Mwanafunzi auawa na mamba akioga Ziwa Victoria

OKTOBA 13, 2019

Kutokea Sengerema Mwanza.

Mwanafunzi wa Darasa la sita katika Shule ya Msingi Itabagumba Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza Tanzania, Magesa Beseko (12) amekufa baada ya kuliwa na mamba alipokuwa akioga ziwani.

Tukio limetokea Oktoba 11, 2019 saa 12 jioni katika Kitongoji cha Msuswiga kilichopo katika kijiji cha Bulyaheke B Wilayani Sengerema.

Mwanafunzi huyo alienda eneo hilo kwa lengo la kumwagilia bustani ya nyanya inayomilikiwa na baba yake na alipomaliza shughuli hiyo, akaamua kwenda kuoga ziwani.

Baba wa mtoto huyo, Biseko Kapunda aliliambia Mwananchi kuwa maiti ya mwanawe bado haijapatikana.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji Cha Bulyaheke B, Barenadetha Sandu alilithibitishia Mwananchi kutokea kwa kifo hicho na amesema hadi sasa mabaki ya mwili wa mwanafunzi huyo hayajapatikana na wakazi wa eneo hilo kwa kushirikiana na askari wa wanyamapori wanaendelea kutafuta.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Itabagumba Maimuna Hamis amesema kuwa mwanafunzi aliyekubwa na mauti yao anasoma katika shule hiyo Darasa ya sita na amepokea kwa masikitiko juu ya tukio hilo.

MCL
 
Sasa kama mabaki ya mwili hayajapatikana na hamsemi kama kuna ishara inayoonyesha kuliwa na mamba mmethibitishaje kwamba ameliwa na mamba?
 
Back
Top Bottom