Mwanafunzi kizimbani kwa tuhuma za kutupa kichanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanafunzi kizimbani kwa tuhuma za kutupa kichanga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Sep 29, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Mwanafunzi kizimbani kwa tuhuma za kutupa kichanga Send to a friend Wednesday, 29 September 2010 09:17 0diggsdigg

  Joseph Lyimo, Mbulu

  JESHI la Polisi mkoani Manyara linamshikilia mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya sekondari Genda, wilayani Mbulu kwa tuhuma ya kukitupa kitoto kichanga ****** baada ya kuzaa.

  Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Parmena Sumary, mwanafunzi huyo ambaye hakutajwa jina lake anadaiwa kutupa kichanga hicho Septemba 23 saa 6:30 mchana.

  Sumary alisema kichanga hicho kiliokotwa na mtu mmoja kikiwa kizima wakati akipita karibu na choo hicho.

  Alisema baada ya kukiokota kichanga hicho mtu huyo alikipeleka hospitali ya wilaya hiyo kitoto hicho na jeshi hilo lilifanikiwa kumkamata mwanafunzi huyo.

  Mwanafunzi huyo alikiri kufanya kitendo hicho cha kutupa mtoto kwa madai kuwa alifanya hivyo ili aweze kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne utakaofanyika mwezi Oktoba.


  Kamanda Sumary alisema mwanafunzi huyo atafikishwa mahakamani muda wowote mara baada ya kutoka hospitalini hapo ambapo hadi hivi sasa amelazwa.
   
 2. Mnene 1

  Mnene 1 Senior Member

  #2
  Sep 29, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana kwa kiumbe ambacho hakina kosa kutelekezwa. Jambo la Msingi wampe huyo mwanafunzi ruhusa ya kufanya mitihani na baada ya mitihani ndio kesi yake iendelee. Ni mawazo yangu.
   
 3. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Inaonyesha haja ya msingi ya kutokukatisha elimu ya wanaopatwa na janga hili.

  Mabinti wakijua hawaachishwi shule pengine baadhi ya watoto watasalimika kutupwa.
   
 4. kisu

  kisu JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 802
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Elimu mbofu, Afya mbofu, Mazingira mbofu. We need change. Chagua SLAA 2010.
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  nasikitika kutoelewa hii post... sijui slaa atasababishaje watoto wadifanye mapenzi kabla ya muda na bila kinga??

  the problem is systemic and we need to address it comprehensively na sio kisiasa-siasa with one or two sweeping statements
   
Loading...