Mwanafunzi akutwa amekufa kwa kutoa mimba ktk chumba cha mwanafunzi wa chuo

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
MWANAFUNZI ATUKWA AMEKUFA KWA KUTOA MIMBA KTK CHUMBA CHA MWANAFUNZI WA CHUO

Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Iringa aliyetambuliwa kwa jina la Yasinta Kasuga amekutwa amekufa eneo la Ngome katika Manispaa ya Iringa akiwa ndani ya chumba cha kijana ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Tumaini mjini Iringa.

Taarifa za mashuhuda wa tukio hilo ambao wameteta na mtandao huu wa Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima wamedai kuwa mwanafunzi huyo alikuwa akifika katika nyumba ya mwanafunzi huyo mara kwa mara na wamekuwa wakiishi kama mke na mume japo wote ni wanafunzi.

Hivyo walisema kuwa kutokana na mazoea hayo walichukulia watu hao kama ni wapenzi na kuwa hata siku ya tukio walipotapa taarifa ya mwanafunzi huyo kufa walitegemea kijana huyo kuwajulisha ila cha kushangaza kijana huyo hakupata kuonekana kabisa na badaal yake kuutelekeza mwili wa mwanafunzi huyo katika chumba chake.

Jeshi la polisi mkoa wa Iringa kupitia kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Evarist Mangalla (pichani) limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa katika chumba hicho walikuta dripu na dawa nyingine ambazo zinaonyesha kuwa mwanafunzi huyo kifo chake kimetokana na kutaka kujaribu kutoa mimba.
 
Back
Top Bottom