Haha MEMKWA Tena Mkuu.Miaka 27 yupo second year... Tatzo la memkwa hili..
Hii Habari ni ya mwaka 2009 hebu angalieni vizuri hilo jina la huyu dada...MWANAFUNZJ wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Elimu (Duce), jijini Dar es Salaam, Bertha Mwarabu (23), ameuawa na mwanafunzi mwenzake kwa kuchomwa kisu kwenye titi na tumboni kwa kinachodaiwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika hosteli za chuo hicho zilizopo Mabibo, jijini Dar es Salaam.
Kamanda Kalunguyeye amemtaja mtuhumiwa wa mauaji hayo kuwa ni Masamba Musiba (27) ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo hicho, ambacho ni sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Amesema mauaji hayo yalitokea juzi saa 3:45 usiku baada ya Musiba kuingia chumbani kwa marehemu ambaye inadaiwa alikuwa mpenzi wake na kuanza kumshambulia kwa kisu.
Ameongeza kuwa baada ya marehemu kuanza kushambuliwa, alipiga kelele kuomba msaada na ndipo wanafunzi wenzake walipokwenda na kumkamata mtuhumiwa wakati akijaribu kukimbia.
Amesema kelele za marehemu, ndizo zilizowashtua wanafunzi wenzake.
Kamanda Kalunguyeye alifafanua kuwa marehemu alikimbizwa hospitali kupatiwa matibabu lakini alifia njiani.
Mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, amesema tukio la mauaji hayo ni la kwanza kutokea chuoni hapo.
Profesa Mukandala alisema tangu aanze kufanya kazi chuoni hapo kwa miaka mingi, hajawahi kushuhudia tukio la namna hiyo na kuongeza kuwa amesikitika kwa kuondokewa na mwananfunzi huyo.
Ni mpenzi wake lakini sababu inaweza isiwe papuch! af tambua kwamba sheria ni ngumu, ngumu, ngumu mno. hiyo kesi inaweza kuwa first degree murder au ghafra ikawa mauaji ya bila kukusudia. maelezo tu na ushahidi! unaweza shangaa kafungwa miaka mitano tu akatoka baada ya mwaka for good conduct.Adhabu ya kifo isifutwe ili itumike kwa watu kama hawa papuchi tu unamtoa uhai mwenzio
Mbona unapotosha?Hii habari ni ya mwaka
Hii Habari ni ya mwaka 2009 hebu angalieni vizuri hilo jina la huyu dada...
Nadhani umeiona na mods wameamua wauanganishe..Sijui umeokota wapi hii habari...Mbona unapotosha?
Hili tukio ni la mwaka 2009Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Elimu (Duce), jijini Dar es Salaam, Bertha Mwarabu (23), ameuawa na mwanafunzi mwenzake kwa kuchomwa kisu kwenye titi na tumboni kwa kinachodaiwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika hosteli za chuo hicho zilizopo Mabibo, jijini Dar es Salaam.
Kamanda Kalunguyeye alimtaja mtuhumiwa wa mauaji hayo kuwa ni Masamba Musiba (27) ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo hicho, ambacho ni sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Alisema mauaji hayo yalitokea juzi saa 3:45 usiku baada ya Musiba kuingia chumbani kwa marehemu ambaye inadaiwa alikuwa mpenzi wake na kuanza kumshambulia kwa kisu. Aliongeza kuwa baada ya marehemu kuanza kushambuliwa, alipiga kelele kuomba msaada na ndipo wanafunzi wenzake walipokwenda na kumkamata mtuhumiwa wakati akijaribu kukimbia.
Alisema kelele za marehemu, ndizo zilizowashtua wanafunzi wenzake.
Kamanda Kalunguyeye alifafanua kuwa marehemu alikimbizwa hospitali kupatiwa matibabu lakini alifia njiani.
Mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, alisema tukio la mauaji hayo ni la kwanza kutokea chuoni hapo.
Profesa Mukandala alisema tangu aanze kufanya kazi chuoni hapo kwa miaka mingi, hajawahi kushuhudia tukio la namna hiyo na kuongeza kuwa amesikitika kwa kuondokewa na mwananfunzi huyo.