Mwanafunzi azidiwa na kukimbizwa hospitali baada ya mwalimu kumchapa viboko 10

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi madeke halmashauri ya wilaya ya njombe mwenye umri wa miaka 10 inadaiwa kuwa anaendelea kuugulia maumivu ya adhabu ya kuchapwa viboko visivyopungua 10 na mwalimu wake wa hesabu baada ya kufeli somo hilo hapo machi 21 mwaka huu

Kwa mujibu wa baba mzazi wa mtoto huyo Bonface Manga Kwa masharti ya kutorekodiwa na waandishi mwanae Hosea Manga alichapwa viboko kumi na mwalimu wake na kisha akazidiwa na kukimbizwa hospitali.

Kutoka hospitali ya teule ya Mkoa wa Njombe Kibena ambako mtoto huyo amelazwa hali yake bado ingali si nzuri kwa kuwa hawezi kusimama wala kutembea licha ya kaimu mganga mfawidhi Wa hospitali hiyo Isaya mvinge kueleza kuwa uchunguzi wa kitabibu bado unaendelea

Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe Kupitia Mkurugenzi Mtendaji monica kwiluvya anakiri kupokea taarifa kwa njia ya simu kutoka kwa afisa elimu kata kuwa mwalimu aliyehusika anashikiliwa na polisi

Jitihada za kupata taarifa ya jeshi la polisi zimegonga mwamba baada a kamanda wa jeshi la polisi kueleza kuwa yuko nje ya mkoa kikazi.

Chanzo: ITV
 
Hapa kazi tuu... Kila mtu ni kambare..baba anandevu watoto wanandevu basi ni vurugu tupu... Hayo ndo majibu yake
 
Uonevu haufai... Ila huyo dogo nae mzembe tu... Viboko kumi hoi!?

Enzi zile unadundwa viboko 30 kila kona ya mwili afu mwanaume unanyanyuka unarudi zako back benches.
 
Hunipigii mwanangu kihivyo halafu nikuache tu.

Nitakuua kwa mikono yangu mwenyewe.

Hii ilikuwa kawaida kwa aina fulan ya wanafunz, na walikuwa hawatoi hata chozi! Sometimes hata kama hujafanya kosa adhabu itakukumba tu coz its in ur DNA kuwa mkosoj
 
zama zetu walimu wa madarasa hayo walikuwa ni watu wazima, kwa leo usishangae kwa kichapo hicho ni mwl kijana ambae hata barehe bado.
 
Mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi madeke halmashauri ya wilaya ya njombe mwenye umri wa miaka 10 inadaiwa kuwa anaendelea kuugulia maumivu ya adhabu ya kuchapwa viboko visivyopungua 10 na mwalimu wake wa hesabu baada ya kufeli somo hilo hapo machi 21 mwaka huu

Kwa mujibu wa baba mzazi wa mtoto huyo Bonface Manga Kwa masharti ya kutorekodiwa na waandishi mwanae Hosea Manga alichapwa viboko kumi na mwalimu wake na kisha akazidiwa na kukimbizwa hospitali.

Kutoka hospitali ya teule ya Mkoa wa Njombe Kibena ambako mtoto huyo amelazwa hali yake bado ingali si nzuri kwa kuwa hawezi kusimama wala kutembea licha ya kaimu mganga mfawidhi Wa hospitali hiyo Isaya mvinge kueleza kuwa uchunguzi wa kitabibu bado unaendelea

Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe Kupitia Mkurugenzi Mtendaji monica kwiluvya anakiri kupokea taarifa kwa njia ya simu kutoka kwa afisa elimu kata kuwa mwalimu aliyehusika anashikiliwa na polisi

Jitihada za kupata taarifa ya jeshi la polisi zimegonga mwamba baada a kamanda wa jeshi la polisi kueleza kuwa yuko nje ya mkoa kikazi.

Chanzo: ITV
Mbona zamani tulikuwa tunachapwa zaid hata ya hivo viboko? Watoto wa siku hizi nao shida. Nishawahi kuchapwa zaid ya viboko kumi mimi. Hatuwezi kujua mwanafunza alimfanyia nini mwalimu?
 
Huyo dogo nae mlaini sana!! Viboko kumi tu unaenda hospital?? Enzi zetu ulikua unapigwa mpaka walimu wanachoka ndio unaachwa...ma bado tumedunda mpaka chuo na kumaliza!!

Au hili litakua tukio jipya baada ya lile la bandarini kufeli?
 
Juzi tu ilikuwa Tanga,Mwalimu kampiga mwanafunzi mpaka akapooza,akapelekwa hospital ya mkoa,ikashindikana,akapewa rufaa Muhimbili.Na kabla ya hapo,ilikuwa Mbeya.
Hawa waalimu,akili zao ziko vipi?
 
Kama ni mtoto wa miaka kumi kaonewa sanaa
Huyo mwalimu achukuliwe hatua
 
Kinacho nishangazaga Mimi jamani eti kati ya polidi na mwalimu Mani anajua kupiga? Mbona mwanafunzi akipigwa na polisi huwa hazidiwi? Akipigwa na MWL ndo huwa anazidiwa.duuu ndo maana cku hizi sichapi
 
Back
Top Bottom