Mwanafunzi asimamishwa kwa kuwaroga wenzake, walimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanafunzi asimamishwa kwa kuwaroga wenzake, walimu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BIN BOR, Jan 27, 2011.

 1. BIN BOR

  BIN BOR JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  MWANAFUNZI wa Shule ya Msingi Liwiti Tabata jijini Dar es Salaam (jina tunalo) amesimamishwa masomo baada ya kukiri kuwa mshirikina na kwamba alikuwa akiwaroga walimu na wanafunzi wenzake.

  Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Simeon Kawa alisema shuleni hapo jana kuwa walilazimika kumsimamisha masomo mwanafunzi huyo baada ya wenzake kumkataa darasani na kwamba atalazimika kukaa nyumbani hadi suala lake litakapojadiliwa na kikao cha kamati ya shule na wazazi.

  "Kwanza tulimtuma akamlete mlezi wake na leo amekuja na bibi yake na amekiri kuhusika na vitendo vya kishirikina hapa shuleni,"alisema Kawa.

  Kutokana na hali hiyo, uongozi wa Manispaa ya Ilala wameagiza mtoto huyo achunguzwe afya ili kujiridhisha kama ana matatizo yoyote ya akili.

  Tukio la mwanafunzi huyo kudaiwa kuroga wenzake liligunduliwa na mmoja wa walimu wanaomfundisha shuleni hapo Mwalimu Mary Mwalongo ambaye alisema mara kwa mara mwanafunzi huyo awapo darasani huinamisha kichwa chini na hata anapoulizwa swali huwa hajibu. "Yaani ametupa shida tangu alipokuwa darasa la kwanza na hadi sasa hajui kusoma wakati wote akiwa darasani anainamisha kichwa chini na hata ukimuuliza swali hajibu anakaa kimya tu.

  "Juzi nilimuuliza swali hakujibu, nikamwambia tena arudie kusema jibu walilojibu wenzake, lakini alikaa kimya tu, nikawauliza wenzake mbona Rehema haongei,? wakasema anaongea ila ni mchawi,"alisema Mwalongo.

  more from mwananchi newspaper (leo)
   
Loading...