Mwanafunzi auawa Mabibo Hostel | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanafunzi auawa Mabibo Hostel

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Kaniki1974, Jun 7, 2009.

 1. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuna tetesi kwamba mwanafunzi wa kike aishiye Mabibo hostel kauawa na mpenzi wake kwa kuchomwa kisu usiku huu. Pia mtuhumiwa kuuwa kapigwa sana na wanafunzi wenziwe. Ka inzi huko au wenye taarifa zaidi watuhabarishe zaidi.

  Nawasilisha.

  =================

  Mwanafunzi UDSM amuua mwenzake kwa wivu wa mapenzi

  Richard Makore


  Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Elimu (Duce), jijini Dar es Salaam, Bertha Mwarabu (23), ameuawa na mwanafunzi mwenzake kwa kuchomwa kisu kwenye titi na tumboni kwa kinachodaiwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.

  Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika hosteli za chuo hicho zilizopo Mabibo, jijini Dar es Salaam.

  Kamanda Kalunguyeye alimtaja mtuhumiwa wa mauaji hayo kuwa ni Masamba Musiba (27) ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo hicho, ambacho ni sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

  Alisema mauaji hayo yalitokea juzi saa 3:45 usiku baada ya Musiba kuingia chumbani kwa marehemu ambaye inadaiwa alikuwa mpenzi wake na kuanza kumshambulia kwa kisu. Aliongeza kuwa baada ya marehemu kuanza kushambuliwa, alipiga kelele kuomba msaada na ndipo wanafunzi wenzake walipokwenda na kumkamata mtuhumiwa wakati akijaribu kukimbia.

  Alisema kelele za marehemu, ndizo zilizowashtua wanafunzi wenzake.

  Kamanda Kalunguyeye alifafanua kuwa marehemu alikimbizwa hospitali kupatiwa matibabu lakini alifia njiani.

  Mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.

  Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, alisema tukio la mauaji hayo ni la kwanza kutokea chuoni hapo.

  Profesa Mukandala alisema tangu aanze kufanya kazi chuoni hapo kwa miaka mingi, hajawahi kushuhudia tukio la namna hiyo na kuongeza kuwa amesikitika kwa kuondokewa na mwananfunzi huyo.


  Chanzo: Nipashe
   
 2. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Sad news
   
 3. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2009
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Yote hayo sabu ni hiyo sehemu ndogo kabisa hata Robo wakiya haifiki
   
 4. Kimori

  Kimori JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2009
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Du! It's very SAD to hear that!
   
 5. Mhache

  Mhache JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2009
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hilo ni jambo la kuhuzunisha kama ni kweli kuuawa kwa huyo msomi. Kulikuwa na nini hadi kifo kumkuta huyo msomi? Vijana yulinde hasira zetu, kila mtu ana haki ya kuishi.
   
 6. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2009
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Maranyingi mauaji ya kusudia yanatokana na vitu viwili:
  1. Mambo ya Mapenzi
  2. Mambo ya Siasa

  Ili rare cases
  3. Mambo ya kugombea madaraka au vyeo including siasa
  4. Visasi

  So sad!
   
 7. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  jamani hiyo ni tetesi tu, kama kuna mwenye data amwage basi hapa janvini ili tuchangie kwa ufasaha tukijua chamzo cha hayo mauhaji
   
 8. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #8
  Jun 7, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kuna mwanafunzi ameuwawa na mwanafunzi mwenzake kule mabibo
   
 9. Kweli

  Kweli JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,124
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  So sad! vitu kama hivi ni nadra kusikia vimetokea kwetu, tumezowea kusikia haya matukio kila siku ughaibuni
   
 10. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Nakuunga mkono Allien, Kwa pale mabibo hostel au kwenye vyuo vikuu kwa ujumla swala la mapenzi lisababisha vifo vya wanafunzi wengi. Kuna vifo vya watu watatu vilivyotokea katika miaka tofauti kwa kipindi cha miaka minne niliyokuwa pale, ambavyo vilisababishwa na mambo ya mapenzi.
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa nini uongozi wa chuo hadi sasa haujatoa taarfa yoyote kwa umma?
   
 12. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #12
  Jun 7, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Labda weekend haijaisha msemaji hayuko kazini
   
 13. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mwanafunzi UDSM amuua mwenzake kwa wivu wa mapenzi

  Richard Makore

  Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Elimu (Duce), jijini Dar es Salaam, Bertha Mwarabu (23), ameuawa na mwanafunzi mwenzake kwa kuchomwa kisu kwenye titi na tumboni kwa kinachodaiwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.

  Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika hosteli za chuo hicho zilizopo Mabibo, jijini Dar es Salaam.

  Kamanda Kalunguyeye alimtaja mtuhumiwa wa mauaji hayo kuwa ni Masamba Musiba (27) ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo hicho, ambacho ni sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

  Alisema mauaji hayo yalitokea juzi saa 3:45 usiku baada ya Musiba kuingia chumbani kwa marehemu ambaye inadaiwa alikuwa mpenzi wake na kuanza kumshambulia kwa kisu. Aliongeza kuwa baada ya marehemu kuanza kushambuliwa, alipiga kelele kuomba msaada na ndipo wanafunzi wenzake walipokwenda na kumkamata mtuhumiwa wakati akijaribu kukimbia.

  Alisema kelele za marehemu, ndizo zilizowashtua wanafunzi wenzake.

  Kamanda Kalunguyeye alifafanua kuwa marehemu alikimbizwa hospitali kupatiwa matibabu lakini alifia njiani.

  Mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.

  Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, alisema tukio la mauaji hayo ni la kwanza kutokea chuoni hapo.

  Profesa Mukandala alisema tangu aanze kufanya kazi chuoni hapo kwa miaka mingi, hajawahi kushuhudia tukio la namna hiyo na kuongeza kuwa amesikitika kwa kuondokewa na mwananfunzi huyo.
  Souce: NIPASHE
   
 14. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  so sad ni kwamba, Dr. Isack Ndodi alikuwa nao ijumaa kuzungumzia mambo hayo hayo ya mapenzi kabla ya ndoa na wakati wa uchumba. Jumamosi mauaji yakatokea. Hii inathibitisha kuwa wabongo wengi tunaendeshwa na hisia pamoja na silika zaidi kuliko akili.
   
 15. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Taabu unakuta demu wa chuo ana mabwana wengi..ana mchumba, ana kipanga wa kumsaidia shule na ana father ATM!!!

  Hapo ndo kazi ipo!!!
   
 16. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #16
  Jun 8, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  KWa mujibu wa marafiki za marehemu, inasemekana walikuwa marafiki tangu wako A level Morogoro, na hadi chuo uhusiano ukaendelea,
  Ila marehemu alikuwa analalamika kwamba mpenzi wake ni mlevi sana na anavuta madawa ila hawakusema ni madawa gani, ndo marahemu akaamua kumuacha na kuwa na jamaa mwingine, na kama unavyojua mtuhumiwa alikuwa ni mtu wa msoma hasira na hakutaka kuachwa ndo akaamua amuue wakose wote, na alifanya hivyo wanafunzi wengine wakiwa kwenye paty kwenye hall hapo jirani. (kwa mujibu wa gazeti la Daily News)
   
 17. R

  REOLASTON Member

  #17
  Jun 8, 2009
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Du so sad wajamen.
   
 18. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #18
  Jun 8, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  MAPENZI jamani ni HATARI! una jua mwenzako anakapo kukabizi funguo za moyo wake na hisia zake,halafu unamvuruga mara nyingi watu huwa wanashindwa kujizuia ma matokeo yake huwa kama hivi.Jamani tuwe makini sana na hasira zetu zisije tufikisha pabaya.jamaa ndo asahau tena swala la masomo hapo,kitu kidogo tu kimearibu maisha ya watu.eeh mungu tuepushe na haya mabalaaa AMINI.
   
 19. Kaka Mkubwa

  Kaka Mkubwa Senior Member

  #19
  Jun 8, 2009
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 154
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  MWANAFUNZI mmoja wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu Dar es Salaam (DUCE), ameuawa kwa kuchomwa kisu mara nne na mwanafunzi mwenzake kwa madai ya wivu wa mapenzi.

  Inadaiwa mwanafunzi huyo, Bertha Mwarabu, 23, wa mwaka wa pili, alitofautiana na mpenzi wake, Masamba Musiba, 27, katika masuala ya mapenzi wakiwa katika hosteli ya wanafunzi wa Chuo Kikuu iliyopo Mabibo.

  Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 2:30 usiku kwenye varanda ya Jengo 'C' la hosteli hiyo linalotumiwa na wanafunzi wa kike na kiume, lakini mauaji yalifanyika katika upande wa wanawake.

  Kamanda wa Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Bertha alifariki njiani wakati akipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Mwananyamala.

  Kalunguyeye alisema baada ya tukio hilo, Musiba alijeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa na wanafunzi wengine na hivyo kukimbizwa katika hospitali hiyo hiyo kwa matibabu.

  "Musiba anashikiliwa na polisi katika kituo kidogo cha polisi, Mbezi jijini hapa," alisema Kalunguyeye.

  Inadaiwa Musiba alifanya tukio hilo baada ya marehemu Bertha kuvunja uhusiano wao wa kimapenzi.

  Kwa mujibu wa habari kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo, Musiba alichukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa Bertha ameanzisha uhusiano mpya wa kimapenzi na mwanamume mwingine.

  "Baada ya Musiba kubaini hilo, aliamua kumwadhibu. Alimchoma kisu mara nne, kimoja katika ziwa la upande wa kushoto, mara mbili tumboni na kusababisha utumbo kutokeza nje na kingine alimchoma kifuani. Kisu hicho kilipinda na mpini wake ukaanguka chini," alisema shuhuda huyo ambaye alikataa jina lake kuandikwa gazetini.

  Habari zaidi zinasema wakati tukio linatokea, wanafunzi wengi walikuwa nje ya hosteli na hasa kwenye kiwanja cha mpira kilichopo eneo hilo wakiangalia tamasha la muziki.

  Habari zinasema kabla ya kumshambulia kwa kisu msichana huyo, Musiba alimwita Bertha kwa ajili ya maongezi ambayo alitaka yafanyike ndani ya chumba ambacho msichana huyo alikuwa akiishi na wenzake watatu. Ilikuwa majira ya saa 2:00 usiku.

  Wakati huo, Bertha alikuwa ametoka kujiandaa kwenda kuimba kwaya kwa ajili ya mazoezi ya Jumapili. Alikuwa ni mwanakwaya ya kanisa moja la Roma lililopo Bunju wilayani Kinondoni.

  "Ndipo akaitikia wito na wakakutana chumbani humo. Waliyoyazungumza hatukuweza kuyajua, lakini ghafla tulisikia kelele za mwanamke na tulipofika tulimkuta Bertha akiwa amejiegemeza kwenye ukuta na damu nyingi zikiwa zimetapakaa koridoni huku akiwa ameshikilia sehemu ya utumbo ambao ulikuwa umejitokeza nje," alisema.

  Mpashaji habari huyo alisema, Bertha alifanikiwa kuchoropoka chumbani mara baada ya kuonyeshwa kisu na alidondoka kwenye korido hiyo na ndipo zahama yote ikamkuta.

  "Kuna dada mmoja alikuwa chumba kingine ambaye alisikia purukushani na alipochungulia akamwona Bertha anagaragara chini, ndipo alipoanza kupiga kelele za kuomba msaada," alisema.

  Baada ya kufanya tukio hilo, Musiba alitokea kwenye moja ya dirisha na kuanza kukimbia, lakini baadhi ya wanafunzi waliokuwa chini ya ghorofa hilo walidhani kuwa ni mwizi na wakamkamata na kumpa kipigo.

  Inaelezwa kuwa matatizo ya kutoelewana kati ya wawili hao yalianza baada ya Bertha kubaini Musiba anatumia vilevi vya pombe, bangi na sigara.

  Inadaiwa kuwa Bertha alimkataza kuendelea kutumia vilevi hiyo kama alikuwa na nia ya kuendelea kuwa mpenzi wake, lakini hakujirekebisha.

  "Bertha alimpa miezi mitatu ili jamaa aache kuvuta sigara, bangi na kunywa pombe, lakini jamaa alishindwa masharti hayo na ndipo uhusiano wao ukavunjika," alidai mpashaji huyo.

  Taarifa tulizozipata kutoka kwa mtu wa karibu na Musiba zilidai kuwa, kabla ya kufanya tukio hilo, alinunua kisu kipya na alikusanya vitu vyake ikiwemo nguo katika mfuko.

  "Juzi alinunua kisu kipya na alipakia vitu vyake kwenye mfuko aina ya 'Volcano'. Wakati huo mimi nilikuwa sijui ana lengo gani" alisema mtu huyo bila kutaja jina lake.

  Uchunguzi unaonyesha kuwa, Musiba ni mwenyeji wa wilaya ya Musoma mkoani Mara, wakati Bertha ni mwenyeji wa Mkoa wa Morogoro.


  Source:
  Mwananchi 08/06/2009
   
 20. ram

  ram JF-Expert Member

  #20
  Jun 8, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,197
  Likes Received: 899
  Trophy Points: 280
  Ni kweli amekufa, chanzo ni wivu wa kimapenzi
   
Loading...