Sine r Winters
Senior Member
- Jul 10, 2012
- 110
- 15
Kuiona cheki hapo social network udom. Hongera sana UDOM. Mungu ibariki UDOM, Mungu ibariki Tanzania.
Salamu wana Jamvi!
Jana katika tupiatupia macho kurasa za magazeti nikajikuta katika kurasa moja ya makala ya gazeti la "Mwananchi" ikiwa na kichwa cha habari kama nilivyokiandika katika "Title" yangu. Nilivyoshawishika kuisoma habari hiyo nikagundua kumbe vyuo vyetu vinaweza kuzalisha vijana ambao wana mawazo ya kujiajiri.
Huyu kijana ameanzisha "mtandao wa kijamii" kama ilivyo kwa "facebook" (Welcome to Mayocoo - Sign in, Sign up). Na kwa jinsi alivyoelezea, anadai inamambo mengi na salama hata zaidi ya hiyo "facebook".
Mimi nimefarijika (ingawa ni duplication ya idea).
Ombi langu kwa viwanda hivi (Vyuo), watazame zaidi mihula yao ili si tu hawa "mazalia" waweze kutengeneza vitu ambavyo tayari vipo, ila wawe na uwezo wa kufikiri na kuja na idea mpya. Na pia naamini vyuo vinaweza kuanzisha miradi ya kuwasaidia vijana ambao wanafungua njia za kujitemea. Ni rahisi kwa vyuo kutambua umuhimu wa mawazo ya wahitimu wao kuliko "taasisi" nyingine.
Mwisho: Kuzalisha wahitimu wenye mawazo ya kujiajiri inawezekana.