Mwanafunzi kizimbani kwa mauaji.....................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
202,854
2,000
Mwanafunzi kizimbani kwa mauaji

Wednesday, 08 December 2010 07:50 newsroom
NA HAPPINESS MWAMSYANI (DSJ)
MWANAFUNZI na mfanyabishara mmoja wa mjini Dar es Salaam, wamepandishwa kizimbani kujibu tuhuma za mauaji.
Mlenda Iddy (17) na Ramadhani Hamba (18), walipandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Wilaya Ilala, mbele ya Hakimu Mkazi Tarsila Kisoka. Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Naima Mwanga, alidai watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Novemba 21, mwaka huu, eneo la Majohe kwa Ngozoma, Dar es Salaam. Alidai watuhumiwa hao walimuua Omary Mwinyimvua, ambaye alikuwa ni mchezesha muziki (DJ) aliyekuwa akitoa burudani katika mkesha wa sherehe moja jirani na eneo la tukio. Naima alidai watuhumiwa hao walidaiwa kutumia panga, mawe na bisibisi na kutekeleza mauaji hayo yalitokea baada ya majibizano baina ya watuhumiwa na Mwinyimvua.
Ilidaiwa kuwa kabla ya mauaji hayo, watuhumiwa hao walimtuhumu Mwinyimvua kuwa aliwatukana na kuanza kumshambulia kwa kutumia silaha hizo. Watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwani, mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo. Kesi hiyo itatajwa Desemba 20, mwaka huu, watuhumiwa walirudishwa rumande na kwamba upelelezi bado unaendelea. Wakati huohuo, mkazi wa Ukonga Galus Anthony (35), alipandishwa kizimbani kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Mussa Gumbo, alidai mbele ya Hakimu Janet Kinyage, kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 26, mwaka huu, maeneo ya Posta mpya. Ilidaiwa kuwa Anthony akiwa na wenzake walimtapeli Anna Mwasha fedha taslimu sh. milioni 9.35. kwa madai kwamba, watamtolea magari yake mawili bandarini. Hata hivyo, mshitakiwa hakutekeleza makubaliano hayo na badala yake walitokomea mahali kusikojulikana. Mshitakiwa alikana shitaka na alirudishwa rumande baada ya kukosa wadhamini, kesi itatajwa Desemba 21, mwaka huu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom