Mwanafunzi Kavunjwa mguu ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanafunzi Kavunjwa mguu !

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nkyandwale, Mar 27, 2011.

 1. nkyandwale

  nkyandwale Member

  #1
  Mar 27, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  Ni mwanafunzi wa darasa la N'ne wa Shule ya Msingi Kawama katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa, Adamu Bilauli umri {11-13} ambaye alipigwa na kuvunjwa mguu wa kulia yapata wiki moja sasa.
  Ilikuwa muda wa jioni ambao Adamu na rafiki zake waliichukua pikipiki ya aliyemvunja mguu kuisukuma huku wakiipanda bila ya kuiwasha kwa kuisukuma huku kati yao mmoja akiwa amepanda katika hali ya kuichezea. pasi idhini ya mwenye mali. {jina la mwenye pikipiki polisi wanalo}
  Mwenye pikipiki akiwa ameingia ndani na hakujua ni kitu gani kiliendelea n'nje na wale watoto siwo wa familia yake, mara alipotoka n'nje hakuiona pikipiki alipoiweka na katika hali ya kuitafuta aligundua mwelekeo wa pikipiki alipofuatilia aliwaona watoto hao zaidi ya watatu wakiichezea.
  Wale watoto wengine walipomwona mwenye pikipiki walifanikiwa kukimbia, Adamu hakumudu mbio, alikamatwa na kucharazwa bakora halafu alichukuliwa mkumku hadi nyumbani kwa mwenye pikipiki ambako kazi ya kumvunja mguu Mwanafunzi Adamu ilifanyika kwa kupondaponda kwa kutumia kitu kigumu bila kujali utu!. Masikini Adamu sasa anatembelea magongo mchezo umemponza mbaya!
  Baada ya hatua ya kipolisi Adamu amefungiwa muhogo {P.O.P} na anatuhumiwa kuhusishwa na njama ya kuiba kifaa hicho cha usafiri. kwa dhana kuwa baadhi ya wezi huwatumia watoto katika kufanikisha shughuli za wezi kwa kuwalaghai na kuwapa vitu wavipendavyo watoto na wao bila ya kujitambua kuwa hujiingiza katika kaa la moto.
  Wanahaki za binadamu angalieni uhalali wa jambo hili, bado wenye nguvu hujichukulia sheria mkononi za kuwatenda watakavyo wale wanaonekana kuwa na hatia kabla ya hukumu ya kisheria. :smash:
   
Loading...