Mwanafunzi kulipwa zaidi ya mfanyakazi wa kima cha chini!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanafunzi kulipwa zaidi ya mfanyakazi wa kima cha chini!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ms Judith, Jul 20, 2011.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Posho elimu ya juu yapanda kwa Sh 2,500/-

  SERIKALI itaongeza fedha za kujikimu kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini kutoka Sh. 5,000 ya sasa hadi Sh. 7,500 katika mwaka huu wa fedha.

  Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dk. Shukuru Kawambwa, alipokuwa akisoma hotuba yake ya Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa Wizara yake kwa mwaka huu.

  Alisema, kiasi cha Sh. bilioni 77.8 kitatumika kwa suala hilo na wanafunzi 91,568 wa elimu ya juu wa mwaka wa kwanza na wanaoendelea na masomo na kwa wanaosoma shahada za uzamili na uzamivu, wanatarajiwa kupewa mikopo kwa mwaka 2011/12.

  Alisema katika mwaka huu wa fedha, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) itaimarisha utoaji na urejeshaji wa mikopo kwa kuainisha taarifa za wakopeshwaji na zile za Tume ya Vyuo Vikuu, Baraza la Mitihani na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa.

  Alisema pia Bodi hiyo itasogeza huduma za utoaji mikopo karibu na wananchi kwa kuanzisha ofisi ya kanda Zanzibar.

  Akisoma maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii kuhusu wizara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Margaret Sitta , alisema ili kuimarisha uwezo wa Serikali kuendelea kutoa mikopo kwa wanafunzi, Kamati yake ilishauri Serikali itafute mbinu mbadala za kupata fedha ili kuinua uwezo wa kutoa mikopo mwaka hadi mwaka.

  Alisema, ili kuimarisha urejeshwaji wa mikopo iliyotolewa tangu mwaka 2006, kiundwe chombo mahususi chini ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, ili kufuatilia ukusanywaji wa marejesho ya mikopo iliyokwishatolewa.

  Alisema, taarifa za mikopo husika zitambulike kwa walengwa ili kurahisisha ukusanyaji wa fedha hizo kwa ushirikiano wa mwajiri na Bodi ya Mikopo na kuwa fedha za marejesho ya mikopo hiyo zitambulike bayana, kwa kuonekana katika taarifa ya utekelezaji wa majukumu kila mwaka.

  Pia Kamati ilishauri utoaji vitambulisho vya Taifa ukamilike ili kutambua wanafunzi wanaokopa na waliokopa na uraia wao, ambapo pia Kamati ilishauri kuwapo udhibiti wa karo hasa katika vyuo visivyo vya Serikali.

  Mbunge wa Viti Maalumu, Diana Chilolo (CCM), alishauri kutokana na utata katika urejeshwaji wa mikopo, Serikali itoe fedha hizo bure kwa wanafunzi badala ya kuwakopesha.

  Akiwasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani, Msemaji Mkuu wa Kambi hiyo kwa Wizara ya hiyo Cristowaja Mtinda, alisema kutokana na muundo wa Bodi ya Mikopo na uendeshaji mbaya, kuna haja ikavunjwa kwani imeshindwa kuifanya elimu ya juu ipatikane kwa kila mwanafunzi anayestahili.

  Alisema Bodi hiyo ilitoa mikopo kwa wanafunzi 91,568 mwaka uliopita, lakini ilikusanya marejesho ya mikopo yenye thamani ya Sh. bilioni 7.9 kati ya Sh. bilioni 21 zilizotarajiwa kukusanywa.

  “Kutokana na sababu hizo, Serikali iazimie kuivunja Bodi hii, pamoja na kufanya uchunguzi huru wa fedha zilizotumika chini yake hadi sasa na kujiridhisha kama waliopewa dhamana hii hawakutumia nafasi zao kujinufaisha binafsi,” alisema.

  Alisema baada ya Bodi hiyo kuvunjwa, Serikali iunde chombo kipya kitakachojulikana kama Mamlaka ya Taifa ya Kugharimia Elimu ya Juu (TAHEFA), ambacho kitachukua majukumu yote ya Bodi.

  chanzo: HabariLeo | Posho elimu ya juu yapanda kwa Sh 2,500/-
   
 2. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Ni ongezeko la 50% tu bila shaka kima cha chini kitaongezeka kwa zaidi ya 50% unless the government applies the irrational decisions.
   
 3. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mwanafunzi posho 7500 * 30 = 225,000


  Mfanyakazi wa serikali: Net Salary 200,000
  1. Kodi ya nyumba
  2. Ada za Watoto
  3. Chakula cha familia
  4. Matibabu
  5. Umeme na Maji ...................................
  Kufanya kazi bongo yataka uzalendo wa hali ya juu.
  Afadhali ya Mkopo wa Chuo.
   
 4. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  soma hii

  inapatikana hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/156545-ongezeko-la-mshahara-kwa-wafanyakazi-wa-serikali.html
   
 5. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mkuu, hiyo net ya 200,000/- wanapata wangapi? hebu soma post #4 nne hapo juu kuna nyepesi nyepesi
   
 6. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mie yangu macho. Mtazamo wangu, tuangalie pia elimu ya huyo anayepokea kima cha chini serikalini.
   
 7. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2011
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  huo wa wanafunzi ni mkopo jamani.watalipa waacheni vijana wasome
   
 8. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Miss Judith hujambo dada!

  Kwa mtindo huu hata sie wazee wa siku nyingi itabidi tujifanye wanafunzi ili tupate udhamini wa serikali.

  Ndio maana hata mtoto wa rais anaishi kimjini mjini maana Tsh 149,850 utafanyia nini jamani kama sio kututia majaribuni kuomba rushwa.
  Ni heri Tsh 225,000 ya mwanafunzi ambayo hana pressure ya maisha
   
 9. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #9
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kama serikali imeona ya kuwa sh. 5,000 haimtoshi mwanafunzi wa chuo. Imeshindwa nini kuona ugumu wa maisha ya mfanyakazi wake mwenye familia.
   
 10. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #10
  Jul 20, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mi sijambo kabisa mpendwa,

  kwa kweli mambo mengine yanashangaza sana! imagine huyo mwanafunzi analelewa na mzazi mlezi aliyeko kwenye category ya kima cha chini, ina maana anamzidi kipato mzazi/mlezi wake anayemlea na cha kushangaza, chanzo cha mapato yao ni kimoja, SERIKALI!
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Bila ya kuwa mwizi au mdokozi kwa mshahara huo huwezi kuendesha maisha na ukayafrahia
   
 12. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #12
  Jul 20, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mwanafunzi akiwa chuoni kabla hajahitimu huwa ana elimu gani? kama ana elimu ya sekondari inashawishi kuwa ni haki amzidi mzazi/mlezi wake mwenye limu ya sekondari kama yeye na aliyeko kazini?
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Huyo mfanyakazi mwenye familia hajui kuandamana kuishinikiza serikali, inaonyesha anaridhika na hicho kipato kiduchu dili nyingi mtaani anapiga
   
 14. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #14
  Jul 20, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  ajabu!!!
   
 15. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #15
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tatizo wafanyakazi wa Tz wamezidi upole, na hofu ya kufukuzwa kazi.
   
 16. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #16
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Pasipo imani ni vigumu kuishi Tanzania.

  Serikali na taasisi zake ina baadhi ya watumishi watumishi wanakula na kusaza ili hali wengine wengi wakiangukia kwenye chini ya dola moja kwa siku.
   
 17. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #17
  Jul 20, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,382
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana watu wanapenda wawe wanafunzi wa vyuo milele!
   
 18. Jimjuls

  Jimjuls JF-Expert Member

  #18
  Jul 20, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 461
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Huo si mkopo tu.......utarudishwa tu jamani!!!!!!!!!!!!!!
   
 19. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #19
  Jul 20, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Miss J .. kumbuka hizi fedha wakopeshwa... toka bodi ya mikopo... so usijali kuhusu fedha wapewazo....
   
 20. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #20
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Basi ni vema na waalimu nao wapewe hii mikopo isiyokuwa na riba..., Hapa issue sio kwamba wanafunzi wanapata pesa nyingi.., issue ni kwamba waalimu hawapewi fedha za kutosha. Sasa kama serikali imetambua kwamba pesa hizo hazimtoshi mwanafunzi kujikimu, iweje idhani kwamba pesa pungufu ya hizo inamtosha mwalimu tena mwenye familia na majukumu zaidi?

  Bad enough ni kwamba huenda huyo huyo mwanafunzi atakuja kuwa mwalimu baadae.., so how are you preparing him for the future..., si huku ndio kuhalalisha rushwa...?, cause people have got to eat
   
Loading...