Mwanafunzi apandishwa kizimbani kwa tuhuma za kubaka na kumpa mimba mwanafunzi mwenzake

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
636
1,000
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Songwe, imempandisha kizimbani Chrispin Kibona (18) mwanafunzi wa kidato cha pili Idigima Sekondari, kwa tuhuma za kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake miaka wa 17.

Akisomewa mashtaka hayo Mahakamani hapo na Mwendesha Mashitaka wa Serikali Gibson Tawale mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Neemes Chami, amesema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Januari 19, 2019, saa sita mchana, katika kijiji cha Iyula Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, ambapo alimbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake wa kidato cha pili mwenye umri wa miaka 17.

Aidha Mwendesha mashita wa Serikali Gibson ameongeza kuwa aliyepewa ujauzito na alimpatia wote walikuwa wanafunzi wa Shule Sekondari Idigima kidato cha pili, ambapo upelelezi wa tukio hilo umekaamilika.

Kwa upande wake mtuhumiwa huyo wa ubakaji mwenye umri wa miaka 18 amekana shtaka hilo na Hakimu wa Mahakama hiyo Neemes Chami, amehairisha hadi tarehe 10 mwezi wa 12 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa tena.
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
24,085
2,000
Ukiona mtu alibakwa akapata Mimba kwenye huo ubakaji tafakari Mara mbili
Mwanamke akiwa kwenye kipindi cha kupata ujauzito anakuwa na hamu sana sasa inawezekana yeye ndio alijigonga gonga jamaa akakosea kusoma Signal akafanya kweli
 

Ezekiel Mbaga

JF-Expert Member
May 28, 2018
9,508
2,000
Sidhani kama kulikuwa na ushahidi wa kubakwa, au mimba ilionekana siku hiyo hiyo alivyobakwa?
 

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
13,875
2,000
Upuuzi yaani kamekubali kakaonesha ushiriano kitandani kisa kapo -18 wanasema UMEBAKA!!
 

ROGATH MCHAU

JF-Expert Member
Jan 17, 2017
469
1,000
MIAKA 18 FORM TWO? IPO KAZI, HAPO KIJANA WA KIUME WALA HAJAUFAIDI UJANA NA WA KIKE HIVYO HIVYO ANAKUA MAMA MAPEMAAAA!!!!
 

boga la kiangazi

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
505
1,000
Wanaume tunaonewa sana sana Wallah.Yaani mnagegedana watu hawajui ila ikitokea mimba ndiyo unakua umebaka,unakuta katoto ndiyo kalikua kanatoroka kwao kanakuja geto.

sisi pia ni binadamu sio kutufanyia uonevu mkubwa hivyo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom