swimming waweke guide wa kuwacontrol watoto
Ipo haja ya wenye hizi swimming pools kujua na kusimamia sheria
Pole kwa wafiwa
Rest well watoto
 
SGH.jpg
 
Hapo kwenye hayo matukio mawili kuna uzembe kwa wamiliki wa hizo pool dawa ni kuwashtaki walipe fidia kwa wathirika na pia hizo pool zifungwe hadi zikidhi vigezo vya kiusalama. Haiwezekani pool itumike na watoto au watu wengine bila kuwepo life saver au mwangalizi mwokozi maisha.
 
R.i.P waliokufa maji!
Kabla ya kuwalalumu wamiliki wa swimming pool,tuanze na wenye watoto wanaoenda ku bariz jirani na hizo sehemu huku wakiwa na watoto wadogo ndio wawe wakwanza kuwa na tahadhari.
 
Mkuu wewe una umri gani? una watoto? Unaujua umri wa hao watoto waliokufa? Unajua ukuaji wa watoto unavyohusisha kujaribu vitu hatari huku wakiamini vinawezekana? Jaribu kuwa na moyo wa huruma kidogo japo kwa wazazi waliopoteza vijana wao
Huyo mdudu alotoa comment uliyoreply hana tofauti na Meko, wote miroho kama shetani
 
Hapo kwenye hayo matukio mawili kuna uzembe kwa wamiliki wa hizo pool dawa ni kuwashtaki walipe fidia kwa wathirika na pia hizo pool zifungwe hadi zikidhi vigezo vya kiusalama. Haiwezekani pool itumike na watoto au watu wengine bila kuwepo life saver au mwangalizi mwokozi maisha.
Mkuu kwa hizi cases usihukumu mapema bila kuelewa mazingira yaliyokuwepo. Kuna mwaka mmoja siku ya krismas kama jana tu tulienda na familia katka moja ya hotels zilizopo ufukweni mwa bahari ya hindi. Sitotaja jina la hotel ila ni huu uelekeo ilipo beach komba. Mle ndani waliandaa bufee kwa ajili ya watakaoingia na unalipia kabisa kabla ya kuhudumiwa. Mle ndani kulikuwa na sehemu za michezo ya watoto games za kwenye screen kubwa na swimming pool na sehemu za watu kukaa pembezoni mwa bahari. Watu waliendelea kisherehekea kama kawaida na watoto waliopenda kuogelea walipewa hivyo vi life jackets na guider alikuwepo. Kama kawaida saa kumi na mbili jioni ni mwisho wa kuogelea so kwenye swimming pool kulifungwa kukabakia kwenye games na sehemu nyingine. Baadhi ya wazazi kama kawaida wanapata mvinyo etc. Ebwana wee kumbe kuna katoto katundu tundu hivi na kile kigiza kakaenda kujipenyeza sijui sehemu gani kakaimgia kwenye swimming pool bila kuonekana. Sasa muda wa ile familia kuondoka wacha wazunguke kumtafuta mtoto wakijua yuko kwenye games. Tafuta wee wapi hawamuoni. Wakaenda kwa wale madj wa pale watangaze kwa loud speakers kumwita. Holaaa mtoto hatokezei. Mwisho ikawa kutafuta pamoja na watumishi wa ile hotel. Lahaula wanamwona mtoto anaelea juu ya maji kwenye swimming pool keshakufa. Ilihali sehemu ya kuingilia ilishafungwa muda. Ktk mazingira yale nirudi kwenye hija yako tatizo sio wenye hotel kama unavyosema. Inategemea na mazingira. Inauma sana ila basi tu ndo familia ilielekea motuary baada sherehe zile. Any way nimetoa mfano tu hai kama angalizo.
 
Maji sio kitu cha kufanyia mzaha kabisa.

Maji ni mazuri kunywa na kuoga ila sio kuyachezea kama huyajui. Maji kama huyajui hata ya kwenye beseni yanakuua.

Poleni wafiwa wote.

Sisi tuliokulia maeneo yenye ziwa na mito mikubwa inayojaa maji yanayotembea kwa kasi ndio tunayajua maji vizuri.

Sasa mtu unazaliwa Dodoma, Singida, Tabora, Manyara, Arusha, Kilimanjaro halafu ujifanye unayajua maji lazima ndugu zako watakuimbia parapanda tu.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom